Nilivyotaka kupigwa kisa kufananishwa, ushawahi kufananishwa na mtu?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Habari wakuu,

Sitasahau siku niliyofananishwa na mdada mmoja huko kijijini kwetu.
Ilikuwa hivi;

Huyo dada alikuwa ni rafiki yangu na mara nyingi nilipokuwa nikipita naye watu walikuwa wakisema kuwa nafanana naye. Sasa hali ile ya kufananishwa mimi nikawa naichukulia poa na urafiki ukawa unaendelea mimi na huyo rafiki yangu.

Siku moja nikiwa natembea njiani mwenyewe, akaja mtu mmoja na kuniambia kuwa wewe umekataa kunilipa deni langu. Nikamwambia utakuwa umenifananisha na huyo mtu maana mimi sikufahamu.Akanza kuwa mkali na kutaka hata kunipiga.

Akaendelea kulazimisha na akataja jina la mtu aliyemchukulia, akataja jina la huyo rafiki yangu, hapo ndio nikajua ni rafiki yangu. Nikamwambia mimi siitwi hilo jina unalosema mimi naitwa fulani, akaniambia sawa unakataa ila kesho nitakuja dukani kwako.

Basi akaniacha nikaenda zangu, niliogopa sana nikasema kama je ningepigwa kwa kosa amabalo sijawahi fanya! Ila nikashukuru Mungu. Usiku niliwaza sana juu ya kufananishwa na huyo mtu nikaona ili kuondoa mtafaruku niende kwa rafiki yangu dukani.

Kesho yake nikaenda kule dukani kwa yule rafiki yangu, kufika nikamweleza mkasa mzima, akasema ni yeye alimkopa huyo mtu. Basi nikakaa hapo nikisubiri huyo mtu anayetufananisha aje, alipofika alitahamaki akasema kweli duniani wawiliwawili. Ndipo nikapata nafuu ya moyo.

Je ushawahi kufananishwa na mtu? Ilikuwaje?
 
Window7

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
3,916
2,000
Hiyo kitu imenitokea.. Kuna jamaa nafanana nae sana huko nyumbani, tulisoma shule tofauti ila tulikua tukikutana kwenye michezo. Watu walituita pacha. Juzi nmerudi nyumbani jamaa amekua mkwapuaji na mwizi mzuri. Basi nashangaa sehem nyingine nikipita nanyooshewa vidole... Hapa natafuta mbinu nifanye nini nisifanane nae. Nimeudhika sana.
 
Pole jamani...yani sina hamu na kufananishwa nikikumbuka ule msala wangu
 
MarkHilary

JF-Expert Member
Feb 8, 2015
1,516
2,000
Nikiwa chuo kikuu kulikua na dada alikua mtani wangu sana. Kuna kozi moja tulisoma mwaka wa kwanza tukawa kundi moja, kuanzia hapo ukazuka urafiki na utani baina yetu

Sasa siku moja nikiwa katikati ya jiji nikamuona akichat kwa simu yake.. Basi nikamvamia mithili ya kibaka kutaka kumpora simu

Kumbe bwana hakuwa yule dada nilimfananisha! Mdada akapiga yowe la mwizi, wananzengo wakaniweka kati. Nilijieleza siku ile mate yote yakaniisha mdomoni... Kilichonisaidia, nilikua na wanachuo wenzangu wakanitetea sana, halafu kati ya wananzengo alikuwepo mzee mmoja mwenye busara kweli kweli

Mpaka leo nikikumbuka hilo tukio nakemea pepo kwa jina la Yesu!
 
luhuye

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
289
250
Hiyo kitu imenitokea.. Kuna jamaa nafanana nae sana huko nyumbani, tulisoma shule tofauti ila tulikua tukikutana kwenye michezo. Watu walituita pacha. Juzi nmerudi nyumbani jamaa amekua mkwapuaji na mwizi mzuri. Basi nashangaa sehem nyingine nikipita nanyooshewa vidole... Hapa natafuta mbinu nifanye nini nisifanane nae. Nimeudhika sana.
Moto unakuhusu mkuu
 
kibhopile

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
1,510
2,000
Pole sana, mi nishaingia bar siku moja nikatulia kuna jamaa alikuwa pembeni akaja akanimbia amenitafuta sana sipatikani kwenye simu, akaniomba msamaha kwanini kachelewesha kulipa deni akatoa laki 2 akanipa afu akaninulia Na Heineken 3 (huwa sinywi Heineken) though) afu akasepa. Muda wote Nilikuwa nahisi kama nacheki muvie. Ila ndo hivo god answers your prayers in a mysterious way.
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,340
2,000
Baada ya kumaliza form six nilikua napiga tempo shule moja hivi,sasa wakati wa break akaja jamaa tulokua tunafundisha nae akaniuliza 'ulimuona yule mshkaj nilokua naongea nae pale?' Nikamwambia niliona tu unaongea namtu sikutiilia maanan. Basi jamaa akanambia 'yule mshkaj ameshangaa kukuona hapa maana walikuaga wanakutafuta siku nyingi sababu ulimchomaga kisu mdogo wao afu ukatoroka'.
Nikamuuliza unasema?????

Hakuna siku nilipata kizunguzungu cha ghafla kama siku hiyo. Bahati nzuri jamaa yangu alicheka sana baada ya kuambiwa hivyo huku akimwambia huyo mshkaj kanifananisha maana huo mkoa kwanza mi ni mgeni hapo ndo lishkaji likatulia maana lilikua limeapa lazima linilipizie, ila bado nilikosaga amani kabisa.
 
kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,749
2,000
Nikiwa chuo kikuu kulikua na dada alikua mtani wangu sana. Kuna kozi moja tulisoma mwaka wa kwanza tukawa kundi moja, kuanzia hapo ukazuka urafiki na utani baina yetu

Sasa siku moja nikiwa katikati ya jiji nikamuona akichat kwa simu yake.. Basi nikamvamia mithili ya kibaka kutaka kumpora simu

Kumbe bwana hakuwa yule dada nilimfananisha! Mdada akapiga yowe la mwizi, wananzengo wakaniweka kati. Nilijieleza siku ile mate yote yakaniisha mdomoni... Kilichonisaidia, nilikua na wanachuo wenzangu wakanitetea sana, halafu kati ya wananzengo alikuwepo mzee mmoja mwenye busara kweli kweli

Mpaka leo nikikumbuka hilo tukio nakemea pepo kwa jina la Yesu!
Nimejaribu kupata taswira ya hali uliyokuwa nayo naamini kijasho chembamba kilikutoka.
 
John locke

JF-Expert Member
May 6, 2012
801
1,000
Kuna binamu yangu tunafanana nae sana. Sijawahi kuonana nae hata siku moja. Ila naambiwa nmefanana nae. Mara ya kwanza nilikataa kuwa haiwezikani. Sasa mwaka 2013 nilikuwa likizo Moshi kwa babu yangu, basi jumapili moja nmetoka kanisani nipo na mjomba wangu nikawaona wabibi wawili(siwafahamu) wananiangalia kama vile wananifananisha. Nikawasalimu wakaitikia wakaniuliza, wewe ni Tony nikawajibu hapana, mi ni John. Walikataa kata kata wakasema nawadanganya. Basi baada ya hapo tukaondoka na mjomba huku nikiwa siamini kilichotokea. Ila siku hizi nmeshazoea kufananishwa huku.
 
urumrawi

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,492
2,000
Aisee....gentleman hawezi kunyamaza akiona binti anakuwa bullied.
Kwani kumjali mtu ni bullying (jamaa kamjali kwa kusituka kuwa anapoteza muda mwingi katika kulete sredi hapa JF wakati wenzake wanawajibika)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom