Nimeamini kweli mke wa mtu ni sumu

Nimeamini kweli mke wa mtu ni sumu

aiseeee... let him rest where he deserves
 
Story mzigo hivi..waiii ngoja niachie wavumilivu..!
 
tunajifunza kutokana na makosa ya watu wengne na wakat mwngne kutokana na makosa yetu yenyew!!!!!!!!
 
leo bwana ngoja nishare na washikaji wangu wa jf story za kitaa changu,kitaa changu bwana kina drama za kutosha, drama ambazo nikianza kusimulia mojabaada ya nyingine tutakesha ila hii iliyotokea jana sina budi kuwapa kamchapo kidogo.

Kama mjuavyo mitaani kwetu mara nyingi watu mnakuwa mnajuana, yule fulani anatoka na fulani, sasa basi kuna jamaa yetu bwana alikuwa anamgonga mke wa mtukwa mda mrefu sana na watu kitaani tulikuwa tunajua, mshikaji alikuwa na age kama ya miaka 28 hivi na huyo demu alikuwa same age na jamaa.

Basi bwana mshikaji akawa anajigongea kama kaoa vile, mahaba yakanoga nakama mjuavyo mahaba yakinoga lazima mtajisahau, yakanoga ile mbaya kiasi kwamba mshikaji akawa anapikiwa msosi home kwa dem anapelekewa geto kwa mchizi.

Yakaendelea kunoga zaidi na zaidi mchizi alikuwa anamtoto alizaa na dem mwingine akawaanampeleka kushinda na yule dem siku nzima.

Wakati yanafanyika haya yote mume wa yule dem alikuwa anaona na anajua ila aliuchuna kama hajui lolote ila ukweli ni kwamba alikuwa anajua kila kitu.

Kama mjuavyo washikaji sometimes mkikaa nyumbani huwa mnapiga story zinazowahusu, kuna siku bwana niliimuuliza mchizi kuhusu mahusiano yake na yule dem (mke wa mtu) mume wake anayachukuliaje ukizingatia jamaa anajua kila kitu.

Jamaa alichonijibu akasema jamaa (mume wa mtu) haongei kitu kwa mkewe kwasababu mkewe kamtengeneza vyakutosha, (muvi hili lilianza kama miaka miwili nyuma).

Basi bwana, muvi lilianza kunoga zaidi siku nne tano zilizoisha yule dem(mke wa mtu) alibeba ujauzito wa mchiz na mimba ilikuwa kubwa tu ya miezi kama sita hivi, kukatokea kutoelewana kati ya mchiz na yule dem.

Yule dem akaamua kuitoa ile mimba, kile kitendo cha yule dem kuitoa ile mimba mchiz kikamkera sana, akamwita dem geto kwake kichapo alichompa nusu amtoe roho kama sio majirani kuvunja mlango kumuokoa yule dem.

Dem kurudi kwake mumewe anamuona na majeraha, kuuliza vipi mkewe anajiumauma jamaa akajua aliyefanya hivi atakuwa mchiz.

Akamfata mchizi geto kwake akamwambia sasa wangu ulipofikia hapo sipo,akamwambia mimi sio mjinga kama mke wangu alivyokwambia kwamba amenitengeneza hivyo siongei kitu.

Ukweli ni kwamba mimi na mke wangu ni waathirika wa hiv kitambo sana ndio maana sikuwa na wasiwasi wala presha ya kukimbizana na wewe.

Kama uliamua kutembea na mke wangu sio mbaya ila mambo ya kunipigia mke wangu mimi siyataki. Jamaa akamaliza kuongea akasepa zake.

Baada ya jamaa kumfata mchiz na kumchana, jumatatu ya wiki hii akaenda kupima hiv bahati mbaya kweli akakutwa ameathirika.

Basi kurudi home mchizi akaamua anywe sumu, (hapa nawaunganishia matukio ili mpate mtiririko mzuri, kwasababu sisiwenyewe tumejua yote haya baada ya jamaa kuacha ujumbe baada ya kujiua).

Basi mchizi jumatatu (ya wiki hii) hajatokea skani, jumanne (juzi) akaja ila hakuwa yule tunayemjua, hakukaa sana akasepa.

Jana nipo job mida ya tisa hivi napigiwa simu naambiwa mchizi amekunywa sumu, amegundulika kama amekunywa sumu baada ya majirani kumsikia anakoroma ile mbaya.

Kuvunja mlango kuingia ndani wanamkuta jicho lishamtoka yupo kwenye hatua za mwisho,wakajaribu kumywesha maziwa ikashindika, wakambeba mpaka hospital wakamchomasindano mbili na dripu.

Wakaambiwa wampeleke lugalo kufika lugalo wanaanza kumpa huduma mchiz akakata roho. Mchizi aliacha barua akaelezea sababu ya kuchukua maamuzi hayo mazito.

Kubwa ni hilo la hiv, mchizi tumemzika leo mida ya saa 10. Hili ni tukio la pili sasa la kwanza lilitokea miezi kama mitatu au minne hivi iliyopita baada ya mjukuu wa mzee ruksa kujiua kisa kikiwa cha mapenzi.
i miss you much
 
Hivi unaanzaje kupiga demu bila condom? Tena humjui?
 
Dah mkuu wat a coincidence maana jana mida hiyo nilienda kutibiwa mahali nikakutana na case km hiyo ya mtu amekunywa sumu sijui ya panya.nahisi ndo yeye.polen sana
 
Dah mkuu wat a coincidence maana jana mida hiyo nilienda kutibiwa mahali nikakutana na case km hiyo ya mtu amekunywa sumu sijui ya panya.nahisi ndo yeye.polen sana

Huyohuyo..mchizi kalamba pakti 8 za sumu ya panya..lol...
 
Duuu Mke wa mtu sumu ila huyu alikuwa Bomu na kwel limelipuka...
 
Back
Top Bottom