Nilivyoshindwa kizembe kusoma udaktari

Nilivyoshindwa kizembe kusoma udaktari

Joined
Dec 18, 2019
Posts
73
Reaction score
135
Leo nimekumbuka mbali kidogo wakuu

miaka kadhaa nyuma nilifaulu masomo yangu ya kidato cha sita na kwenda kusomea udaktari hapa jiji la karaha

Nikiwa chuo mambo hayakuwa mabaya sana kwa mwaka wa kwanza yaani kwa vijana wanasema ilikuwa dezo. Mambo yalikuwa magumu nilipoingia mwaka wa pili.

Iko hivi tukiwa mwaka wa pili mimi na wenzangu kama mia moja na ishirini hivi katika course yetu ya medical alikuja professor mmoja nakumbuka jina lake prof mayombi.

prof alikuja ili atufundishe course ya anatomy. Tukiwa laboratory mbele professor ameweka mwili (maiti) ya mtu kwa ajili ya kufanya dissection lakini kabla hajafanya chochote alituasa kuwa daktari mzuri ni yule ambaye anazingatia mambo mawili jambo la kwanza haoni kinyaa!

Basi bwana proffesor akasema tufate kile anachofanya. Lakini katika hali isiyo ya kawaida proffesor aliingiza kidole kwenye puru la maiti na kuingiza mdomoni kwake, Kama vile haitoshi akatutaka tufanye vilevile kheeee!

Kwa nini nifeli mtoto wa kiume nikajikaza kisabuni nikampiga doko maiti nikazamisha kidole chote mdomoni na wenzangu pia hivyohivyo.

baada ya hili zoezi proffesor akasimama tena mbele akasema hilo lilikuwa jambo la kwanza jambo la pili daktari mzuri ni yule ambaye ni muangalifu mfano mimi nilitumia kidole cha kati kuingiza kwenye puru la maiti hii lakini niliingiza mdomoni kidole cha kwanza.

kikakumbuka kidole nilichotumia ni kimoja kwenye mambo yote niliishiwa nguvu nilizimia wiki mbili.

-kwa sasa mkulima wa vanilla.
 
kwa sasa ndo wewe unaesumbua kwa matangazo ya kuuza mkongo kule instagram
 
Back
Top Bottom