Adiya5
Member
- Jun 5, 2025
- 92
- 227
Watanzania wenzangu, Mungu aliumba watu wawili wawili waweze kuishi na kufanya maisha pamoja ikitokea mtu yupo peke yake kiasili kuna kitu utakiona hakipo sawa, hautakua na furaha ile inayotakiwa hata kama nje utaonesha furaha, utajihisi mpweke muda wowote hata kama umezungukwa na watu, maisha yako ya kila siku utajihisi kama kuna kitu mwilini mwako kimetolewa au kimekosekana,
Ukiona wapendanao wakitembea barabarani wameshikana mikono au wamebebeana pochi au wanasogezeana kiti au wanafunguliana mlango au wapo beach wamepakatana na kulishana kwa furaha unajiuliza mimi nilikosea wapi hapa duniani?
Pia kuna ule uoga wa umri, unawaza inamaana mimi nitazeeka na kufa nikiwa peke yangu? yaani mpweke?
Ukiwa peke yako kitandani unaperuzi mitandaoni unaona watu wanafunga ndoa unajiuliza hawa waliwezaje?walikutana vipi, wakaongea yapi hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa na hadi kuzaa watoto na kutulia bado wakiwa na furaha zao?
Kwa hakika huyu mdudu upweke anatisha sana, sikuwahi kuwaza ungeweza kunivaa na mimi,
Nawashauri mliopo kwenye mahusiano shikilianeni hivyo hivyo, huku nje kugumu sana na wala haichekeshi kabisa.
Salaam.