Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,512
Habari wakuu,
Sitasahau siku niliyofananishwa na mdada mmoja huko kijijini kwetu.
Ilikuwa hivi;
Huyo dada alikuwa ni rafiki yangu na mara nyingi nilipokuwa nikipita naye watu walikuwa wakisema kuwa nafanana naye. Sasa hali ile ya kufananishwa mimi nikawa naichukulia poa na urafiki ukawa unaendelea mimi na huyo rafiki yangu.
Siku moja nikiwa natembea njiani mwenyewe, akaja mtu mmoja na kuniambia kuwa wewe umekataa kunilipa deni langu. Nikamwambia utakuwa umenifananisha na huyo mtu maana mimi sikufahamu.Akanza kuwa mkali na kutaka hata kunipiga.
Akaendelea kulazimisha na akataja jina la mtu aliyemchukulia, akataja jina la huyo rafiki yangu, hapo ndio nikajua ni rafiki yangu. Nikamwambia mimi siitwi hilo jina unalosema mimi naitwa fulani, akaniambia sawa unakataa ila kesho nitakuja dukani kwako.
Basi akaniacha nikaenda zangu, niliogopa sana nikasema kama je ningepigwa kwa kosa amabalo sijawahi fanya! Ila nikashukuru Mungu. Usiku niliwaza sana juu ya kufananishwa na huyo mtu nikaona ili kuondoa mtafaruku niende kwa rafiki yangu dukani.
Kesho yake nikaenda kule dukani kwa yule rafiki yangu, kufika nikamweleza mkasa mzima, akasema ni yeye alimkopa huyo mtu. Basi nikakaa hapo nikisubiri huyo mtu anayetufananisha aje, alipofika alitahamaki akasema kweli duniani wawiliwawili. Ndipo nikapata nafuu ya moyo.
Je ushawahi kufananishwa na mtu? Ilikuwaje?