Nimeamini maneno ya wahenga: Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,971
35,113
Habarini wanajf.

Jana jioni nilithibitisha kuwa misemo, semi na methali za wahenga zina beba maana nzuri.

Story iko hivi, mtaani kwetu kuna kaka tunaishi naye, wao ndio wazawa wa huo mtaa wanajiita wazawa sie wengine kwa kisukuma wanatuita MAJOGOLI. Kaka huyu ni mwizi sugu tena ambaye amevuka hatua ya kibaka sasa ni jambazi.
Ni jambazi ambaye tukio lolote la wizi likitokea kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela lazima Polisi wamkamate kama mshukiwa wa kwanza. Huwa anakaa sana mahabusu hadi tunamsahau lakini baadae anarudi tena uraiani kuendelea kutusumbua, hajawahi kuhukumiwa. Watu walishahoji sababu ya yeye kutokufungwa lakini OCD akasema kuwa tatizo ni kwamba watu hawaendi mahakamani kutoa ushahidi kwahiyo kesi inakosa uzito hadi anaachiwa huru.

Oooops! ngoja sasa niwasimulie yaliyotokea jana.

Jana jioni wakati natoka kibaruani nikakutana naye barabarani tukasalimiana akaniomba nisimame tuongee kidogo kwa kuwa ana matatizo, na mie bila hiyana nikamkubalia kumsikiliza.

Ndipo hapo alipoanza kunielezea mkasa uliompata juzi usiku 7/11/2017. Alisema kuwa watu walivamia kwake usiku, wakamfungia mlango kwa nje halafu wamemubia kuku wake wa kienyeji 16. Baada ya kugundua kuwa wamemfungia, ilibidi apige simu kwa jirani zake na hapo ndio jirani walikuja wakavunja komeo la mlango.

Akazidi kuongea kwa hasira "Yaani sister nitahakikisha hawa wezi nitawasaka hadi niwapate, nitazunguka hoteli, baa, vibalu vya pombe za kienyeji na hata kwa mama lishe wote hapa Buswelu hadi nijue kuku wangu walipouzwa"

Baada ya kumsiliza kwa kina sasa ikawa zamu yangu kutoa ushauri. Nikamshauri kuwa aende Kituo cha Polisi Nyakato wakamfungulie taarifa.

Lahaula kwata! Aliniangalia jicho baya, la hasira ambalo kwa mie mtaalamu wa "non-verbal communication" nilitafsiri kama vile ananiambia:

1. Wee mwehu nini ushauri gani huo.
2. Wee naye hebu ni kome sitaki ushauri wako wa kipuuzi
3...

Leo nitajitahidi sana nimtafute jioni anipe mrejesho wa kutafuta mali yake halafu nitauweka hapa JF.

MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU.
 
Sana tu. Wengi wanapenda kutendea wenzao wasiyopenda kutendewa wao
Yaani Numbisa nilimshangaa kweli yule kaka mwizi povu alilokuwa nalo, halafu ana machungu kweli ya kuibiwa, tena nadhani moyoni alisemea "nimeibiwa na tuvibaka, na hali mimi ni jambazi" Leo nitamtafuta hadi nimpate anipe mrejesho, hahahahahah
 
Mzoee halafu uje ulie hapa . Kibaka si wa kuzoea, atawaleta wanamemba wake wakushughulikie
Yuko hapo hapo mtaani wenyewe wasukuma wanaita "nzengo" sina namna ya kumkwepa, ila kwa kweli anatisha. Ushauri wako ni mzuri. Hata simkaribishi kwangu japo anapajua ila hajawahi kuingia ndani
 
Binadamu tumeumbwa hivyo. Hata kama unatenda mabaya siku zote hatupendi yaturudie. Alafu hao majira wanaroho nzuri sana au jamaa hapigagi matukio hapo mtaani?
Anapiga sana, hata wiki chache zilizopita alipiga kwa kaka mmoja hivi anafanyia TBL. Ni jambazi hatari sana.
 
hahahha, yaani ungemuona alivyokuwa amefura kwa hasira, kama unacheko za karibu kama za kwangu ungejikuta unacheka, mie nilijisemea tu moyoni, Mungu nisaidie cheko zangu zisitokeze hapa,hahahahahahahahaah
Kuwa nae makini asikuzoee huyo kibaka wa kisasa maana hapo anakutafutia gia tu
 
Anapiga sana, hata wiki chache zilizopita alipiga kwa kaka mmoja hivi anafanyia TBL. Ni jambazi hatari sana.
Sasa Dada NAHUJA nishaanza kutia shaka kwako, wewe na utanashati na umaridadi wako ( nakujua physically) umetokana wapi na urafiki na jambazi hili? kwani kapita watu wangapi hapo mtaani kwenu? kwanini aje kwako tu? hebu nitafute nikupe ushauri ( ambiere)
 
Sasa Dada NAHUJA nishaanza kutia shaka kwako, wewe na utanashati na umaridadi wako ( nakujua physically) umetokana wapi na urafiki na jambazi hili? kwani kapita watu wangapi hapo mtaani kwenu? kwanini aje kwako tu? hebu nitafute nikupe ushauri ( ambiere)
Tuko mtaa mmoja, kanisimamisha wakati napita barabarani nisingeweza kumchunia. Unajua kwenye jamii yetu tuko michangany
Sasa Dada NAHUJA nishaanza kutia shaka kwako, wewe na utanashati na umaridadi wako ( nakujua physically) umetokana wapi na urafiki na jambazi hili? kwani kapita watu wangapi hapo mtaani kwenu? kwanini aje kwako tu? hebu nitafute nikupe ushauri ( ambiere)
 
Back
Top Bottom