Nime-Design na kuunda Game ya Electronics

Nime-Design na kuunda Game ya Electronics

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,640
electronics.jpg



Nime-design na kuunda game ya electronics,Game hii niliiwaza na kuiunda hivyo wazo likawa kweli.

Game hii nimeiunda kwa vifaa vya electronics sijatumia programic card yeyote.

JINSI GAME INAVYOFANYA KAZI

Game hii inatoa point pale tu itakapo washa taa ya ACTION,ambayo inawaka kwa nusu sekunde mchezaji inatakiwa abonyeze buttons kabla taa hiyo haijazima ambapo akibonyeza button hizo kabla taa ya ACTION haijazima atapewa point 2.Kushoto moja Kulia moja.Kinyume cha hapo mchezaji anakosa point.

Ifahamike pia Ubongo wa Binadamu hutumia muda flani katika kufanya maamuzi baada ya tukio flani,hivyo taa ya ACTION ikiwaka muda wa maamuzi wa kubonyeza buttons lazima uwe speed zaidi ya speed ya taa kuwaka na kuzima.

Kama akili ikiwa slow tu basi utakosa point.

MATUMIZI YA GAME

Kuchangamsha akili na kuburudisha

Kutengeneza ushindani kati ya mtu na mtu.


NB:Kwa yeyete mwenye wazola game tunaweza kuwasiliana na nikamtengenezea.Tuwasiliane

Tazama video hii kwa kufahamu zaidi....

 
Amepata tumipigie makofi kwakwa hahahahaha...

Mkuu hongera Kwa ubunifu huo, nadhani ni mwanzo na nitoleo la kwanza la hiki kifaa Kwa ajili ya gamers au brain activator..

Pita kwenye pub/glossary mbili tatu au vibanda umiza kama una muda wa zaidi chezesha watu hata bure baadae wakinogewa chezesha Kwa pesa then wakinogewa zaidi Kuna watu watanunua kwenda kufanyia biashara sehemu mbalimbali...

Toka tembea na kifaa chako, pia kama ni mtaalamu wa programming na electronics itakuwa poa sana najua baadae unaweza fikiria kukuletea gadgets kama hizo ambazo ni za kisasa zaidi...

Mungu akuongezea kipaji na akili ya ubunifu..

Wauza bei gani hiyo kitu, weka na sifa zake hasa matumizi ya umeme ni volt ngapi? Hadi kuwaka hiyo green indicator inachukua muda gani nk?
 
Back
Top Bottom