Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika,Tanzania inawakilishwa na klabu ya Simba. Jana,Simba wamehitimisha michezo yako mitatu ya ugenini/nje ya Tanzania/kimataifa.
Katika michezo yote mitatu kule DR Congo,Misri na Algeria, Simba imepokea kichapo. Imekandikwa jumla ya mabao 12. Simba haijapata hata goli moja kwenye michezo yote ya ugenini.
Kwa kuthibitisha kuwa Simba ni wa ndani ya Tanzania,imeshinda michezo yake miwili Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na imebakiza mchezo mmoja na AS Vita ya Congo tarehe 16/3/2019.
Kwa kukosa ushindi,sare au hata goli kwa mechi tatu nje ya Tanzania,nimeamini kuwa Simba si wa kimataifa. Yanga wanastahili kuitwa hivyo! Kufungwa kila mechi ya ugenini kutaipa vipi Simba nafasi ya kusonga mbele?