Kuna homeboy tulisoma naye zamani, lakini tukapoteana kwa miaka kadhaa baada ya chuo. Miaka mitatu ilikuwa imempita akiwa mtaani hana kazi, hana ramani, hana pa kuanzia.
Siku moja akanipigia simu. Aliomba aje mjini (Dar) aanze maisha upya. Hakuwa na pa kuishi, hakuwa na hata pa kupafikia. Nilipomuangalia, niliona jamaa yuko kwenye hali mbaya nilihisi lazima nichangie angalau kidogo kumtoa pale.
Kwa bahati, mazingira yangu yalikuwa yanaruhusu. Nikamkaribisha kwangu. Tuliishi vizuri, kama ndugu. Siku chache tu baadaye nikataftia kazi mshahara laki mbili. Alikuwa anaondoka saa 12 asubuhi anarudi saa tatu usiku, Jumapili alikuwa free, tunatoka kutembea kidogo kupata bata, kusahau stress za wiki.
Baada ya miezi mitatu nikapata connection nyingine ya kazi nzuri nikampigia simu nikamwambia, “Bro, kuna nafasi, andaa CV.” Nikamsaidia kurekebisha cv Lakini kiukweli, hiyo ilikuwa kuzuga tu. Njia iliyofanikisha ni bahasha na kumjua mtu wa kumpa.
Akapita !!
Kazini anaingia saa mbili asubuhi anatoka saa kumi na moja. Mhsahara ni laki 8, posho zipo ila sijui kiasi kamili.
Nilifurahi kwa niaba yake, ilikuwa hatua kubwa kutoka pale alipoanzia.
Lakini hapo ndipo kila kitu kilianza kubadilika.
Wiki moja tu baada ya mshahara wa kwanza, nikarudi home nikakuta kaondoka bila taarifa. Sikutakeka, nilidhani labda alihisi angenisumbua kunijulisha, au alihisi mimi ningemuambia asiondoke. Nikapotezea.
Lakini mambo yakaanza kubadilika zaidi. Nilikuwa najaribu kumfikia nikimpigia, hazipokelewi. Nikimtext, majibu yanakuja baada ya masaa. Nikimtembelea, ataweka mazingira niondoke (kuna mkutano, naenda mahali, dharura, n.k.).
Nilikaa chini nikajiuliza hivi, nilikuwa rafiki au nilikuwa njia ya kupitia?
Sikuomba chochote kwake nikidhani tutapata muda zaidi wa kuwa close.
Sasa tuko na miezi kadhaa hatujaonana wala kusocialize. Tumepeana “vipi mambo” mara chache tukiwa tunakutana sehemu random, kila mmoja akapita zake. Nikakubali labda hicho kilikuwa kipindi tu cha msaada, si cha urafiki wa kweli.
Na sasa, kuna boss mpya kazini kwao ameanza kupunguza watu ili alete wake. Jamaa kanipigia tena: Bro, huku kuna hali ngumu, naomba unisaidie nisitoke.
sielewi nifanye nini, i am onfused