Niliyoyafanya tangu niwe Mbunge-Shukrani kwa WanaJF

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Wakuu habari!

Ni matumani yangu kuwa tumejiandaa kumaliza mwaka vizuri na kuplan vizuri for next year.

Tukiwa tunafunga mwaka nimeona niandike kwa kifupi yale niliyoyafanya kwa kipindi Cha mwaka mmoja tangu kuapishwa kuwa Mbunge wa Vitimaalum Nov 12,2010.

Taarifa hii inaonyesha utekelezaji wa Kazi za Ubunge,Kazi za chama Wilayani Kilombero na Kazi za Chama Kitaifa.

A. KAZI ZA KIBUNGE
Tangu nimeapishwa nimefanikiwa kufanya Kazi mbalimbali za Kibunge Wilayani Kilombero,Jimbo ambalo niligombea na kupata Kura 38,550 sawa na asilimia 45 ya kura zote zilizopigwa. utekelezaji wa awamu hii ulikuwa ni QUICK WINS. Quick zifuatazo zimefanyika;
1. Nimepigania bei ya Sukari ishuke -Kuna maeneo Bei imeshuka lakini maeneo mengine hali bado ni mbaya. Kilombero ni Wilaya inayozalisha Sukari, Kiwanda Cha Illovo hivyo bei ya Sukari unapaswa kuwa chini kuliko maeneo yasiyodhalisha Sukari.
2. Nimepigania kituo Cha Polisi Cha Wilaya kiboreshwe-kimeboreshwa
3. Nimepigania kituo Cha afya Cha Mlimba kipatiwe Maji na Ambulance lirudishwe hivi vyote vimefanyika.Ambulance ilikuwa gereji zaidi ya miezi Sita mwaka 2010.
4. Nimepigania utekelezaji wa huduma bure kwa Wajawazito,Watoto chini ya Miaka Mitano,Wazee na Wenye Ulemavu-Kuna maeneo imefanikiwa maeneo mengi bado.
5. Nimetetea haki za Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Na KPL-Baadhi ya Kero zimetekelezwa lakini nyingine bado-Suala la Maslahi bado ni tete,suala la Usalama Kazini bado ni tete.
6. Nimetetea na kusimamia kero ya Wakulima na Wafanyabiashara ya kuongezeka kwa Ushuru bila kushirikishwa katika hatua zote muhimu.
7. Nimepigania haki ya Umeme kwa Wananchi wa Kilombero kwani tunavyanzo viwili ya umeme,Kihansi na Kidatu.REA imeenda kule ila inasua sua sana lakini Wizara imetuhakikishia kuwa inatekeleza azma yake ya kupeleka umeme maeneo yote ya karibu na vyanzo vya umeme.
8. Nimepigania barabara ya Kidatu-Ifakara kwa kiwango Cha lami-imeshindikana kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
9. Nimesomesha Wanafunzi 86 Sekondari,13 Vyuo Vikuu hawa wa Vyuo Vikuu walihitaji kutoa advance ili waweze kusajiliwa then wapate Mkopo
10. Nimeezeka madarasa mawili(2) ya shule ya Msingi Mkula
11. Nimegharamia Visima viwili vya maji
12. Nimehudumia Baba aliyekuwa kipofu kwa miaka 8 akaweza kuona tena kupitia hospitali ya CCBRT
13. Nimesaidia wagonjwa wengine zaidi ya 42 wakapata huduma za afya na kupona
14. Nimesaidia Jezi kwa Vijana katika Kata 12 Kati ya 23 za Wilaya ya Kilombero
15. Nimefanikisha ligi Mbili katika Kata Mbili-Ligi za Mpira wa Miguu na Netboli
16. Nimeshiriki kwenye fundraising katika Misikiti 3 na Makanisa 4
17. Nimekuwa sehemu ya kufanikisha Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishirki Cha Mt Fransisco
18. Nimeshiriki kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko Wilayani Kilombero
19. Nimefanikisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kushirki Umitashumta ngazi ya Wilaya,Mkoa na Taifa
20. Nimefanikisha Vikundi Viwili vya kina Mama Wajane kuweza Kujiajiri na kuendesha maisha yao wenyewe.
21. Nimefanikisha Vikundi 5 vya kina mama kuweza Kujiajiri.
22. Nimefanikisha Vikundi 3 vya wenye ulemavu Kujiajiri wenyewe.
23. Nimefanya Mikutano ya Hadhara ya Elimu ya Uraia pamoja na Shukrani zaidi ya 20.

Na mengine madogo madogo mengi.

B. KAZI ZA CHAMA WILAYANI KILOMBERO

Katika kukuza chama Wilayani Kilombero nimefanikiwa kufanya yafuatayo;
1. Nimelipia na kufungua Ofisi za CHADEMA katika Kata 5
2. Nimefungua na Kuzindua Matawi 13 yaliyojengewa na yenye Uongozi wa Kudumu
3. Nimeingiza Wanachama zaidi ya 8,000

C. KAZI ZA CHAMA ZA KITAIFA
1. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Kanda ya Ziwa katika Mikoa yote ya Kanda hiyo katika kupigania haki za watanzania.
2. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kasoro (Mikoa ya Iringa na Ruvuma) katika kupigania haki za watanzania.
3. Nimeshiriki kwenye Kazi za Siasa Arusha - Sakata la Kuvuliwa Uanachama Madiwani kusaka muafaka.
4. Nimeshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo wa Igunga
5. Nimeshiriki kutoa Mafunzo ya Mapungufu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2011 katika Mkoa wa Ruvuma
6. Nimeshiriki kwenye Siasa za Vyuo Vikuu, Makongamano, Mikutano ya Hadhara na Uzinduzi wa Matawi
7. Nimeshiriki kwenye Siasa za Dodoma, Singida na Morogoro.

Natambua nilipaswa kuyafanya zaidi ya haya lakini kutokana na sababu mbalimbali hayo ndio niliyofanikiwa kuyafanya. Angalau nimefanikiwa kufanya karibu asilimia 70 ya niliyopanga kuyafanya kwa mwaka huu 2011 kama Mbunge wa Vitimaalum Wilayani Kilombero.

Naomba nichukue fursa hii pia kuwashukuru wanaJF wote kwa support yenu kwangu kwa hakika ninawashukuru sana tena sana.JF imekuwa ni nyumbani, JF imekuwa ni darasa, Vile vile JF imekuwa ni Tanuru la Moto maana wakati mwingine huwa ninaingizwa kwenye moto hasa. Na mwisho nichukue fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine, tuanze upya mwaka ujao..

With Love
Regia
 
Hongera sana Regia. Kazi nzuri na endeleza jitihada zaidi.

Changamoto kubwa unayoipata ni kwamba mbunge mwenzako naye anaweza kuclaim kuwa yeye ndio aliyofanya hayo ya kuboresha huduma za afya etc. Hata hivyo cha msingi ni kwamba huduma imekuwa bora.

Kwenye point namba 9 mpaka 15 katika list ya mambo uliyofanya jimboni ingekuwa vizuri kama ungetoa ufafanuzi jinsi ulivyofanikisha hayo. Je, ulitumia posho zako au source gani ya funds za kuwezesha hayo?
 
Mkuu ahsante sana kwa Mlishonyuma huo mzuri. Ila mkuu epuka neno nime.. tumia neno tume... Hii itaonyesha kwamba umeshirikiana na wananchi kufanya yote hayo kwani bila wananchi wa kilombero hayo yote yasingefanyika!

Umefanikiwa mengi. Hata hiyo barabara unayosema imeshindikana mimi najua imewezekana.
 
Hongera sana Dada,

Ila hapo kwenye kazi za chama kitaifa ulipotumia neno maandamano kuna uwezekano wengine wakalitumia kukukebehi, nadhani ungetumia neno kupigania haki za watanzania kupitia maandamano. Kwa sababu lengo la chama au taasisi au jamii yoyote ile kufanya maandamano ni kwa sababu ya kupigania haki zao. Ila kwa kweli umenifurahisha sana.

Nakutakia kila la heri dada yangu.
 
Hongera dada kwa kazi nzuri, hatahivyo sehemu kubwa ya mafanikio yametokana na mazingira bora yaliyowekwa uko wilayani na serikali ya CCM
 
Dada regia namba 8 barabara ya kidatu ifakara naomba uendlee kuipigania nikilometa chini ya sabini lakini kwa ubovu wake unatumia masaa zaidi ya mawili hata matatu kipindi cha mvua ndio kabisa aifai ukiwa na gari dogo unaweza lala njiani.wekeni mkaka na wabunge wenzako mama kombani na dk mponda tena ni mawazi wanashdwaje kuharakishia maendeleo wananch wao.congratulation dada and happy new year,office ya cdm ipo wapi maeneo ya kibaoni feb nitakuja uko!
 
Hongera mbunge wa viti maaalum. vipi kuhusu mkataba wa MOU uliwahi kuuliza swala hili bungeni? maana jamii ya kiislam huwa wanaulalamikia sana kwa kipindi kirefu. 2012 unaweza kumuuliza Mh waziri mKUU pINDA ktk maswala ya papo kwa papo?

Hata kama serikali ikisema tuko tayari kufanya MOU na waislamu. Hebu orodhesha basi waingie nao MOU kwenye nini i.e Hospitali zipi, vyuo vipi ama kwa huduma gani ya kijamii wanayotoa isiyo na ubaguzi ? au wao wanataka tu kusiwe na MOU?
 
[Taarifa hii inaonyesha utekelezaji wa Kazi za Ubunge,Kazi za chama Wilayani Kilombero na Kazi za Chama Kitaifa.

A.KAZI ZA KIBUNGE
Tangu nimeapishwa nimefanikiwa kufanya Kazi mbalimbali za Kibunge Wilayani Kilombero,Jimbo ambalo niligombea na kupata Kura 38,550 sawa na asilimia 45 ya kura zote zilizopigwa. utekelezaji wa awamu hii ulikuwa ni QUICK WINS. Quick zifuatazo zimefanyika;
1. Nimepigania bei ya Sukari ishuke -Kuna maeneo Bei imeshuka lakini maeneo mengine hali bado ni mbaya.Kilombero ni Wilaya inayozalisha Sukari,Kiwanda Cha Illovo hivyo bei ya Sukari unapaswa kuwa chini kuliko maeneo yasiyodhalisha Sukari.

Imeshuka kwa kiasi gani sehemu ulizopigania ili tuweze kupima hayo mafanikio, sehemu ambazo haijashuka sukari ni sh.ngapi?

6.Nimetetea na kusimamia kero ya Wakulima na Wafanyabiashara ya kuongezeka kwa Ushuru bila kushirikishwa katika hatua zote muhimu.
Ushuru ulikua kiasi gani na baada ya kuwapigania wananchi wako ni kwa kiasi gani ushuru umeshuka au umebaki palepale?

19.Nimefanikisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kushirki Umitashumta ngazi ya Wilaya,Mkoa na Taifa

Umefanikisha kivip?, kiushauri,kifedha au.....

20.Nimefanikisha Vikundi Viwili vya kina Mama Wajane kuweza Kujiajiri na kuendesha maisha yao wenyewe.

Umefanikisha kivip?, kiushauri,kifedha au.....


21. Nimefanikisha Vikundi 5 vya kina mama kuweza Kujiajiri.

Umefanikisha kivip?, kiushauri,kifedha au.....

22.Nimefanikisha Vikundi 3 vya wenye ulemavu Kujiajiri wenyewe.

Umefanikisha kivip?, kiushauri,kifedha au.....


Ufafanuzi tafadhari kwenye red, hongera kwa kutupatia tathimi ya kaz ulizozifanya
 
Hongera mbunge wa viti maaalum. vipi kuhusu mkataba wa MOU uliwahi kuuliza swala hili bungeni? maana jamii ya kiislam huwa wanaulalamikia sana kwa kipindi kirefu. 2012 unaweza kumuuliza Mh waziri mKUU pINDA ktk maswala ya papo kwa papo?

Hata kama serikali ikisema tuko tayari kufanya MOU na waislamu. Hebu orodhesha basi waingie nao MOU kwenye nini i.e Hospitali zipi, vyuo vipi ama kwa huduma gani ya kijamii wanayotoa isiyo na ubaguzi ? au wao wanataka tu kusiwe na MOU?


Dears naona mshaanza badilisha muelekeo wa mada husika..... Sio siri MOU ni delicate matter an entity in itself which requires it's discussion.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom