Nimeachana na mke wangu leo

Nimeachana na mke wangu leo

Kumbuka umeoa binadamu sio malaika, kokote utakapoenda utakuta madhaifu ya binadamu mwingne, je utaacha wangap??

Unataka kutuambia wewe ni mkamilifu kiasi hicho?

Upendo huvumilia, hauhusudu wala hauhesabu mabaya.

Vumilia madhaifu yake coz hata wewe unayako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nineachana na mke wangu leo sababu kubwa mkewangu haniheshimu wala hanisikilizi kabisa
Awali ya Yote kama maamuzi yenu mumeyafanya usiku wa leo basi hamjaachana ila nyie wote mnaviburi na hamjui maana ya Ndoa ni nini... Labda nikuulize mambo yafuatayo kama utajisikia huru kunijibu nijibu ila pia kama utaona siyo sawa utawezA KUAACHA kujibu pia..

  • Mna Muda gani kwenye hiyo Ndoa?
  • Umri wenu wa kuzaliwa ?
  • Uwezo wenu wa kutatua matatizo yenu upoje?
  • Je Unaelewaje kutoheshimiwa ndani ya Ndoa na Kutosikilizwa Ndani ya Ndoa?
  • Je Unaamini kwa kufanya hivyo Umetibu Matatizo yako na yale yaliyo upande wako?
  • Je Kuna mzazi yeyote aliyeshilikishwa katika maamuzi yenu?
  • Je Kitu gani mnachobishania hasa mpaka uje kulalamika kuwa hakusikilizi au kukuheshimu?
  • Je kwa upande wako unatenda sawa na atakavyo?
  • Wewe unatokea Mkoa Gani wa Kuzaliwa kwa upande wa wazazi katika Tanzania.
  • Hivi Unaamini Kuwa humu kuna watu wanaendelea na Mahuiano yao lakini hizo sababu zako siyo sababuza msingi katika kile ulichokiamua na kuja kukianika Humu?
Zaidi siyo kila kitu unapashwa kukileta humu..

Akili Unazo!
 
We kabila gan kwanza?maana kuna makabila mengine wanaacha wake zao kwa sababu za kijinga km hizo au atakwambianimemuacha mke wangu sababu ya ndugu
 
Aisee tafadhali nitumie namba yake, ukisema cha nini, wenzio tunasema tutakipata lini.
 
Pole sana mkuu ni moja ya changamoto za kimaisha.Cha muhimu songa mbele hakuna kukata tamaa.Ila mimi huwa sio muumini wa suluhisisho la kuachana katika ndoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom