Nimeachana na mke wangu

Nimeachana na mke wangu

Wabari wakuu na wana Jf
Natumaini niwazima wacha niende kwenye mkasa

Mkewangu ni mjamzito sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma now inaenda wiki ya 3 lakini baada ya kuondoka
Hii inafaa hapa jukwaa la siasa?

Halafu mbona ni kama sentensi Moja tu?
 
Usimuache. Wakati wa kelele acha azipige weee atanyamaza tu. Akipiga simu kwa ajili ya ugomvi pokea weka laud endelea na mambo mengine ataongea weweee vocha itaisha. Usitafute usuluhishi nje. Furahia maisha kwa namna nyingine.

Mwanamke wa kuacha ni mzinzi, muuaji na mchawi, mengine ni kuyachukulia kama ya mtoto mjinga.
 
Piga mashine Bob....,pendelea kula Nyanya chungu mbichi saa Moja kabla ya show....au bamia mbichi kama utaweza na limau..... Utakuja nishukuru hapa,...Hicho ni kiherehere kinamsumbua...na kinatokana na wewe kutomfikisha kileleni.

Sema nini jombaaa.sio kesi...kama vipi we mwache wahuni tumshone tukuambukize mi yutiai sugu .....
Hela muhimu kuliko mapenzi maana uzeeni hela ndio zitakutunza na sio mapenzi
 
Bado huna sababu ya kumwacha mke wako, subiri mke wako ajifungue, atakaa sawa. Ikiwa changamoto ni mimba itajulikana, ikiwa tatizo lipo kiroho itajulikana, na ikiwa tatizo linasababishwa na wewe napo itajulikana.

Tunapaswa kuelewa mwanamke mjamzito anahitaji ukaribu wa mume wake, anapoukosa na mawasiliano yakawa hafifu ujue umetengeneza mgogoro mwenyewe. Acha kutangaza kumwacha mke sio sifa, Kaa tulia, tumia akili, mambo yatakuwa sawa.
 
Wabari wakuu na wanaJF,

Natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa

Mke wangu ni mjamzito sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma now inaenda wiki ya 3 lakini baada ya kuondoka home kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na wife ni maugomvi, kulumbana na kugombana kila siku mke wangu amekuwa na maugomvi yasiyoisha sjui kwanini lakini kila siku ni maugonvi kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana coz wife amekuwa kama hakimu mfawidhi wa mahakama ya Taifa kilasiku kesi zisizo na msingi bila sababu

Kutokana na hayo kiukweli ikafika stage Dadaake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakin wapi jitihada zake hazikuzaa matunda kabsa moto ukawa ni uleule lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini lakini sipati jibu nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu coz mpaka dadake kashakaa nae na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema
Kiukweli ikafika kipindi dadaake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndo inamsumbua lakini dadaake aliniambia kuwa ni wivu tu ndo unamsumbua coz anajua upo mbali ndo maana kila siku anaanzisha maugonvi

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia text kuwa nitakupigia later niko kwa meeting lakini hakutaka kunielewa kabisa na kuanzisha ugomvi usiokuwa na sababu na kusema et namdharau sipokei simu zake

Hivi kweli wakuu hii iko sawa na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu kiukweli hii hali ikafikia stage nikashindwa wakuu kila siku maugonvi

Weekend hii nikaamua kwenda home nikaongee nae vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku maugonvi ukizingatia hata hajiurumii na hali yake nikataka anieleze nini shida na anataka tuishij. Wakuu nilijuta kurudi home kiukweli tuligomaba sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana, kiukweli naona tumeshindwana nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi home tena nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi nimetafuta nyumba ya apartment nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu na kuna hela kwenye account ambazo nimemuekea kama akiba ya emergency kutokana na hali yake na nimeshamtaarifu dadake kwa maangalizi lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa lakini sitaki amuambie mdogo wake kuwa nimempatia hela na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua then baada ya hapo nafikiri ndo mengine yatafuta kama ni talaka au vipi lakini mpaka now uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake

Wakuu ni hayo yaliojiri,kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya maugonvi kila siku hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba

Shukrani wakuu
Amekuchukia kwasababu ya mimba na anavyofanya ivyo moyoni mwake anakuwa na amani sana,usijali mwanamke akikuchukia sana anakuletea kopi yako,akishajifungua utashangaa anabadilika kabisa
 
Back
Top Bottom