Nimeamua kurudi CCM

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Wahenga wanasema chanda chema huvikwa pete,na hili limethibika kuwa Ccm ni chanda chema kwa watanzania.

Niliamua kujiunga na Nccr Mageuzi nikiwa na imani kuwa ni chama ambacho kitakuwa mbadala wa kuiondoa Ccm na kukamata dola.

Ila kuna jambo moja limenifanya nirudi Ccm na hili ni kupambana na ufisadi,kisha pesa zilizokuwa zinaporwa na mafisadi kutumika kuwaletea maendeleo watanzania. Maana sekta ya afya,elimu,miundo mbinu na kila sekta imeimarishwa.

Ila jambo moja muhimu ni kuokoa zaidi ya bil 719 ambazo Iptl na Agreco walikuwa wanalipwa kila mwaka bila sababu ya msingi. Maaana sasa hakuna kampuni kama Iptl au Agreco ambayo inalipwa hizi fedha kifisadi na hakuna mgao wa umeme wala hakuna deal za kupiga pesa kama Richmond n.k.

Kwa ufupi zimebaki siku tano na kwenye karatasi ya kupigia kura Ccm ni namba moja,kwa hiyo naweka tick kwa Ccm na huku chini sipotezi muda kuangalia tena.
 
Hata mimi nitajiunga CCM iwapo watatolewa mafichoni walioiba au walioficha hii trilioni 1.5 ambayo alisema CAG haipo kwenye mahesabu ya matumizi ingawaje inakosekana kwenye mfuko wa Serikali.

1603377043882.png
 
Hizo hela zilizokuwa zinapigwa kifisadi na hao Agreco na Richmond zilikua zikipigwa na Serikali ya NCCR Mageuzi au ni ya CCM hiyo hiyo?

Unafiki siyo kitu kizuri. Hakuna mtu wa kukupangia kujiunga au kuwa mfuasi wa chama chochote kile. Ika siyo haki kukihusisha chama kingine na makosa ya chama kingine, ili tu kufanikisha matakwa yako.
 
Hizo hela zilizokuwa zinapigwa kifisadi na hao Agreco na Richmond zilikua zikipigwa na Serikali ya NCCR Mageuzi au ni ya CCM hiyo hiyo?

Unafiki siyo kitu kizuri. Hakuna mtu wa kukupangia kujiunga au kuwa mfuasi wa chama chochote kile. Ika siyo haki kukihusisha chama kingine na makosa ya chama kingine, ili tu kufanikisha matakwa yako.
Ccm huwa inajitathimini ikifanya makosa, na huwa inajirekebisha,ndio maana wamiliki wa Iptl wapo lupango kwa kufanya ufisadi.
 
Usibadilishe chama tu, badilisha jina (changudoa wa malude) ambalo linaweza kukujengea tabia sambamba na jina hilo, kwa sababu kwa Mtu unayejulikana ni ccm damu siku zote, kuandika kwamba unahamia leo, ni uchangudoa!
 
Back
Top Bottom