Nimeamini Rais Samia ni moto wa kumbi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Moto wa kumbi ni moto mkali sana unaweza kuyeyusha chuma au kutoboa sufuria likiwa na maji yake ndani lakini hauna miale, moshi wingi wala kelele kama mioto ya mabiwi, nyika, kuni au petroli. Unapoota moto wa kumbi inakubidi ukae mbali kidogo vinginevyo utapata mbalanga.

Kwa muda mrefu wananchi na watumishi tumezoea viongozi wanaotoa sauti kubwa kama radi wanapokerwa na jambo fulani na kukemea. Na mara nyingi wanaweza kufoka sana mdomoni na hadharani kuhusu rushwa lakini matendo yao hayaendani na maneno yao. Wanaweza kuonekana wakimtaja Mungu sana lakini matendo yao yako kinyume na Mungu, wanaweza kuonekana wanawapenda viongozi wa dini lakini kuna viongozi wa dini wako jela kwa maagizo yao.

Rais Samia ni utamaduni mpya sana nchini ambao unaweza kuondoka na watu wengi sana na hasa wavaa suruali. Anaetaka apewe maji ya kunywa kwa ukali na kufoka na anaeomba maji kwa upole na unyenyekevu wote watapata maji yaleyale, matokeo yatakuwa yaleyele ya kupata glasi ya maji safi ya kunywa, lakini yule aliyeomba kwa upole atakuwa na faida ya ziada ya kupendwa zaidi na aliyemletea maji kuliko yule aliyefoka kwa ukali.

Ndugu zangu urais ni taasisi, jukumu na mamlaka, na sio jinsia, personality, dini, kabila wala kanda ya mtu alikotoka, lazima mindset zetu zibadilike haraka kutoka kusia sauti zinazokwaruza kwenda kwenye sauti nyororo lakini zenye maana ileile na zaidi.

Tuzoee utamaduni mpya wa kuongozwa, tii mamlaka bila shuruti
 
Huwa mnaanzaga kuwasifia hivi hivi mwisho wa siku vichwa vinawavimba hawasikii Wala muaddhini wala la sista mgonga kengele

Taratibu mna pave way towards to their udikteta uchwara

Tutakuja kukumbushana hapa 2025 januari
 
Huwa mnaanzaga kuwasifia hivi hivi mwisho wa siku vichwa vinawavimba hawasikii Wala muaddhini wala la sista mgonga kengele

Taratibu mna pave way towards to their udikteta uchwara

Tutakuja kukumbushana hapa 2025 januari

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
watende kwa mujibu wa katiba iliyowaingiza hapo, nothing more nothing less. Hawa ni matunda ya Katiba hawategemewi kutenda nje ya katiba. Mama Kaboyoka hayuko peke yake
 
hukuona alivyozirarua suruali kwa tone ya kawaida sana na matokeo yakabaki yaleyale ambayo yangepatikana kwa kufokafoka na mbwembwe nyingi?
Then basi hii ni habit tu yake maana u cant escape that. Kila mtu ana character yake ila shida inakuwa pale watu wanapochanganya character ya mtu na utendaji wake..
 
Back
Top Bottom