Nimeamini sasa, Rais Kikwete amechoka

Nimeamini sasa, Rais Kikwete amechoka

TAWA

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
3,674
Reaction score
1,572
Kupitia taarifa ya habari ya ITV usiku huu nimesikia kwamba Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambi rambi Waziri mkuu mh. Mizengo Pinda kutokana kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ulanga na waziri katika ofisi ya rais utumishi Mh. Celina Kombani.
Sasa najiuliza hivi nani ni mfiwa hapo?
1. Huyu ni mteule wa rais kwa maana ya waziri.
2. Huyu ni waziri anayefanya kazi katika ofisi ya Rais ambayo kimsingi ndiye Mh. Kikwete.
3. Mjumbe katika baraza la mawaziri ambalo Mh. Kikwete ni mwenyekiti.
4. Mwanachama na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM chama ambacho Mh. Rais Kikwete ndiye mwenyekiti wake.
Sasa salamu hizo za rambi rambi kwa waziri mkuu zinamantiki ipi?
Hebu watu wa itifaki tusaidiane hapa.
 
Da! kamanda tawa hata mm nmejiulza sana baada ya kuona habari hiyo. Nkajua labda mizemgo ndiye rais
 
Imenishangaza...labda ni kutaka tu asikike kuonyesha kuguswa. Angalau nimesikia pia kamtumia salaam za rambirambi mme wa marehemu.
 
Kwenye mkutano mkuu wa CCM alijisahau pia kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa CCM
 
gazeti la serikali Habari leo limeshindwa kuweka msiba huu kama habari kuu....
 
kwani karudi kutoka kwa Obama?

Inawezekana ni salamu kutoka serikali yake ya amezituma kutoka serikali yake ya kwenye ndege.
 
Akili ni nywele kila mtu na zake,
Bosi wa waziri ni waziri mkuu au rais? Unadhani kuwa waziri ofisi ya RAIS kuna mfanya waziri kuripoti kwa rais au kwa bosi wako waziri mkuu?

Ofisi ya RAIS ni eneo lake la kazi, anaripoti baraza la.mawaziri ambako mkuu wake ni Pinda.

Kabla hatujaanza kupiga makelele walau tujitahidi kujua chain of command ya uongozi wa nchi yetu.

Kesho mtataka RAIS asimheshimu mwenyekiti wake wa serikali za mitaa kisa yeye ni rais yupo juu yake bila kujua bosi wa serikali ya mtaa ni.mwenyekiti wa mtaa husika
 
Sukushangai, tatizo ni viporo vyako vya wanzuki unavyofakamia kabla ya kuja kubwata humu.
Kwa hiyo leo unauaminisha umma kuwa bosi wa baraza la mawaziri ambalo kimsingi mawaziri ndiyo wanawajibika ni waziri mkuu!?
Usijitie upofu hapa hatujadili chain of command tunajadili mheshimiwa waziri mkuu kupewa salamu za rambi rambi kwa kifo cha waziri.
 
Akili ni nywele kila mtu na zake,
Bosi wa waziri ni waziri mkuu au rais? Unadhani kuwa waziri ofisi ya RAIS kuna mfanya waziri kuripoti kwa rais au kwa bosi wako waziri mkuu?

Ofisi ya RAIS ni eneo lake la kazi, anaripoti baraza la.mawaziri ambako mkuu wake ni Pinda.

Kabla hatujaanza kupiga makelele walau tujitahidi kujua chain of command ya uongozi wa nchi yetu.

Kesho mtataka RAIS asimheshimu mwenyekiti wake wa serikali za mitaa kisa yeye ni rais yupo juu yake bila kujua bosi wa serikali ya mtaa ni.mwenyekiti wa mtaa husika

Na dalali wa nyumba anaripoti kwa nani?
 
Back
Top Bottom