Kisa kizuri cha kaka mwenye wake wawili..hata mwenye mmoja afu ana "mchepuko"

byongo

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
827
1,944
Assalam alaikum.
Naitwa AbdulMalik na nina kisa changu napenda niwajulishe. Nimeoa wake wawili. Nilimuoa mke wangu wa kwanza Nadiya nikiwa na umri wa miaka 31 na yeye akiwa na miaka 21.

Yalikuwa ni mapenzi kwa mara ya kwanza. Nilimpenda kwa dhati na nilitaka awe wangu kwa maisha yangu yote. Nadiya ni mpole, msafi na mvumilivu. Nimezaa nae watoto 5.

Nilikutana na mke wangu wa pili Bilqis kupitia kwa rafiki yangu. Hii ilikuwa ni miaka 14 baada ya kufunga ndoa na Nadiya. Bilqis ni mrembo, Bint mdogo na ndiyo......mbichiiiiii

Nilimuoa Bilqis. Nadiya alikuwa mkimya sana kwa mimi kuongeza mke wa pili kiasi ambacho alinitia mashaka. Uvumilivu wake kupita kiasi ulinitia shaka kama kuna usalama ndani yake. Alimkubali/alimpokea mke wangu wa pili na alimkaribisha (mke mwenzie).

Hili lilinifurahisha haswa baada ya kuona imekuwa tofauti na yaliyowakuta baadhi ya marafiki zangu waliothubutu kuwa na ndoa ya wake wengi. Siyo jambo rahisi. Nilichukulia kiurahisi tu kuwa kama mwanamke wa kiislamu Nadiya lazima aukubali ukewenza.

Siku moja hivi karibuni, Sadiq, kaka binamu wa Nadiya alikuja kututembelea. Nadiya na Sadiq walilelewa ndani ya nyumba/familia moja hivyo walikuwa wanaelewana. Nadiya na binamu yake walikuwa na mambo mengi sana ya kuongea. Waliketi pamoja sebuleni wakiongea na walionekana wazi kuyafurahia mazungumzo yao wakikumbushiana matukio mengi mazuri walipokuwa wakiishi pamoja nyumbani kwao.

Wakati huo nilianza kupatwa na hali fulani..., hali fulani ya kujuta ilinijia ndani yangu. Nilianza kumuonea wivu Sadiq kwa vile alivyoweza kumfanya Nadiya kucheka kwa nguvu, na jinsi alivyoyazungusha macho yake kwa furaha kadri walivyoendelea na mazungumzo yao.

Sikuwahi kumuona mke wangu akiwa na furaha kiasi kile na aaah ndiyo......nilimuona ni mrembo baada ya kipindi kirefu. Nilianza kutafuta vijisababu vya kumfanya Nadiya aondoke pale sebuleni. “Ndio kwanza tumeanza kuongea” alilalamika Sadiq pale nilipomtuma Nadiya atuandalie vitafunwa. Ilibaki kidogo nimlipukie Sadiq kwa hasira.

Sadiq hatimaye aliondoka baada ya masaa mawili..... Nilimuona mke wangu Nadiya akianza kurudi katika hali yake ya unyonge. Niliona furaha usoni pake ikitoweka ghafla mbele yangu. Nilimuona Nadiya akirejea hali ya huzuni. Alionekana mpweke.

Ni hapa ndipo nilipoanza kubainikiwa na ukweli.
Je, nimefeli katika wajibu wangu kama mume? Nilianza kujiuliza maswali.
Ni lini kwa mara ya mwisho nilifanya juhudi kumfanya Nadiya acheke?

Ni lini kwa mara ya mwisho tulikaa pamoja na kuongea huku tukibadilishana hili na lile kama tulivyokuwa tukifanya kipindi alipokuwa tunda pekee la macho yangu?
Je, Nadiya ana furaha?

Sikuweza kujizuia bali kukumbuka ile hali ya upweke ya ghafla niliyomuona nayo mke wangu mara baada ya Sadiq kuondoka. Hii hali kiukweli ilinitatiza sana. Kisha nikajiuliza......endapo upata hali fulani ya wivu kwa sababu tu mwanaume mwingine unayemfahamu ameweza kutoka na mwanamke uliyekuwa nae, ni hali gani Nadiya anaipitia kwa sasa?

Hmmm. Nilitafakari peke yangu. Ni vipi anajisikia kila anaponiona nikiwa na Bilqis? Hali ya majuto ilinimeza/ ilinitawala. Nimekuwa nikijihusisha/ nimeegemea mno kwa mke wangu mpya na mbichi kiasi ambacho sikujali kuyawaza mengine.

Mara nikaanza kutambua ya kuwa kuna mengi nyuma ya pazia la uvumilivu wa Nadiya. Nilihitaji kujua. Nilihitaji kujua ukweli kwa kuwa ile hali ya huzuni ya Nadiya iliendelea kunisumbua akilini. Hivyo nilijipanga katika mkakati wangu wa kujua ukweli.

Yafuatayo ni majibu niliyoyapata.
Nadiya aligundua mabadiliko yangu kipindi kile kile nilipoanza kumfukuzia Bilqis. Nilikuwa na hasira za haraka, mwepesi wa kulalamika na mgumu wa kubembeleza. Muda mwingi nilikunja sura yangu hali ambayo ilimtisha na kumzuwia Nadiya kutoa sauti yake kuelezea hisia zake.

Kipindi nilipoanza kumshusha thamani kutokana na mwonekano wake wa kuchuja baada ya kuzaa (hili lilimuumiza sana) Ya Salaam! Niliacha kutambua jitihada zake za kuonekana mrembo ili kunifurahisha kwa mavazi yake, kujipodoa na manukato yake aliyojipulizia kwa ajili yangu...Nilijisahaulisha kabisa kumsifia pale kila alipojipamba kwa ajili yangu

Aliniona nikiwa mwepesi mno kujibu sms kutoka kwa Bilqis na nilivyokuwa nikiikodolea simu yangu macho kusubiria kupigiwa na Bilqis. Pia ilitokea mara nyingi nikiacha kwa makusudi kujibu msg za maana za kufikirisha na mazungumzo kutoka kwa Nadiya. Mara nyingine sikumpigia nilipokuwa mbali ma nyumbani. (Nadiya mara zote alinipigia simu).

Aliniangalia nikirudi nyumbani na kubwa nililolifanya ni maandalizi ya bi harusi mpya Bilqis. Nilitekwa mno na furaha ya kuoa, nilimtumia pesa nyingi na kuacha kutimiza baadhi ya mahitaji muhimu ya familia yangu.

Mara zote Nadiya ndiye aliyenianza kwenye suala la kupeana unyumba, kwa sababu mara nyingi nilijilaza tu kitandani na kumpuuza mke wangu. (Mbaya sana!!!) Ilibidi afanye yeye juhudi zote kwa kuwa hakuwa tayari kuniudhi hata kidogo.

Alikuwa na khofu ya mwanamke mpya anaekuja. Je, wataweza kuvumiliana? Je, atawapenda watoto wake? Ikiwa huyu mwanamke ameweza kumharibu mume wake akiwa nje ya ndoaIf 'this woman could distract , nini kitatokea akiingia ndani? Ataweza ...? Aliwaza mambo mengi sana kichwani bila kuyapatia majibu, bila kuwa na mtu wa kumwambia maumivu na khofu yake. Alishindwa kwa kukhofia ataambiwa kuwa ana wivu.

Haya ni katika uhalisia kwa uchache tu. Niliyapataje haya yote? Nilimkalisha chini Nadiya, nikamshika mikono yake na nikamuomba kwa ajili ya Allaah aongee nami. Alifanya kama nilivyomuomba, huku akibubujikwa na machozi. Nilijihisi haya/aibu.Nilihisi nilimdharau na kumbagua vya kutosha.

Unasemaje? Ndoa ya wake wengi siyo sunnah ya Mitume ambayo kila mwanamke wa kiislamu anawajibika kuikubali?
Ni kweli. Kaka zangu, tunahitaji kuiendea sunnah hii bila kuwaumiza mke/ wake zetu wengine.

Ushauri.
Kamwe usimdharau mkeo / wake zako. Siku zote wajibika na kuwajali. Wewe unaweza kuwa na wengi wa kuwaonesha upendo na kuwajali, lakini yeye ana WEWE PEKEE.

Mpe mkeo mahitaji yake. Hapa namaanisha tumia muda wa kutosha kaa na mkeo na umridhishe umtimizie mahitaji yake, haswa ya kitandani/chumbani. Mkumbatie, mpige busu na ucheze nae. Kumbuka wewe ni mume wake pekee.

Toka nae pamoja peke yenu. Nenda nae safari, matembezi, watembeee ndugu/marafiki pamoja, na nendeni kufanya manunuzi pamoja.
Ikiwezekana mfanye fungate tena mbali nje ya mji wenu. Kama ikishindikana kwenda mbali na mji wenu basi nendeni sehemu ya karibu mtakayomudu.

Muulize habari za asubuhi na mtakie usiku mwema. Usisubiri akuanze yeye kila siku. Jali uwepo wake muda wote. Call when you're not around. Mpigie unapokuwa mbali na nyumbani.

Wajibika/onyesha kumjali: msikilize na umjali kiukweli. Jibu msg zake na mazungumzo yake. Mrushie mabusu...

Kila mwanamke anataka kujua MUME WAKE bado ni wake. Unaweza kuwa ni wa wa2, 3 or 4 kwa wakati mmoja ikiwa utafuata sunnah ya Nabiy SAW.
Namaanisha usiache kuwa mume mpenzi wa wake zako wote. Kamwe usimfanye yeyote katika wake zako akajiona anaishi kwa matakwa ya mke mwenzake.

Mpe kila mmoja katika wake zako haki zake za msingi anazostahili. Mlishe na mvishe kama inavyotakikana. Ikiwa utafanya hivi pale tu pindi unapooa mke mwingine, tegemea machafuko na ukosefu wa uaminifu. Hata watoto wataona mabadiliko.

Mfanye mke wako au wake zako waliotangulia wajue kuwa unawathamini. Usisubiri ujio wa mtu mwingine aseme AHSANTE.

Kamwe usioe mke ukamlinganisha na wa mwanzo. Usimtowe kasoro mke mkubwa na kumkejeli kuwa amezeeka au matiti yake yapo hivi au vile na ukamwacha na kuoa binti mdogo na mbichi Ya Salam! Umempa sababu za kujiona hafai na sababu za kumchukia mkeo mpya.

Ndiyo, una wengi wa kuwachagua, lakini wewe ni pekee aliye nae.
Juu ya yote, ni muhimu kuwasiliana. Mazungumzo husaidia kuondoa sintofahamu na kuponya vidonda vya moyo.

Niliongea na Nadiya na kuhisi machungu yake. Alinipenda kiasi cha kuwa na wivu nami, alinipenda sana kiasi cha kuweza kuyabeba yote haya kwa amani kabisa.

Nadiya ni mke mwema na mama kipenzi. Ni kipi zaidi niombe? Nilichukua muda wangu kurejesha upendo wa mke wangu tena..........na nimeupata!
Ninawapenda wake zangu wote wawili.
Kila mmoja ana sifa zake za kipekee.

Namuomba Allah atusamehe kaka zangu na atusaidie kutunza amana.

Wanawake ni lazima tuwajali na kuwapenda.
Hawahitaji chochote cha ziada katika kutufurahisha na kushindana, zaidi ni kwa ajili ya kupata upendo na kuwajali. Hii ndio sunnah.
Alhamdulillah!

Tuma kisa hiki kwa wanaume wote waliooa.... Na kwa wanawake pia.
 
Assalam alaikum.
Naitwa AbdulMalik na nina kisa changu napenda niwajulishe. Nimeoa wake wawili. Nilimuoa mke wangu wa kwanza Nadiya nikiwa na umri wa miaka 31 na yeye akiwa na miaka 21. Yalikuwa ni mapenzi kwa mara ya kwanza. Nilimpenda kwa dhati na nilitaka awe wangu kwa maisha yangu yote. Nadiya ni mpole, msafi na mvumilivu. Nimezaa nae watoto 5.

Nilikutana na mke wangu wa pili Bilqis kupitia kwa rafiki yangu. Hii ilikuwa ni miaka 14 baada ya kufunga ndoa na Nadiya. Bilqis ni mrembo, Bint mdogo na ndiyo......mbichiiiiii
Nilimuoa Bilqis. Nadiya alikuwa mkimya sana kwa mimi kuongeza mke wa pili kiasi ambacho alinitia mashaka. Uvumilivu wake kupita kiasi ulinitia shaka kama kuna usalama ndani yake. Alimkubali/alimpokea mke wangu wa pili na alimkaribisha (mke mwenzie).
Hili lilinifurahisha haswa baada ya kuona imekuwa tofauti na yaliyowakuta baadhi ya marafiki zangu waliothubutu kuwa na ndoa ya wake wengi. Siyo jambo rahisi.
Nilichukulia kiurahisi tu kuwa kama mwanamke wa kiislamu Nadiya lazima aukubali ukewenza.

Siku moja hivi karibuni, Sadiq, kaka binamu wa Nadiya alikuja kututembelea. Nadiya na Sadiq walilelewa ndani ya nyumba/familia moja hivyo walikuwa wanaelewana. Nadiya na binamu yake walikuwa na mambo mengi sana ya kuongea. Waliketi pamoja sebuleni wakiongea na walionekana wazi kuyafurahia mazungumzo yao wakikumbushiana matukio mengi mazuri walipokuwa wakiishi pamoja nyumbani kwao.

Wakati huo nilianza kupatwa na hali fulani..., hali fulani ya kujuta ilinijia ndani yangu. Nilianza kumuonea wivu Sadiq kwa vile alivyoweza kumfanya Nadiya kucheka kwa nguvu, na jinsi alivyoyazungusha macho yake kwa furaha kadri walivyoendelea na mazungumzo yao. Sikuwahi kumuona mke wangu akiwa na furaha kiasi kile na aaah ndiyo......nilimuona ni mrembo baada ya kipindi kirefu. Nilianza kutafuta vijisababu vya kumfanya Nadiya aondoke pale sebuleni. “Ndio kwanza tumeanza kuongea” alilalamika Sadiq pale nilipomtuma Nadiya atuandalie vitafunwa. Ilibaki kidogo nimlipukie Sadiq kwa hasira.

Sadiq hatimaye aliondoka baada ya masaa marefuawili..... Nilimuona mke wangu Nadiya akianza kurudi katika hali yake ya unyonge. Niliona furaha usoni pake ikitoweka ghafla mbele yangu. Nilimuona Nadiya akirejea hali ya huzuni. Alionekana mpweke.

Ni hapa ndipo nilipoanza kubainikiwa na ukweli.

Je, nimefeli katika wajibu wangu kama mume? Nilianza kujiuliza maswali.
Ni lini kwa mara ya mwisho nilifanya juhudi kumfanya Nadiya acheke?
Ni lini kwa mara ya mwisho tulikaa pamoja na kuongea huku tukibadilishana hili na lile kama tulivyokuwa tukifanya kipindi alipokuwa tunda pekee la macho yangu?
Je, Nadiya ana furaha?
Sikuweza kujizuia bali kukumbuka ile hali ya upweke ya ghafla niliyomuona nayo mke wangu mara baada ya Sadiq kuondoka. Hii hali kiukweli ilinitatiza sana.
Kisha nikajiuliza......endapo upata hali fulani ya wivu kwa sababu tu mwanaume mwingine unayemfahamu ameweza kutoka na mwanamke uliyekuwa nae, ni hali gani Nadiya anaipitia kwa sasa?
Hmmm. Nilitafakari peke yangu. Ni vipi anajisikia kila anaponiona nikiwa na Bilqis? Hali ya majuto ilinimeza/ ilinitawala. Nimekuwa nikijihusisha/ nimeegemea mno kwa mke wangu mpya na mbichi kiasi ambacho sikujali kuyawaza mengine. Mara nikaanza kutambua ya kuwa kuna mengi nyuma ya pazia la uvumilivu wa Nadiya. Nilihitaji kujua. Nilihitaji kujua ukweli kwa kuwa ile hali ya huzuni ya Nadiya iliendelea kunisumbua akilini. Hivyo nilijipanga katika mkakati wangu wa kujua ukweli.

Yafuatayo ni majibu niliyoyapata.

Nadiya aligundua mabadiliko yangu kipindi kile kile nilipoanza kumfukuzia Bilqis. Nilikuwa na hasira za haraka, mwepesi wa kulalamika na mgumu wa kubembeleza. Muda mwingi nilikunja sura yangu hali ambayo ilimtisha na kumzuwia Nadiya kutoa sauti yake kuelezea hisia zake.
Kipindi nilipoanza kumshusha thamani kutokana na mwonekano wake wa kuchuja baada ya kuzaa (hili lilimuumiza sana) Ya Salaam! Niliacha kutambua jitihada zake za kuonekana mrembo ili kunifurahisha kwa mavazi yake, kujipodoa na manukato yake aliyojipulizia kwa ajili yangu...Nilijisahaulisha kabisa kumsifia pale kila alipojipamba kwa ajili yangu
Aliniona nikiwa mwepesi mno kujibu sms kutoka kwa Bilqis na nilivyokuwa nikiikodolea simu yangu macho kusubiria kupigiwa na Bilqis. Pia ilitokea mara nyingi nikiacha kwa makusudi kujibu msg za maana za kufikirisha na mazungumzo kutoka kwa Nadiya. Mara nyingine sikumpigia nilipokuwa mbali ma nyumbani. (Nadiya mara zote alinipigia simu).?
Aliniangalia nikirudi nyumbani na kubwa nililolifanya ni maandalizi ya bi harusi mpya Bilqis. Nilitekwa mno na furaha ya kuoa, nilimtumia pesa nyingi na kuacha kutimiza baadhi ya mahitaji muhimu ya familia yangu.
Mara zote Nadiya ndiye aliyenianza kwenye suala la kupeana unyumba, kwa sababu mara nyingi nilijilaza tu kitandani na kumpuuza mke wangu. (Mbaya sana!!!)
Ilibidi afanye yeye juhudi zote kwa kuwa hakuwa tayari kuniudhi hata kidogo.
Alikuwa na khofu ya mwanamke mpya anaekuja. Je, wataweza kuvumiliana? Je, atawapenda watoto wake? Ikiwa huyu mwanamke ameweza kumharibu mume wake akiwa nje ya ndoaIf 'this woman could distract , nini kitatokea akiingia ndani? Ataweza ...? Aliwaza mambo mengi sana kichwani bila kuyapatia majibu, bila kuwa na mtu wa kumwambia maumivu na khofu yake. Alishindwa kwa kukhofia ataambiwa kuwa ana wivu.
Haya ni katika uhalisia kwa uchache tu. Niliyapataje haya yote? Nilimkalisha chini Nadiya, nikamshika mikono yake na nikamuomba kwa ajili ya Allaah aongee nami. Alifanya kama nilivyomuomba, huku akibubujikwa na machozi. Nilijihisi haya/aibu.Nilihisi nilimdharau na kumbagua vya kutosha.

Unasemaje? Ndoa ya wake wengi siyo sunnah ya Mitume ambayo kila mwanamke wa kiislamu anawajibika kuikubali?
Ni kweli. Kaka zangu, tunahitaji kuiendea sunnah hii bila kuwaumiza mke/ wake zetu wengine.

Ushauri.
Kamwe usimdharau mkeo / wake zako. Siku zote wajibika na kuwajali. Wewe unaweza kuwa na wengi wa kuwaonesha upendo na kuwajali, lakini yeye ana WEWE PEKEE.
Mpe mkeo mahitaji yake. Hapa namaanisha tumia muda wa kutosha kaa na mkeo na umridhishe umtimizie mahitaji yake, haswa ya kitandani/chumbani. Mkumbatie, mpige busu na ucheze nae. Kumbuka wewe ni mume wake pekee.
Toka nae pamoja peke yenu. Nenda nae safari, matembezi, watembeee ndugu/marafiki pamoja, na nendeni kufanya manunuzi pamoja.
Ikiwezekana mfanye fungate tena mbali nje ya mji wenu. Kama ikishindikana kwenda mbali na mji wenu basi nendeni sehemu ya karibu mtakayomudu.
Muulize habari za asubuhi na mtakie usiku mwema. Usisubiri akuanze yeye kila siku. Jali uwepo wake muda wote. Call when you're not around. Mpigie unapokuwa mbali na nyumbani.
Wajibika/onyesha kumjali: msikilize na umjali kiukweli. Jibu msg zake na mazungumzo yake. Mrushie mabusu...
Kila mwanamke anataka kujua MUME WAKE bado ni wake. Unaweza kuwa ni wa wa2, 3 or 4 kwa wakati mmoja ikiwa utafuata sunnah ya Nabiy SAW.
Namaanisha usiache kuwa mume mpenzi wa wake zako wote. Kamwe usimfanye yeyote katika wake zako akajiona anaishi kwa matakwa ya mke mwenzake.
Mpe kila mmoja katika wake zako haki zake za msingi anazostahili. Mlishe na mvishe kama inavyotakikana. Ikiwa utafanya hivi pale tu pindi unapooa mke mwingine, tegemea machafuko na ukosefu wa uaminifu. Hata watoto wataona mabadiliko.
Mfanye mke wako au wake zako waliotangulia wajue kuwa unawathamini. Usisubiri ujio wa mtu mwingine aseme AHSANTE.
Kamwe usioe mke ukamlinganisha na wa mwanzo. Usimtowe kasoro mke mkubwa na kumkejeli kuwa amezeeka au matiti yake yapo hivi au vile na ukamwacha na kuoa binti mdogo na mbichi Ya Salam! Umempa sababu za kujiona hafai na sababu za kumchukia mkeo mpya.
Ndiyo, una wengi wa kuwachagua, lakini wewe ni pekee aliye nae.
Juu ya yote, ni muhimu kuwasiliana. Mazungumzo husaidia kuondoa sintofahamu na kuponya vidonda vya moyo.

Niliongea na Nadiya na kuhisi machungu yake. Alinipenda kiasi cha kuwa na wivu nami, alinipenda sana kiasi cha kuweza kuyabeba yote haya kwa amani kabisa.
Nadiya ni mke mwema na mama kipenzi. Ni kipi zaidi niombe? Nilichukua muda wangu kurejesha upendo wa mke wangu tena..........na nimeupata!
Ninawapenda wake zangu wote wawili.
Kila mmoja ana sifa zake za kipekee.

Namuomba Allah atusamehe kaka zangu na atusaidie kutunza amana.

Wanawake ni lazima tuwajali na kuwapenda.
Hawahitaji chochote cha ziada katika kutufurahisha na kushindana, zaidi ni kwa ajili ya kupata upendo na kuwajali. Hii ndio sunnah.
Alhamdulillah!

Tuma kisa hiki kwa wanaume wote waliooa.... Na kwa wanawake pia.
Yani sa zingine bora hata upande huu kuliko ule,wa one wife lkn michepuko mia.
 
Assalam alaikum.
Naitwa AbdulMalik na nina kisa changu napenda niwajulishe. Nimeoa wake wawili. Nilimuoa mke wangu wa kwanza Nadiya nikiwa na umri wa miaka 31 na yeye akiwa na miaka 21.

Yalikuwa ni mapenzi kwa mara ya kwanza. Nilimpenda kwa dhati na nilitaka awe wangu kwa maisha yangu yote. Nadiya ni mpole, msafi na mvumilivu. Nimezaa nae watoto 5.

Nilikutana na mke wangu wa pili Bilqis kupitia kwa rafiki yangu. Hii ilikuwa ni miaka 14 baada ya kufunga ndoa na Nadiya. Bilqis ni mrembo, Bint mdogo na ndiyo......mbichiiiiii

Nilimuoa Bilqis. Nadiya alikuwa mkimya sana kwa mimi kuongeza mke wa pili kiasi ambacho alinitia mashaka. Uvumilivu wake kupita kiasi ulinitia shaka kama kuna usalama ndani yake. Alimkubali/alimpokea mke wangu wa pili na alimkaribisha (mke mwenzie).

Hili lilinifurahisha haswa baada ya kuona imekuwa tofauti na yaliyowakuta baadhi ya marafiki zangu waliothubutu kuwa na ndoa ya wake wengi. Siyo jambo rahisi. Nilichukulia kiurahisi tu kuwa kama mwanamke wa kiislamu Nadiya lazima aukubali ukewenza.

Siku moja hivi karibuni, Sadiq, kaka binamu wa Nadiya alikuja kututembelea. Nadiya na Sadiq walilelewa ndani ya nyumba/familia moja hivyo walikuwa wanaelewana. Nadiya na binamu yake walikuwa na mambo mengi sana ya kuongea. Waliketi pamoja sebuleni wakiongea na walionekana wazi kuyafurahia mazungumzo yao wakikumbushiana matukio mengi mazuri walipokuwa wakiishi pamoja nyumbani kwao.

Wakati huo nilianza kupatwa na hali fulani..., hali fulani ya kujuta ilinijia ndani yangu. Nilianza kumuonea wivu Sadiq kwa vile alivyoweza kumfanya Nadiya kucheka kwa nguvu, na jinsi alivyoyazungusha macho yake kwa furaha kadri walivyoendelea na mazungumzo yao.

Sikuwahi kumuona mke wangu akiwa na furaha kiasi kile na aaah ndiyo......nilimuona ni mrembo baada ya kipindi kirefu. Nilianza kutafuta vijisababu vya kumfanya Nadiya aondoke pale sebuleni. “Ndio kwanza tumeanza kuongea” alilalamika Sadiq pale nilipomtuma Nadiya atuandalie vitafunwa. Ilibaki kidogo nimlipukie Sadiq kwa hasira.

Sadiq hatimaye aliondoka baada ya masaa mawili..... Nilimuona mke wangu Nadiya akianza kurudi katika hali yake ya unyonge. Niliona furaha usoni pake ikitoweka ghafla mbele yangu. Nilimuona Nadiya akirejea hali ya huzuni. Alionekana mpweke.

Ni hapa ndipo nilipoanza kubainikiwa na ukweli.
Je, nimefeli katika wajibu wangu kama mume? Nilianza kujiuliza maswali.
Ni lini kwa mara ya mwisho nilifanya juhudi kumfanya Nadiya acheke?

Ni lini kwa mara ya mwisho tulikaa pamoja na kuongea huku tukibadilishana hili na lile kama tulivyokuwa tukifanya kipindi alipokuwa tunda pekee la macho yangu?
Je, Nadiya ana furaha?

Sikuweza kujizuia bali kukumbuka ile hali ya upweke ya ghafla niliyomuona nayo mke wangu mara baada ya Sadiq kuondoka. Hii hali kiukweli ilinitatiza sana. Kisha nikajiuliza......endapo upata hali fulani ya wivu kwa sababu tu mwanaume mwingine unayemfahamu ameweza kutoka na mwanamke uliyekuwa nae, ni hali gani Nadiya anaipitia kwa sasa?

Hmmm. Nilitafakari peke yangu. Ni vipi anajisikia kila anaponiona nikiwa na Bilqis? Hali ya majuto ilinimeza/ ilinitawala. Nimekuwa nikijihusisha/ nimeegemea mno kwa mke wangu mpya na mbichi kiasi ambacho sikujali kuyawaza mengine.

Mara nikaanza kutambua ya kuwa kuna mengi nyuma ya pazia la uvumilivu wa Nadiya. Nilihitaji kujua. Nilihitaji kujua ukweli kwa kuwa ile hali ya huzuni ya Nadiya iliendelea kunisumbua akilini. Hivyo nilijipanga katika mkakati wangu wa kujua ukweli.

Yafuatayo ni majibu niliyoyapata.
Nadiya aligundua mabadiliko yangu kipindi kile kile nilipoanza kumfukuzia Bilqis. Nilikuwa na hasira za haraka, mwepesi wa kulalamika na mgumu wa kubembeleza. Muda mwingi nilikunja sura yangu hali ambayo ilimtisha na kumzuwia Nadiya kutoa sauti yake kuelezea hisia zake.

Kipindi nilipoanza kumshusha thamani kutokana na mwonekano wake wa kuchuja baada ya kuzaa (hili lilimuumiza sana) Ya Salaam! Niliacha kutambua jitihada zake za kuonekana mrembo ili kunifurahisha kwa mavazi yake, kujipodoa na manukato yake aliyojipulizia kwa ajili yangu...Nilijisahaulisha kabisa kumsifia pale kila alipojipamba kwa ajili yangu

Aliniona nikiwa mwepesi mno kujibu sms kutoka kwa Bilqis na nilivyokuwa nikiikodolea simu yangu macho kusubiria kupigiwa na Bilqis. Pia ilitokea mara nyingi nikiacha kwa makusudi kujibu msg za maana za kufikirisha na mazungumzo kutoka kwa Nadiya. Mara nyingine sikumpigia nilipokuwa mbali ma nyumbani. (Nadiya mara zote alinipigia simu).

Aliniangalia nikirudi nyumbani na kubwa nililolifanya ni maandalizi ya bi harusi mpya Bilqis. Nilitekwa mno na furaha ya kuoa, nilimtumia pesa nyingi na kuacha kutimiza baadhi ya mahitaji muhimu ya familia yangu.

Mara zote Nadiya ndiye aliyenianza kwenye suala la kupeana unyumba, kwa sababu mara nyingi nilijilaza tu kitandani na kumpuuza mke wangu. (Mbaya sana!!!) Ilibidi afanye yeye juhudi zote kwa kuwa hakuwa tayari kuniudhi hata kidogo.

Alikuwa na khofu ya mwanamke mpya anaekuja. Je, wataweza kuvumiliana? Je, atawapenda watoto wake? Ikiwa huyu mwanamke ameweza kumharibu mume wake akiwa nje ya ndoaIf 'this woman could distract , nini kitatokea akiingia ndani? Ataweza ...? Aliwaza mambo mengi sana kichwani bila kuyapatia majibu, bila kuwa na mtu wa kumwambia maumivu na khofu yake. Alishindwa kwa kukhofia ataambiwa kuwa ana wivu.

Haya ni katika uhalisia kwa uchache tu. Niliyapataje haya yote? Nilimkalisha chini Nadiya, nikamshika mikono yake na nikamuomba kwa ajili ya Allaah aongee nami. Alifanya kama nilivyomuomba, huku akibubujikwa na machozi. Nilijihisi haya/aibu.Nilihisi nilimdharau na kumbagua vya kutosha.

Unasemaje? Ndoa ya wake wengi siyo sunnah ya Mitume ambayo kila mwanamke wa kiislamu anawajibika kuikubali?
Ni kweli. Kaka zangu, tunahitaji kuiendea sunnah hii bila kuwaumiza mke/ wake zetu wengine.

Ushauri.
Kamwe usimdharau mkeo / wake zako. Siku zote wajibika na kuwajali. Wewe unaweza kuwa na wengi wa kuwaonesha upendo na kuwajali, lakini yeye ana WEWE PEKEE.

Mpe mkeo mahitaji yake. Hapa namaanisha tumia muda wa kutosha kaa na mkeo na umridhishe umtimizie mahitaji yake, haswa ya kitandani/chumbani. Mkumbatie, mpige busu na ucheze nae. Kumbuka wewe ni mume wake pekee.

Toka nae pamoja peke yenu. Nenda nae safari, matembezi, watembeee ndugu/marafiki pamoja, na nendeni kufanya manunuzi pamoja.
Ikiwezekana mfanye fungate tena mbali nje ya mji wenu. Kama ikishindikana kwenda mbali na mji wenu basi nendeni sehemu ya karibu mtakayomudu.

Muulize habari za asubuhi na mtakie usiku mwema. Usisubiri akuanze yeye kila siku. Jali uwepo wake muda wote. Call when you're not around. Mpigie unapokuwa mbali na nyumbani.

Wajibika/onyesha kumjali: msikilize na umjali kiukweli. Jibu msg zake na mazungumzo yake. Mrushie mabusu...

Kila mwanamke anataka kujua MUME WAKE bado ni wake. Unaweza kuwa ni wa wa2, 3 or 4 kwa wakati mmoja ikiwa utafuata sunnah ya Nabiy SAW.
Namaanisha usiache kuwa mume mpenzi wa wake zako wote. Kamwe usimfanye yeyote katika wake zako akajiona anaishi kwa matakwa ya mke mwenzake.

Mpe kila mmoja katika wake zako haki zake za msingi anazostahili. Mlishe na mvishe kama inavyotakikana. Ikiwa utafanya hivi pale tu pindi unapooa mke mwingine, tegemea machafuko na ukosefu wa uaminifu. Hata watoto wataona mabadiliko.

Mfanye mke wako au wake zako waliotangulia wajue kuwa unawathamini. Usisubiri ujio wa mtu mwingine aseme AHSANTE.

Kamwe usioe mke ukamlinganisha na wa mwanzo. Usimtowe kasoro mke mkubwa na kumkejeli kuwa amezeeka au matiti yake yapo hivi au vile na ukamwacha na kuoa binti mdogo na mbichi Ya Salam! Umempa sababu za kujiona hafai na sababu za kumchukia mkeo mpya.

Ndiyo, una wengi wa kuwachagua, lakini wewe ni pekee aliye nae.
Juu ya yote, ni muhimu kuwasiliana. Mazungumzo husaidia kuondoa sintofahamu na kuponya vidonda vya moyo.

Niliongea na Nadiya na kuhisi machungu yake. Alinipenda kiasi cha kuwa na wivu nami, alinipenda sana kiasi cha kuweza kuyabeba yote haya kwa amani kabisa.

Nadiya ni mke mwema na mama kipenzi. Ni kipi zaidi niombe? Nilichukua muda wangu kurejesha upendo wa mke wangu tena..........na nimeupata!
Ninawapenda wake zangu wote wawili.
Kila mmoja ana sifa zake za kipekee.

Namuomba Allah atusamehe kaka zangu na atusaidie kutunza amana.

Wanawake ni lazima tuwajali na kuwapenda.
Hawahitaji chochote cha ziada katika kutufurahisha na kushindana, zaidi ni kwa ajili ya kupata upendo na kuwajali. Hii ndio sunnah.
Alhamdulillah!

Tuma kisa hiki kwa wanaume wote waliooa.... Na kwa wanawake pia.

Kuwa na mke mmoja au wawili ni kutokana na imani aliyonayo mtu yaweza kuwa ya kidini au ya kimila.
Ninachokupongeza wewe ni kuweza kutambua tatizo ulilokuwa nalo wewe na maumivu uliyomsababishia mkeo na kujikebisha kama mume, kitu ambacho wanaume tungeweza kuwa na ufahamu kama wako paradiso ingeanzia hapa dunia katika ndoa zetu.

Kinachotutatiza wanaume ni ile hali ya kiburi na dharau tuliyo nayo juu ya wake zetu, ubinafsi wa kujiona bora kuliko mkeo na yeye ni mtumwa kwako, tunajikuta wake zetu wanapata matatizo mengi ya kiafya, BP, vidonda vya tumbo, stress mwisho wa siku vinatugarimu sie wenyewe wanaume kugaramia matibabu na muda..

Nakupongeza sana kwa kujitambua na kuelewa wajibu na majukumu kama mume, saidia wengine kwakushauri mabadiliko katika jamii inayokuzunguka kwakushauri wanaume jinsi ya kuishi na wake zao.
Nakutakia furaha tele kati ndoa yako
Inshaalah!
 
Shukran kwa mchango wako..japo hio story ni Copy&Paste
 
Back
Top Bottom