Habari zenu wana jf, nimefurahi kupata sehemu ambayo naweza kusema imenisaidia kujua mawazo ya watu na jinsi gani tunaweza kusaidiana katika masuala mazima tunayokabiliana nayo katika maisha yetu ya kila siku. Ni mara yangu ya kwanza kupost humu na ntafurah kama mtanisaidia ktk hili suala linalontatiza...
Nilizama ktk mapenzi mazito ya msichana ambaye jina lake naomba nilihifadhi, yeye ndie alikua wa kwanza kunitamkia kuwa ananipenda, na kwakua hakua mgeni machoni mwangu, na tulishazoeana hapo mwanzo kama mtu na rafiki yake, ilibidi nikubali kuwa naye, nilimpatia mapenzi mazito na tulikua watu wenye furaha sana katka mapenzi yetu, hakuchoka kutabasamu kila alipokutana na mimi. Nilimsimulia story nzuri pamoja na kumpatia zawadi kama inavotakiwa kwa wapenzi. Naye pia hakusita kunipatia zawadi mbalimbali ambazo zilinifanya nijione ni mimi tu katika dunia ya mapenzi. Katika mwezi wa 1 mwaka 2013, aliweza kuchukuliwa na kwenda kwa Baba mkubwa wake mkoani Shinyanga, alipokua huko tuliweza kuwasiliana kupitia simu kila mara. Na aliporudi mapenzi yetu yaliendelea kama kawaida___. Huku nyumbani alikua anaish na wazazi wake mdogo wake pamoja na kaka yake, sikuzoeana kivile na kaka yake. Pia kulikua na dada mmoja hivi ambae yeye (Mpenzi wangu) aliweza kunitambulisha kuwa ni dada yake, nami niliamini. Na haikuchukua muda kumzoea kwani alikua mchangamfu, mkarimu na mpenda kusali, na aliweza kunishauri mara kwa mara kwenda kusali naye ila sikuwah kufanya hivyo,,, Lakini wakati anarudi kutoka Shinyanga, dada huyo aliyeniambia ni dada yake aliondoka pale kwao na kwenda kwa wazazi wake. Hivyo basi kumbe hakua dada yake na wala hawana mahusiano yoyote.
Sasa alipokuwa hapa nyumbani huyo Mpenzi wangu mimi, hakua na muda wa kutosha wa kukutana na mimi kama alivyokua akisema mwenyewe. Nikiwa naongea naye anaondoka, kifupi ni kuwa alionesha kunichoka, mimi sikukata tamaa, nikijaribu kumpatia zawadi kama zamani, hapo alikua anaonesha tabasamu. Kitu kingine anadai kuwa kuna watu walimfuata na kumwambia aachane na mimi, na hicho ndicho kitu ambacho kinanisumbua na sijawahi fanya kitu kama hicho. Na yeye anajua jins gani nampenda, siku hizi amebadilika na akiniona anatafuta njia nyingine ya kwenda, zile romantic moments tulizokuanazo zamani sasa hazipo.
Sijui amepatwa na jinamizi gani, nikiongea naye anaonesha kama amechoka flan mi hata simuelewi, lakn mimi bado nampenda.
Na sasa yule dada, ambaye aliniambia ni dada yake kumbe hawana udugu wowote anatumia muda mwingingi kunifariji na kunipa moyo na kuniambia huenda labda mungu hajanipangia bado mtu wa kuwa naye. Ananifariji na kunipa moyo kiasi kwamba najikuta namsahau mpenzi wangu.
***
Ambacho naomba mnisaidie ni kuwa ni muache mpenzi wangu wa zamani, niende kwa huyu dada, ambaye ananifanya nasahau matatizo nilo nayo? Au nimvumilie kwa kuamini kua ipo siku atabadilika na kuwa kama zamani? Manake nilimfanya kweli ajione mwanamke, na sikumfosi kufanya kitu alichowahi kuniambia hakimpendezi au kitu ambacho hakujiskia kufanya kwa wakati niliokuanaye.
Ningependa kumaliza kwa kusema nakushukuru wewe ambae umetumia muda wako kwa kusoma post hii, naomba ushauri wako tafadhali. Nifanyeje?