Niliwahi kusema, CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Niliwahi kusema CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Hizi shida zote wanazopata hadi kulaghai akina Mzee Halima na wenzake zingeweza kuepukika kama wange-apply akili kidogo tu kwenye uchaguzi. Katika majimbo 274 ya uchaguzi wangeachia hata majimbo 50 tu kwa upinzani, halafu "wakajizolea" 224 yaliyobaki.

Kwa kufanya hivyo wangepata faida zifuatazo;

1. Wangeweza "kuulaghai" ulimwengu (hasa mabeberu) kwamba uchaguzi ulikua huru na haki.

2. Wangeepusha mgongano kati ya vyama vya siasa na tume ya uchaguzi.

3. Wangejihakikishia kuwepo kwa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

4. Wangejihakikishia kwamba zile kamati 3 (PAC, LAC na POAC) ambazo tumetunga sheria kwamba ni lazima ziongozwe na upinzani, zinapata wapinzani wa kuziongoza.

5. Siri(kali) ingejihakikishia kuvuna "matrilioni" kiulaini kutoka kwa mabeberu kutokana na kamati hizo kuongozwa na upinzani.

Lalini hakuna aliyeliona hili. Sio waziri, sio mbunge, RC, DC wala watu wa system. Hapo ndo utaamini chama chakavu hakina "think tank" kabisa. Labda wangemshirikisha ndugu yangu Thadei Ole Mushi angeweza kuwasaidia maana kichwa chake kina akili nyingi sana kabla hajanywa mbege.

Lakini wote walikua wanashangilia "uchafuzi" wa "TANO TENA" na kufurahia upinzani kufutika bungeni. Ghafla wanakuja kugundua bila upinzani bungeni kuna matrilioni wanapoteza. Wakalazimika kubuni "mbwinu" za kuwahadaa akina mzee Halima na wenzake.

Kumbe wangekua smart tangu mwanzo huu mchezo ulikua unaisha mapema sana bila hata kelele. Hii mijitu inapenda namba lakini haijui hesabu.!
 
Maisha Marefu kwa Malisa JG.

"Wanabunwi Mbwinu " Hahahaa ile Clip inachekesha sana!!! MITANO TENA wengi Vichwa EMpTy aka Zero Brain ,wanapenda namba(yaani wawe na wabunge wote kutoka chama chao) lakini hawajui hesabu.(hapa ndipo wanaforce kina Mzee Mdee na Mkewe waingie Bungeni)
 
Rais nina amini anatamani ule USHINDI WA KISHINDO aufute kwa kifutio na ile "MITANO TENA" iishe haraka sana, au lasivyo watampa BP mabeberu, ikulu patakua hapa laliki usingizi. Maana sio kwa huu mtungo waliomuanzishia mabeberu hata kabla hajamaliza miezi miwili katika hio miaka mitano.

Wameanza kuivua "SKETI" serikali kwa kuweka wazi zile "PROPAGANDA ZA UONGO" kuhusu sakata la mkuu kujitamba kwamba Tanzania hakuna Covid-19, sala na maombi ndio yameondoa maambukizi.

Mara paap, wakamwaga list ya "MISAADA NA MIKOPO" serikali ilioomba kwaajili ya kupambana na Covid-19 (Ambayo sisi raia tulikua hatuijui kabisa, na wasinge mwaga mtama tusingejua).

BAADHI ya hiyo Mikopo na msaada yenyewe ya kupambana na Covid-19 kama ifuatayo;

1) € 27 Million - Kutoka kwa EUROPEAN UNION (Msaada)

2) $ 143 Million - Kutoka kwa INTERNATIONAL MONETARY FUNDS (Mkopo Mwezi June).

3) $ 3.4 Million - Kutoka kwa WORLD BANK (Mkopo Mwezi September).

4) $ 50.7 Million - Kutoka kwa AFRICAN DEVELOPMENT BANK (Mkopo Mwezi October).

5) $ 11 Million - Kutoka kwa GLOBAL FUND (Mkopo).

HALAFU WAKAANGALIA tundu gani serikali itataka kuchomokea. Majibu yakawa tuivue serikali ya tanzania na "BLAUZI NA SHUMIZI" kabisaaa;

1) Kuzuia misaada. Ili nchi isipate hela kwenye bajeti.

2) Kupiga propaganda za kuwatisha watalii wasije Tanzania, kwamba kuna maambukizi ya Covid-19 mengi sana, sambamba na ugaidi. Ili nchi isipate kipato cha kuisaidia bajeti kutokana na "UTALII".

Kiburi/Matusi/Kejeli/Dharau/Uongo wa viongozi wetu sasa zimesababisha mabomba ya hela kufungwa yote. Kilichobakia ni TRA/TRAFIC POLICE/DPP waokoe jahazi kwa kutapeli raia kwa nguvu nguvu. Pamoja na KUZIUZA ZILE VX ZA KIJANI ZA KAMPENI & NDEGE zote.

KUMBUKIZI

1) Waajiriwa serikalini na walimu wanadai NYONGEZA YA MISHAHARA NA KUPANDISHWA MADARAJA KWA MIAKA 5 ILIOPITA NA INAYOKUJA.

2) Rais alisema hataki kuchanganyiwa wabunge wa upinzani, wanachelewesha maendeleo. Sasa taifa zima kuanzia Rais/Makamo/Waziri Mkuu/Mawaziri/Wabunge/Madiwani/Wenye Viti Wa Mitaa Na Vitongoji ni CCM. Tusubiri hayo maendeleo waliokua wakiyatolea MAHUBIRI NA MAWAIZA.

3) Tanzania ni DONA KANTRI, muda umefika wa kuanza kutoa na kuwapa misaada Ethiopia na Msumbiji.

Kauli pendwa ya mkuu "Wataishi Kama Mashetani". Sasa kwenye hii "MITANO TENA" meza imegeuka.
 
Sheria inayoitajwa kwenye Item#4 inasema hivyo kweli? Haiwezekani kuwa na close-ended provision ya aina hiyo wakati upo kabisa uwezekano wa kutokuwa na mbunge au wabunge wa kutosha kutoka kambi ya upinzani. Tuwekee hapa hiyo sheria.

Nadhani hiyo sheria itakuwa inaelekeza hivyo tu kama kuna wabunge wa kutosha kutoka kambi ya upinzani!
 
... kweli nimeamini sio kila msiba ulie, kuna misiba mingine ni ya kuchekesha hasa pale unapo jisababishia msiba wewe mwenyewe

Nakumbuka kile kisa cha Abuu Nuwasi kukata tawi la mti alilokalia

Msumari huu wa moto
 
Hata Elimu ya nchi hii imeharibiwa naCCM. Wanapenda namba ya ufaulu wa wanafunzi kuwa kubwa bila kujali ubora wa wanafunzi. Ndio wakaja na waalimu wa vodafasta,wakadahili wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wasio na uwezo ili mradi tu ionekane elimu ya juu inakua.Wamejenga shule lakini hazina waalimu,wamejenga Hospitali lakini ukienda hukuti daktari.Hao ndo CCM bana.
 
Back
Top Bottom