Niliyoyafanya tangu niwe Mbunge-Shukrani kwa WanaJF

Status
Not open for further replies.
Namba 9 - 22 sio kazi za kibunge kwani mwanaharakati yoyote anatakiwa au anaweza kufanya hayo. Bunge halikulipi kwa kazi hizo. Pia ukiwa mbunge wa viti maalum pia unakuwa na jimbo la Kilombero? Hapo chini kwenye red - "tenda wema nenda zako" HERI YA MWAKA MPYA

Wakuu habari!

Ni matumani yangu kuwa tumejiandaa kumaliza mwaka vizuri na kuplan vizuri for next year.

Tukiwa tunafunga mwaka nimeona niandike kwa kifupi yale niliyoyafanya kwa kipindi Cha mwaka mmoja tangu kuapishwa kuwa Mbunge wa Vitimaalum Nov 12,2010.

Taarifa hii inaonyesha utekelezaji wa Kazi za Ubunge,Kazi za chama Wilayani Kilombero na Kazi za Chama Kitaifa.

A. KAZI ZA KIBUNGE

9. Nimesomesha Wanafunzi 86 Sekondari,13 Vyuo Vikuu hawa wa Vyuo Vikuu walihitaji kutoa advance ili waweze kusajiliwa then wapate Mkopo
10. Nimeezeka madarasa mawili(2) ya shule ya Msingi Mkula
11. Nimegharamia Visima viwili vya maji
12. Nimehudumia Baba aliyekuwa kipofu kwa miaka 8 akaweza kuona tena kupitia hospitali ya CCBRT
13. Nimesaidia wagonjwa wengine zaidi ya 42 wakapata huduma za afya na kupona
14. Nimesaidia Jezi kwa Vijana katika Kata 12 Kati ya 23 za Wilaya ya Kilombero
15. Nimefanikisha ligi Mbili katika Kata Mbili-Ligi za Mpira wa Miguu na Netboli
16. Nimeshiriki kwenye fundraising katika Misikiti 3 na Makanisa 4

18. Nimeshiriki kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko Wilayani Kilombero
19. Nimefanikisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kushirki Umitashumta ngazi ya Wilaya,Mkoa na Taifa
20. Nimefanikisha Vikundi Viwili vya kina Mama Wajane kuweza Kujiajiri na kuendesha maisha yao wenyewe.
21. Nimefanikisha Vikundi 5 vya kina mama kuweza Kujiajiri.
22. Nimefanikisha Vikundi 3 vya wenye ulemavu Kujiajiri wenyewe.


Na mengine madogo madogo mengi.


With Love
Regia
 
Hivi hii tabia ya wanasiasa kuanzisha mjadala halafu hawajibu maswali wala hoja zinazojitokeza ndio trend mpya katika siasa za Tanzania? Where was the spirit of respect lost?
Mnataka kupongezwa na kusifiwa tu?
Haya, HONGERA SANA. YOU ARE PERFECT. WE ARE HERE TO WAIT ANOTHER INFORMATION FROM YOU SO WE CAN HAIL YOU MORE AND MORE.
I mean, if you dont have enough time to respond why do you start an intriguing thread?!!!
 
Hivi hii tabia ya wanasiasa kuanzisha mjadala halafu hawajibu maswali wala hoja zinazojitokeza ndio trend mpya katika siasa za Tanzania? Where was the spirit of respect lost?
Mnataka kupongezwa na kusifiwa tu?
Haya, HONGERA SANA. YOU ARE PERFECT. WE ARE HERE TO WAIT ANOTHER INFORMATION FROM YOU SO WE CAN HAIL YOU MORE AND MORE.
I mean, if you dont have enough time to respond why do you start an intriguing thread?!!!
Ukitoa pongezi na sifa utashukuriwa, ukiuliza maswali hutojibiwa.Get used to it. . . hivyo ndio Tanzania ilivyo!
 
Hivi hii tabia ya wanasiasa kuanzisha mjadala halafu hawajibu maswali wala hoja zinazojitokeza ndio trend mpya katika siasa za Tanzania? Where was the spirit of respect lost?
Mnataka kupongezwa na kusifiwa tu?
Haya, HONGERA SANA. YOU ARE PERFECT. WE ARE HERE TO WAIT ANOTHER INFORMATION FROM YOU SO WE CAN HAIL YOU MORE AND MORE.
I mean, if you dont have enough time to respond why do you start an intriguing thread?!!!

ZeMa......wape benefit of doubt mazee.......umeme wenyewe ndio kama vile....
....imagine sasa hivi yuko kule kijijini kwao.......au umesahau tulivyoambiwa huko nyuma kuwa not more than 20% ya Watanzania ndio wanapata huduma ya umeme and yet not reliable!........
 
Kwenye kazi za ubunge;
Tuseme ukiwa unafanya hizo kazi, mbunge wa hilo Jimbo anakuaga wapi??
Yaani mnashirikiana au kila mmoja kivyake??
Meanwhile 45% + uchakachuaji uliofanyika ni nyingi sana, let hope for 85% on 2015!!
Happy New Year
 
Ukitoa pongezi na sifa utashukuriwa, ukiuliza maswali hutojibiwa.Get used to it. . . hivyo ndio Tanzania ilivyo!
Regia, kwanza ningependa kutoa nasaha zangu.
Awali ya yote kuna jambo linazungumziwa na lina mantiki na ukweli. Unapoweka hoja kama hii kuna mambo yanayojitokeza ambayo yanahitaji ufafanuzi. Kwa hiyo una dhima ya kujibu hoja zitokanazo na taarifa au habari njema uliyowataarifu.
Mathalani, yupo aliyeuliza wakati una timiza majukumu hayo wabunge wa maeneo husika walishiriki vipi au hapakuwepo na ushiriki.
Swali la pili kwa ufafanuzi kama lilivyoulizwa na mmoja wetu. Je pesa za kuwasomesha ni sehemu ya mfuko wa mbunge au ni zako binafsi? Na maswali mengine kama yalivyojitokeza.

Nakubaliana na wote wanaosema huu utaratibu wa wanasiasa kutojibu hoja sio tu unatia mashaka bali unajenga hisia tofauti na ilivyokusudiwa.

Nigeshauri yafuatayo
1. Jaribu kutoa ufafanuzi kwa wale wenye hoja zinazohitaji majibu. Kwa mwanansiasa kuacha maswali au hoja ikielea ni mkakati hatari kwasababu itakapotokea wananchi wamepata majibu yao na si yako huenda usipate nafasi ya kutolea ufafanuzi kwasababu hakuna atakayekuwa na interest isipokuwa majibu aliyo nayo.

2. Kila jambo ulilolifanya nina uhakika lilikuwa na washiriki wengine nyuma yake.Mathalani mfanyakazi wa mapokezi aliyekupa makaribisho na pengine msaada wa kukupa barua au nyaraka ni sehemu kubwa ya mafanikio ya kazi yako. Hakuna anayetarajia umshukuru kila mtu kwa vile ni wengi wakiwemo wananchi. Njia rahisi ni kuwashirikisha katika kauli zako na hapo ndipo ungetumia neno ' Tumefanya hiki au kile'.
Kumbuka mbunge ni mtu na ubunge ni ofisi. Siku za usoni jaribu kulitumia neno 'Tume badala ya nime'.
 
Mbona hupigii kelele bungeni kuhusu posho za kinyonyaji wanazolipwa wabunge na kukataa kuzichukua, Ukizingatia mnapokea mshahara, mna posho kwenye vikao vya halmashauri mnapotoka, mna pesa ya mafuta na marupurupu mengi. utafanya juhudi gani mwaka 2012 ili kuondoa unyonyaji huu?

Mkuu si ni wewe ulikuwa unasema akina Zito wanatafuta umaarufu kupinga hizo posho, sasa how come unamtaka Regia kufanya kile kile ulichoita kutafuta umaarufu?
 
i really impressed with your efforts...may our allah bless u in 2012....mimi naujua moto wako coz nlikua udom pale last year....nakumbuka hata zile koo 12 zinazoiongoza ccm...ebu ukipata mda nikumbushe through my mail abele.campbel@yahoo.com
 
Mie ni mkristo lakini nakerwa sana na malalamiko ya waislam kuwa wakristo tunabebwa na MOU, kwahiyo naomba Dada regia pamoja na mambo mazuri unayofanya lakini suala la MOU lifuatilie ili waislam wasiwe na kisingizio. Mie naona serikali iondoe hata hiyo misamaha ya kodi kwasababu hakuna kitakacho haribika maana makanisa yatapandisha bei ya huduma. Nimechoka kusikiliza malalamiko ya waislam kwa vitu ambavyo tunafaidika wote.

Mkuu ni baadhi ya waislam wachache tu tena wale wasiojitambua hata wao wenyewe ndio wenye kutoa malalamiko,ila wale ambao wako smart na wanajitambua uwa wana appriciate
 
Mheshimiwa Regia.

Napenda nikupe elimu ya bure ambayo itakusaidia siku za usoni:

1) Epuka lugha ya umimi, "Nili...", "Nime...". Hiyo ni lugha ambayo inaonesha u mtu wa aina ipi.

2) Sadaka zako binafsi za kutibu watu na kuwapeleka wengine shule, ni baina yako na hao. Na kujitangazia hayo, ni kuifanya hiyo kuwa ni Rushwa ya kisiasa. Vipi, umsaidie mtu halafu umtangazie? Hii inaonesha "how low you are".

3) Unanshangaza unapokuwa jimbo la wakulima wa miwa halafu unasaidia bei ya sukari ishuke? Umewasaidia nini? Umewapelekea mashine za kusindika sukari, siku hizi zipo hata za kutia muwa mmoja tu na unapata sukari. Au umewasaidia kivipi? Mie naona kama umewaumiza.

Ntarudi kukupa darsa nikiwa kwenye kompyuta,siwezi kuandika mengi nipo kwenye "mobile phone".

Ahsante ndugu, umesema yote, hata sie ambao si wabunge tumetoa misaada mbalimbali bila kuja kusema hapa jf. Hata maandiko yanasema unapotoa sadaka mkono wako wa kushoto usijue. Msaada ni sadaka na haitangazwi otherwise itakuwa rushwa ya kisiasa.
 
Dada Regia wewe ni jembe la ukweli. HONGERA SANA KWA ULOTEKELEZA, natumaini mwaka huu utatekeleza mengi zaidi. Tupo bega kwa bega hadi kieleweke 2012. Mungu akupe nguvu na hekima zaidi uwatumikie wananchi wako kikamilifu. Nilikuona mara ya kwanza mlipokuja Mzumbe na kina Dr wa ukweli mkatufungulia tawi la cdm pale changarawe. TUPO PAMOJA. Cdm for life, viva Regia.
 
Wakuu habari!

Ni matumani yangu kuwa tumejiandaa kumaliza mwaka vizuri na kuplan vizuri for next year.

Tukiwa tunafunga mwaka nimeona niandike kwa kifupi yale niliyoyafanya kwa kipindi Cha mwaka mmoja tangu kuapishwa kuwa Mbunge wa Vitimaalum Nov 12,2010.

Taarifa hii inaonyesha utekelezaji wa Kazi za Ubunge,Kazi za chama Wilayani Kilombero na Kazi za Chama Kitaifa.

A. KAZI ZA KIBUNGE
Tangu nimeapishwa nimefanikiwa kufanya Kazi mbalimbali za Kibunge Wilayani Kilombero,Jimbo ambalo niligombea na kupata Kura 38,550 sawa na asilimia 45 ya kura zote zilizopigwa. utekelezaji wa awamu hii ulikuwa ni QUICK WINS. Quick zifuatazo zimefanyika;
1. Nimepigania bei ya Sukari ishuke -Kuna maeneo Bei imeshuka lakini maeneo mengine hali bado ni mbaya. Kilombero ni Wilaya inayozalisha Sukari, Kiwanda Cha Illovo hivyo bei ya Sukari unapaswa kuwa chini kuliko maeneo yasiyodhalisha Sukari.
2. Nimepigania kituo Cha Polisi Cha Wilaya kiboreshwe-kimeboreshwa
3. Nimepigania kituo Cha afya Cha Mlimba kipatiwe Maji na Ambulance lirudishwe hivi vyote vimefanyika.Ambulance ilikuwa gereji zaidi ya miezi Sita mwaka 2010.
4. Nimepigania utekelezaji wa huduma bure kwa Wajawazito,Watoto chini ya Miaka Mitano,Wazee na Wenye Ulemavu-Kuna maeneo imefanikiwa maeneo mengi bado.
5. Nimetetea haki za Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Na KPL-Baadhi ya Kero zimetekelezwa lakini nyingine bado-Suala la Maslahi bado ni tete,suala la Usalama Kazini bado ni tete.
6. Nimetetea na kusimamia kero ya Wakulima na Wafanyabiashara ya kuongezeka kwa Ushuru bila kushirikishwa katika hatua zote muhimu.
7. Nimepigania haki ya Umeme kwa Wananchi wa Kilombero kwani tunavyanzo viwili ya umeme,Kihansi na Kidatu.REA imeenda kule ila inasua sua sana lakini Wizara imetuhakikishia kuwa inatekeleza azma yake ya kupeleka umeme maeneo yote ya karibu na vyanzo vya umeme.
8. Nimepigania barabara ya Kidatu-Ifakara kwa kiwango Cha lami-imeshindikana kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
9. Nimesomesha Wanafunzi 86 Sekondari,13 Vyuo Vikuu hawa wa Vyuo Vikuu walihitaji kutoa advance ili waweze kusajiliwa then wapate Mkopo
10. Nimeezeka madarasa mawili(2) ya shule ya Msingi Mkula
11. Nimegharamia Visima viwili vya maji
12. Nimehudumia Baba aliyekuwa kipofu kwa miaka 8 akaweza kuona tena kupitia hospitali ya CCBRT
13. Nimesaidia wagonjwa wengine zaidi ya 42 wakapata huduma za afya na kupona
14. Nimesaidia Jezi kwa Vijana katika Kata 12 Kati ya 23 za Wilaya ya Kilombero
15. Nimefanikisha ligi Mbili katika Kata Mbili-Ligi za Mpira wa Miguu na Netboli
16. Nimeshiriki kwenye fundraising katika Misikiti 3 na Makanisa 4
17. Nimekuwa sehemu ya kufanikisha Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishirki Cha Mt Fransisco
18. Nimeshiriki kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko Wilayani Kilombero
19. Nimefanikisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kushirki Umitashumta ngazi ya Wilaya,Mkoa na Taifa
20. Nimefanikisha Vikundi Viwili vya kina Mama Wajane kuweza Kujiajiri na kuendesha maisha yao wenyewe.
21. Nimefanikisha Vikundi 5 vya kina mama kuweza Kujiajiri.
22. Nimefanikisha Vikundi 3 vya wenye ulemavu Kujiajiri wenyewe.
23. Nimefanya Mikutano ya Hadhara ya Elimu ya Uraia pamoja na Shukrani zaidi ya 20.

Na mengine madogo madogo mengi.

B. KAZI ZA CHAMA WILAYANI KILOMBERO

Katika kukuza chama Wilayani Kilombero nimefanikiwa kufanya yafuatayo;
1. Nimelipia na kufungua Ofisi za CHADEMA katika Kata 5
2. Nimefungua na Kuzindua Matawi 13 yaliyojengewa na yenye Uongozi wa Kudumu
3. Nimeingiza Wanachama zaidi ya 8,000

C. KAZI ZA CHAMA ZA KITAIFA
1. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Kanda ya Ziwa katika Mikoa yote ya Kanda hiyo katika kupigania haki za watanzania.
2. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kasoro (Mikoa ya Iringa na Ruvuma) katika kupigania haki za watanzania.
3. Nimeshiriki kwenye Kazi za Siasa Arusha - Sakata la Kuvuliwa Uanachama Madiwani kusaka muafaka.
4. Nimeshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo wa Igunga
5. Nimeshiriki kutoa Mafunzo ya Mapungufu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2011 katika Mkoa wa Ruvuma
6. Nimeshiriki kwenye Siasa za Vyuo Vikuu, Makongamano, Mikutano ya Hadhara na Uzinduzi wa Matawi
7. Nimeshiriki kwenye Siasa za Dodoma, Singida na Morogoro.

Natambua nilipaswa kuyafanya zaidi ya haya lakini kutokana na sababu mbalimbali hayo ndio niliyofanikiwa kuyafanya. Angalau nimefanikiwa kufanya karibu asilimia 70 ya niliyopanga kuyafanya kwa mwaka huu 2011 kama Mbunge wa Vitimaalum Wilayani Kilombero.

Naomba nichukue fursa hii pia kuwashukuru wanaJF wote kwa support yenu kwangu kwa hakika ninawashukuru sana tena sana.JF imekuwa ni nyumbani, JF imekuwa ni darasa, Vile vile JF imekuwa ni Tanuru la Moto maana wakati mwingine huwa ninaingizwa kwenye moto hasa. Na mwisho nichukue fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine, tuanze upya mwaka ujao..

With Love
Regia


much respect kamanda, una uwezo tunategemea makubwa zaidi mwaka huu ,
 
Mheshimiwa Regia.

Napenda nikupe elimu ya bure ambayo itakusaidia siku za usoni:

1) Epuka lugha ya umimi, "Nili...", "Nime...". Hiyo ni lugha ambayo inaonesha u mtu wa aina ipi.

2) Sadaka zako binafsi za kutibu watu na kuwapeleka wengine shule, ni baina yako na hao. Na kujitangazia hayo, ni kuifanya hiyo kuwa ni Rushwa ya kisiasa. Vipi, umsaidie mtu halafu umtangazie? Hii inaonesha "how low you are".

3) Unanshangaza unapokuwa jimbo la wakulima wa miwa halafu unasaidia bei ya sukari ishuke? Umewasaidia nini? Umewapelekea mashine za kusindika sukari, siku hizi zipo hata za kutia muwa mmoja tu na unapata sukari. Au umewasaidia kivipi? Mie naona kama umewaumiza.

Ntarudi kukupa darsa nikiwa kwenye kompyuta,siwezi kuandika mengi nipo kwenye "mobile phone".

kweli kabisa...! Hii ya wagonjwa na wanafunzi,ndiyo imekaa kama ya kujitafutia umaarufu na kujaza page..
 
Hapo kwenye C.1&2.,Hivi siku hizi ukishiriki maandamano ni moja ya CV?!
 
mimi siukupongezi kwanza mpaka unifafanulie mabo yafyatayo:
1. ninvyofahamu mimi wabunge wa viti maalum huchaguliwa/kuteuliwa kutokana na mikoa: iweje katika kazi zote ulizozifanya zijikite katika jimbo la Kirombero? vipi kuhusu maeneo mengine yanayounda mkoa wa Morogoro yanawakilshwa na mbunge gani wa viti maalum? huoni kuwa kujikita zaidi katika jimbo la kirombero utakuwa umemsaidia kazi mbunge wa jimbo hilo hivyo akajisifu kuwa yeye ndio aliyotenda hayo yote?


2. umeeleza zaidi kazi zako za kibunge katika ngazi ya jimbo, lakini ninavyofahamu mimi mbunge pia anajukumu la kupigania mambo ya kitaifa; ni mambo gani ya kitaifa ya kibunge ambayo wewe umeyapigania na yakafanikiwa?

3. kuna huu ugonjwa wa wabunge kutumia posho zao moja kwa moja katika kutatua kero za wananchi kitu ambacho si sahihi maana kufanya hivyo ni sawa na kuwapa samaki wananchi badala ya kuwafundisha kuvua samaki; je wewe umewawezesha vipi wananchi ili wajiletee maendeleo yao wenyewe na kuacha tabia ya kuomba omba kwa wabunge wao?
 
Nilichokigunduwa kwenye thread hii kuna watu wanitwa hater, hao ni kazi yao kuhate tu, kuna wengine humu hata kwenye ngazi za familia zao ukifanyika uchaguzi hawawezi kuchagulika, sasa huwa nashangaa mtu ambae aliaminiwa na wapiga kura zaidi ya 30,000 eti aje kubezwa na mpuuzi mwingine ambaye anatumia siasa za kimtandao + fake name!

Wanaohoji kwamba yeye sio mbunge wa jimbo, je na kuna mbunge anaemiliki kata? si kila kata ina diwani wake? je kukiwa na swala la kimaendeleo kwenye kata ni nani anapaswa kupewa credit?

Kuna wanaosema Regia anatafuta cheap popurality! swali, hivi kuna mwanasiasa gani dunia hii asiyetafuta umaarufu? Nikirudi kwa huyu Kikongwe Faiza Foxy, wewe mama unazeeka vibaya na chuki zitakufanya uwe mchawi uzeeni, unaposema unapomsaidia mtu hupaswi kutangaza, je umewahi kumuambia Rais JK kwamba pale anapotoa msaada wa mbuzi wa sikukuu kwa ajili ya watoto yatima asiite vyombo vya habari kuripoti tukio lile?
 
Hongera sana dada Regia; mm pia nikiwa mdau wa Kilombero nashukuru kusikia hayo. Ila tu nataka kukutahadharisha machache kuwa ingefaa kama mbunge wa CHADEMA mkaondoka katika mtego ule wa wale wa CCM wakuhamishia maendeleo kwenye mifuko yenu badala yake kujenga uwezo wa wananchi na Taasisi kuleta maendeleo endelevu. Tukifanya tathmini ya uhakika pesa ulizo toa mfukoni kwako zingetosha kubadilisha Kilombero kwa kiasi kikubwa kama zingetumiwa kuwezesha kaya kuzalisha wao wenyewe kwa mikono yao ili kukidhi hayo yote wewe uliyefanya kwakutumia nguvu zako ambazo haziwezi kuwa kubwa kiasi cha kuleta significant impact.

Kilombero inafursa nyingi za kubadilika na kuwa sehemu ambapo pengine wengi watatamani kuja kuishi. Changamoto kubwa ni jinsi ardhi inavyotumiwa kwani uzalishaji nimdogo (Less than 5 bags per acre) mno na wale wenye mashamba makubwa ambao wamechukua zaidi ya 70% ya ardhi yote inayolimwa wanafanya kilimo kinacho leta uharibifu wa mazingira huku wakisukuma kaya kwenye maeneo ambayo yanaharibu zaidi ardhi oevu ndiyo maana hata kukatokea mafuriko yaliyosababisha hasara za mali na maisha.

Utambue kuwa 70% ya umeme wa unaozalishwa kwa maji unatoka Kilombero (Eastern arc Mountains) kulihudumia Taifa wakati ni chini ya 1% ya wananchi wa Kilombero wana tumia umeme. Hii ni hatari sana kwa Taifa lenyewe ndiyo maana tumesikia kuwa mabwa yanakauka na umeme unakuwa tatizo kwa watanzania wote kwasababu garama ya umeme wamebeba wananchi wa Kilombero ambao serikali inatumia nguvu nyingi sana kuwadhibiti wasikate miti kwaajili ya matumizi ya nishati na kilimo vitu ambavyo ni vya msingi kwa maisha ya raia wa maeneo hayo. Ni vyema ukatazama changamoto hizi na kuwasaidia wananchi hao siyo kupitia nguvu zako no bali kuwaongoza wao kuweza kuleta suluhisho la matatizo yao ambayo ukitumia wataalamu (siyo wataalamu-wanasiasa bali wataalamu wenye ujuzi wa kweli) inavyotakikana ni raihisi mno nawe utaheshimika siku zote kama mbunge.
 
Wakuu naamini tumeanza mwaka mpya vizuri.

Ninawashukuru wote kwa michango yenu nimeipokea yote.Nitumie fursa hii pia kujibu baadhi ya hoja zilizoibuka humu .
1. Kuna wengine wamenipiga shuti kuwa nimekuwa kimya sijajibu hoja ,ukweli ni kuwa kuna baadhi ya hoja nimezijibu lakini pia nisingweza kujibu kila hoja kwasababu Kuu mbili,moja ni kuwa kuna hoja zingine zinaibuliwa ili kukuchokoza tu hivyo imenibidi nipotezee ,kutumia jina lako halisi JF ni kazi ngumu sana unahitaji uwe na moyo wa jiwe.Nilipokuwa GenderSensitive nilikuwa huru sana ninapoanzisha sredi nilikuwa najibu kila hoja moja kwa moja kwa sasa ningumu kwa kweli..Wahenga wanasema Silence is Gold. Pili nilikuwa nasubiri hoja ziwe nyingi ili zile zitakazojirudia ndio nizijibu kwa pamoja.
2.Kuna hoja imeibuliwa na wengi ya kuacha kutumia neno nime badala yake iwe Tume,nimeipokea na kosa hili halitajirudia tena.
3. Kuna hoja imeibuliwa kuwa je unapokuwa Mbunge wa Vitimaalum unakuwezaje kufanya Kazi za Jimbo?Jibu ni hivi,Mbunge wa Vitimaalum anatakiwa kushugulikia kero za Mkoa kwani yeye anakuwa ni mwakilishi wa Mkoa kwa mujibu Katiba na Kanuni zilizopo hivyo napaswa kushugulikia kero za Mkoa wa Morogoro ama kwa kuzungumza Bungeni,kwenye vikao vya Madiwani au kwanjia nyingine zozote halali.Lakini hapa ikumbukwe kuwa kwenye Uchaguzi wa Mwaka Jana niligombea Jimbo la Kilombero ili nisaidie kuleta maendelea kwenye Wilaya hii iliyojaliwa Rasilimali nyingi nikapata Kura 38,550 watu hawa waliacha shughuli zao wengine wakatembea umbali ndefu Kwenda kunipigia kura,wakapanga na foleni ili niwe mtumishi wao,sikupata Ubunge wa Jimbo nimepata wa Vitimaalum kwa hakika siwezi kuacha kuwatumikia Wananchi hawa.Haiingii akilini Bungeni niisemee Kilombero halafu pale ninapoweza kutekeleza kwa vitendo nisifanye hivyo eti kwakuwa sio Mbunge wa Jimbo.Nikiwa Kijana ambaye nimejaliwa akili,utashi,Ujasiri na uthubutu ninapenda kuona Wilaya yangu inapata Maendeleo endelevu hivyo kwayale ambayo yapo ndani ya uwezo wangu iwe kiushauri au kifedha nitayatekeleza bila kusubiri Mbunge wa Jimbo afanye.
4. Kuna hoja imeibuliwa hapa kuwa je yaliyofanyika yamefanyika kwa fedha binafsi ama la,jibu ni kuwa baada ya kuwa Mbunge nimeanzisha Mfuko kwajili ya kusaidia Maendeleo Wilayani Kilombero na Mfuko huu unajulikana kwa jina la Mfuko wa Maendeleo Kilombero ambao unachangiwa na wahisani mbalimbali wa ndani na nje ya Kilombero so far bado natafuta wahisani wa nje ya nchi na nitakuja pia hapa JF kutembeza Bakuli.Lakini kwa kiwango kikubwa Mfuko huu unafadhiliwa na vyanzo vyangu binafsi so far,najitahidi mwaka huu pesa nyingi zaidi zitoke kwenye vyanzo vya nje kama nyie ndugu zangu wanaJF na wengineo.
5. Kuna hoja zimeibuka kuwa je Mbunge wa Jimbo anaweza akasema kuwa amefanya yeye,jibu ni kuwa mambo mengi ya niliyoyafanya yako wazi kwa wapiga kura.Mara baada ya kuwa Mbunge tulifungua Ofisi ya Mbunge pale Ifakara inayofanya Kazi Siku za Kazi,Jumatatu hadi Ijumaa hivyo kupitia Ofisi ndipo tunapopokea na kutatua kero za Wananchi na tunarekodi kila linalofanyika kwa maandishi,picha n.k.Na mengine tumefanya in public hivyo hata alisema amefanya,tunazorekodi.
6. Kuna hoja imeibuka kuwa niliyoyafanya nisadaka hivyo yapaswa kuwa Siri jibu ni kuwa niliyoyafanya sio Sadaka,nimetimiza wajibu wangu kama Mwakilishi wa Wananchi ninayepata Mkate wa kila Siku kwa Kodi za Wananchi,Huwa sitoi Sadaka kwa Mtindo huu..

Hii nilioandika hapa JF sio ripoti kamili ni kasehemu tu ya ripoti niliamua niweke in public,a detailed report will be submitted to the part
Mwisho ninawatakia mwaka mpya mwema.
Regia
 
Ingekuwa la maana zaidi kama hayo uliyoyaweka humu Jamvini ungekwenda kuwambia wananchi wa jimbo lako

Sasa wewe hujui kwamba baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Kilombero wamo humu JF?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom