Niliwa-MISS-je. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,808
59,317
Dah. . .kweli kijijini kutamu na kuchungu.

Niliwamiss, alafu nikawamiss, kabla sijakaa vizuri nikawamiss zaidi. Sema ndo hivyo tena kijijini mambo mengi kweli. . .yani hujakaa vizuri kuna kuokota kuni, umetua mzigo hata hujahema kuna ng'ombe analia, ile umetoka kumtupia majani unasikia purukushani kwenye banda la kuku, ukishampurukusha alotaka kitoweo cha bure parachichi hiloooo limeanguka, ile umeliweka chini kuna jirani anaita (alafu eti ukifika anasema "napita" tu), hujamaliza kusonya kwa usumbufu kuna alokuja kuchota maji anaomba umfungulie, ndoo haijajaa kheee kuna klasi meti kaja kusalimu, hujamkaribisha hata chai unakumbuka kuna maharage jikoni. . . yaaaani full mizunguko.

Nimefurahije kurudi mjini, kijijini sirudi tena mpaka siku ya Christmass. . . na siku ya tatu yake natimua.

Enheeeee we Bishanga njoo unieleze sababu sa wewe kutaka DNA ya kichanga changu? Baba yake ndo alokutuma ama?

Kongosho , Yummy naona nilimiss mambo mengi kweli(baada ya nyie). . .nikipata muda itabidi mnisaidie kufanya marudio.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom