Nilivyotapeliwa na kuingizwa mkenge na Giraffe Insurance ya pale Menonite Upanga

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Jul 2, 2019
910
1,394
Ilikuwa muda wa saa 10 usiku tarehe 14 mwezi wa 2 mwaka 2013 natokea Ubungo naelekea Mwenge ambapo nilipata ajali round about pale Mwenge Vinyago.......**
Nikiwa na gari aina Mark II Grande ya mwaka 2003 namba T 6**CFG ambayo niliagiza toka Japan kwa msaada wa jamaa mmoja ambaye ndo shughuli zake hizi. Huyu jamaa nilimkabidhi pesa yote pamoja na BIMA kubwa ambayo ilikuwa ni kama Laki 4 na kitu hivi. Na hii ilikuwa ni gari ya pili jamaa kuniagizia kwahiyo sikufuatilia sana taratibu kama nilikuwa zimekamilika kwa usahihi.

....**Siku hiyo nikiwa nakaribia Round About ya pale Vinyago ambapo tayari nilishakadiria speed ya kulala nayo ghafla jamaa wa bodaboda akatokea njia ya Stendi ya Mwenge akapita Round About kwa kasi na kufosi wrong way aje kuingia Mpakani. Kilichotokea pale hadi leo sijapata jawabu maana nilijikuta nimeshika Dashboard na kuona majani na michanga ikipishana kwenye kioo cha mbele, mwishowe gari ikakita kwenye kingo za Round about.. Nikafungua mkanda ambao mda huo ulikuwa umenibana kisawasawa.. Nilichokiona sikuamini baada ya kutoka kama nimetoka mzima maana gari ilikuwa nyang'a nyang'a.....

Dakika chache akatokea mwanajeshi ambaye nafkiri alitokea pale getini kwao. Alinipa msaada wa ulinzi maana kuna majamaa kama watatu ambao nilikuwa siwaelewi ndo walikuwa wa kwanza kufika. Baadaye akaja Askari na Break down gari ikachukuliwa. Hapo laki 2 ilinitoka kwa Askari kuhusu michoro na maelezo maana stori yangu hakuielewa.
Kesho yake nikapigiwa simu na Garage ya wachina Spring City nyuma ya Sheli Oilcom pale Sayansi. Nikakabidhiwa makaratasi yangu pale nipeleke kwa Ofisi ya BIMA yangu.. Hapo ndo mchezo ulipoanza..

Nikafika pale Ofisi kwa huyu wakala wa Bima pale kwenye Kanisa la Mennonite ambalo lipo mkabala na DIT. Jamaa jina lake ni BUMIJA MUZE. Nikamwonyesha picha za tukio na makaratasi yote. Akanipa uhakika kuwa suala langu litakuwa rahis maana niko na Bima kubwa. Nikaenda zangu kwa makubaliano ya kumsubiri jamaa kutoka Bima aje adhibitishe na mambo mengine. Kwahiyo nikawa namtafuta kwa simu tu maana shughuli zangu zilikuwa nje ya mkoa. Baada ya kama miezi mitatu bado akawa anasema ishu inafuatiliwa maana mafaili ni mengi yanayofanyiwa kazi. Nikaona hapana, nikamuuliza ghafla ofisini kwake ambapo akanipa stori ile ile ya nisubiri na akaniambia niandae kama Laki 5 ya kumhonga huyo mwenye atatoka huko Bima makao makuu. Nikamkatalia na tukaelewana labda laki 3.. Baada ya wiki akanambia mambo yako jamaa unakuja ila kakomaa na laki 5, tena akanipa na namba yake nimtafute.. Nikambembeleza yule Mzee lakini wapi akagoma na mikwara mingi akanipa. Sasa nikaangalia muda uliokwishapita na nauli nazopoteza kufuatilia nikasema sawa. Kweli yule Mzee tukakutana pale Garage akaangalia gari nikampa laki 5 tukanywa na chai kwenye mgahawa pale pembeni tukaondoka nilijua muda si mrefu ntalipwa pesa ntanunua gari lingine..
Ikapita miezi kama 6 kazi ikawa kumfuatilia yule Mzee na huyu wakala Wote wanasema nivumilie maana mambo ya kukupa Bima ni process ndefu.
Siku moja nilipokuwa nimerudi Dar kutoka huko nnapotangazia njaa zangu nikaona bora niende mwenyewe pale makao makuu ya BIMA YA IGT pale Kitega Uchumi Ghorofa ya 12. Majibu niliyopewa yalinivunja nguvu kabisa maana niliambiwa gari langu halipo kwenye listi yao.
Niliposhuka ikabidi nimpigie wakala. Acha kabisa jamaa ni fundi wa maneno, pale pale akanibadilishia gia angani kuwa kweli zile risiti zangu ni za IGT ila alighairi akazipeleka kwingine, wakati namhoji akakata simu. Nikakimbilia ofisini kwake nako nikakuta kadada kakanijibu kuwa jamaa kaondoka ghafla muda si mrefu..
Ikabidi niondoke. Baadae nikamtafute yule Mzee akawa hapokei simu yangu. Nilimpigia kwa namba nyingine akapokea ile nipoanza kuongelea ile ishu akakata simu.
Hapo nikaona nilaze mambo yangu nifuatilie ishu ya gari. Kesho yake nikadamka pale Ofisini kwa wakala ambapo sikumkuta ila nikakuta watu kama wawili tena wenye Hadith kama yangu. Tukiwa tunajadili akaja jamaa mwingine akafungua ile Ofisi, ikabidi tumhoji. Jamaa alikwambia kuwa huyo Ndugu Bumija Muze kwakifupi umekuwa tapeli na ana kesho nyingi za namna hiyo na wao wamemshamfukuza kwenye Ofisi yao kwahiyo hajui jinsi ya kumpata. Ila tukajua ni fiksi tu za kumlinda.
Baada ya pale nikawa namwinda huku nina RB ya pale Msimbazi.
Kule kwa mchina niliambiwa nadaiwa kama Milion 8 yaani matengezo na ulinzi wa miaka ikawa inakaribia miwili Sasa.

Ikabidi nimtafute mtu wa kumwinda. Kweli kuna siku jioni akaonekana, nikawahi nikachukua polisi tukampeleka Msimbazi. Kufika Msimbazi baada ya maelezo akakubali ni kweli alitafuna pesa yangu ila nimpe mwezi mmoja atakuwa keshalipia lile gari atalitoa. Polisi ananiuliza kama niendelee na kesi au nimvumilie. Sasa pale napo walikuwepo watu wawili tena na Mzee mmoja ambaye alisema yeye ni Mchungaji yuko Zanzibar akanisihi kuwa angesimamia hilo swala. Mimi na huruma zangu nikamkubalia tukaandikisha maelezo pale basi niakaenda zangu.
Mwezi ukapita nikaona kimya ikabidi nikamuulizie Si ndo nikakuta Ofisi yao iko na watu wengine tofauti tena hata shughuli yenyewe siyo za mambo Bima tena. Nikatafuta wenyeji pale ambao nao hata hawakunipa majibu kuwa wale jamaa wametokomea wapi. Nikiwa kwenye harakiri za kuwaza na kuwaza mara yule jamaa niliyewahi kumkuta pale Ofisi anaingia, nikakimbilia na kumuuliza kulikoni, jamaa alinambia MUZE alikimbia na hata alipo haijulikani maana ana kesi kibao za Utapeli na Madai.. Na yeye kafungua Ofisi yake pale pale pembeni..

Sasa niakaenda kwa mchina labda ni bargain naye, doh! Kwenda nikaambiwa sasa imeongezeka ni Milion 9 maana imewekwa injini mpya. Sasa nikapiga hesabu kwamba kununua Mark 2 Grande iliyokuwa barabarani kwa wakati ule isingezidi hata Miilioni 8.. Gari naiona nzima kabisa kila kitu ila tatizo Ndugu MUZE keshaniingiza MKENGE..
Muda huo wote mambo yangu kule mkoani nako yamesimama, ikabidi nirudi.
Niliendelea kumfuatilia mpaka nikachoka maana nilishindwa kuendelea kutokana na shughuli zangu za utafutaji..

Baadae nikaona isiwe taabu maisha yanaendelea na hela inatafutwa..

Kinachoniuma zaidi ni kuwa huyu MUZE alikuwa anajua kabisa kuwa gari yangu haina Bima walau angenieleza ukweli ningechangia hata nusu ya matengezo lakini yeye bado akaendelea kunitapeli na yule Mzee wake aliyedai katokea IGT.

Kwahiyo ni miaka 6 sasa Ndugu MUZE ( MLOKOLE ) uliyekuwa na OFISI YA GIRAFFE INSURANCE PALE MENNONITE UPANGA KARIBU na hospitali ya REGENCY yawezekana WEWE UNAENDELEA KULA RAHA NA FAMILIA YAKO ILA KUMBUKA KUWA hukunitendea HAKI na ulichonifanyia KIMENIGHARIMU sana...
 
Ilikuwa muda wa saa 10 usiku tarehe 14 mwezi wa 2 mwaka 2013 natokea Ubungo naelekea Mwenge ambapo nilipata ajali round about pale Mwenge Vinyago.......**
Nikiwa na gari aina Mark II Grande ya mwaka 2003 namba T 6**CFG ambayo niliagiza toka Japan kwa msaada wa jamaa mmoja ambaye ndo shughuli zake hizi. Huyu jamaa nilimkabidhi pesa yote pamoja na BIMA kubwa ambayo ilikuwa ni kama Laki 4 na kitu hivi. Na hii ilikuwa ni gari ya pili jamaa kuniagizia kwahiyo sikufuatilia sana taratibu kama nilikuwa zimekamilika kwa usahihi.

....**Siku hiyo nikiwa nakaribia Round About ya pale Vinyago ambapo tayari nilishakadiria speed ya kulala nayo ghafla jamaa wa bodaboda akatokea njia ya Stendi ya Mwenge akapita Round About kwa kasi na kufosi wrong way aje kuingia Mpakani. Kilichotokea pale hadi leo sijapata jawabu maana nilijikuta nimeshika Dashboard na kuona majani na michanga ikipishana kwenye kioo cha mbele, mwishowe gari ikakita kwenye kingo za Round about.. Nikafungua mkanda ambao mda huo ulikuwa umenibana kisawasawa.. Nilichokiona sikuamini baada ya kutoka kama nimetoka mzima maana gari ilikuwa nyang'a nyang'a.....
Endelea...
 
Ilikuwa muda wa saa 10 usiku tarehe 14 mwezi wa 2 mwaka 2013 natokea Ubungo naelekea Mwenge ambapo nilipata ajali round about pale Mwenge Vinyago.......**
Nikiwa na gari aina Mark II Grande ya mwaka 2003 namba T 6**CFG ambayo niliagiza toka Japan kwa msaada wa jamaa mmoja ambaye ndo shughuli zake hizi. Huyu jamaa nilimkabidhi pesa yote pamoja na BIMA kubwa ambayo ilikuwa ni kama Laki 4 na kitu hivi. Na hii ilikuwa ni gari ya pili jamaa kuniagizia kwahiyo sikufuatilia sana taratibu kama nilikuwa zimekamilika kwa usahihi.

....**Siku hiyo nikiwa nakaribia Round About ya pale Vinyago ambapo tayari nilishakadiria speed ya kulala nayo ghafla jamaa wa bodaboda akatokea njia ya Stendi ya Mwenge akapita Round About kwa kasi na kufosi wrong way aje kuingia Mpakani. Kilichotokea pale hadi leo sijapata jawabu maana nilijikuta nimeshika Dashboard na kuona majani na michanga ikipishana kwenye kioo cha mbele, mwishowe gari ikakita kwenye kingo za Round about.. Nikafungua mkanda ambao mda huo ulikuwa umenibana kisawasawa.. Nilichokiona sikuamini baada ya kutoka kama nimetoka mzima maana gari ilikuwa nyang'a nyang'a.....

Dakika chache akatokea mwanajeshi ambaye nafkiri alitokea pale getini kwao. Alinipa msaada wa ulinzi maana kuna majamaa kama watatu ambao nilikuwa siwaelewi ndo walikuwa wa kwanza kufika. Baadaye akaja Askari na Break down gari ikachukuliwa. Hapo laki 2 ilinitoka kwa Askari kuhusu michoro na maelezo maana stori yangu hakuielewa.
Kesho yake nikapigiwa simu na Garage ya wachina Spring City nyuma ya Sheli Oilcom pale Sayansi. Nikakabidhiwa makaratasi yangu pale nipeleke kwa Ofisi ya BIMA yangu.. Hapo ndo mchezo ulipoanza..
Watu wengine wanatutafutia kesi tcra.
Sasa ndio upuuzi gani huu.
Watu tumekuja tujifunze alafu jitu linatuacha soremba.
Hujawahi pigwa wewe.
 
Nikafika pale Ofisi kwa huyu wakala wa Bima pale kwenye Kanisa la Mennonite ambalo lipo mkabala na DIT. Jamaa jina lake ni MUZE. Nikamwonyesha picha za tukio na makaratasi yote. Akanipa uhakika kuwa suala langu litakuwa rahis maana niko na Bima kubwa. Nikaenda zangu kwa makubaliano ya kumsubiri jamaa kutoka Bima aje adhibitishe na mambo mengine. Kwahiyo nikawa namtafuta kwa simu tu maana shughuli zangu zilikuwa nje ya mkoa. Baada ya kama miezi mitatu bado akawa anasema ishu inafuatiliwa maana mafaili ni mengi yanayofanyiwa kazi. Nikaona hapana, nikamuuliza ghafla ofisini kwake ambapo akanipa stori ile ile ya nisubiri na akaniambia niandae kama Laki 5 ya kumhonga huyo mwenye atatoka huko Bima makao makuu. Nikamkatalia na tukaelewana labda laki 3.. Baada ya wiki akanambia mambo yako jamaa unakuja ila kakomaa na laki 5, tena akanipa na namba yake nimtafute.. Nikambembeleza yule Mzee lakini wapi akagoma na mikwara mingi akanipa. Sasa nikaangalia muda uliokwishapita na nauli nazopoteza kufuatilia nikasema sawa. Kweli yule Mzee tukakutana pale Garage akaangalia gari nikampa laki 5 tukanywa na chai kwenye mgahawa pale pembeni tukaondoka nilijua muda si mrefu ntalipwa pesa ntanunua gari lingine..
Ikapita miezi kama 6 kazi ikawa kumfuatilia yule Mzee na huyu wakala Wote wanasema nivumilie maana mambo ya kukupa Bima ni process ndefu.
Siku moja nilipokuwa nimerudi Dar kutoka huko nnapotangazia njaa zangu nikaona bora niende mwenyewe pale makao makuu ya BIMA YA
Msengye kala Premium Huyo, hajaipeleka kwenye kampuni. Hao ndo mawakala wanaodhalilisha Uwakala wa Bima.
 
Hicho kijamaa ni kipare kinakaa Kimara kinaitwa BUMIJA MUZE kina mke mwenye mavi mengi sana. Kina Corolla nyeusi. Kimeshawahi kunikatia BIMA kubwa feki. Siku niliyopata ajali kikaanza story za ngoja ngoja ngoja ngoja. Mpaka Leo namdai tsh 400,000. Very stupid kila apatikanapo apigwe mawe. Nadhani kimehama Kimara mwisho sasa kinakaa suka. Kiepuke kama ukimwi
 
Huyu afaa kupelekwa SHILAWADU kila mtu ajue ni mtu wa kuepukwa. Kila mwaka BUMIJA MUZE anabadili sehemu ya ibada. Alikua Kimara Korogwe kahamia Temboni halafu Mbezi Luis sasa hivi nako haonekani kwa madeni yanavyo muandama. Kila kanisa anakwenda kuna mtu amemtapeli. Nadhani hata kodi ikiisha anamtapeli mwenye nyumba baada ya miezi 5 anatokomea. Yaani yule ataingia 18 zangu au za mtu mwingine aliyemtapeli. Huu ukurasa msiufute
 
Back
Top Bottom