Nilivyopata faida ya 800k kwa Biashara ya Kondoo

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
399
279
Salamu Wakuu wa Jukwaa.

Mimi ni moja ya wafanyakazi katika Taasisi wilaya Ya Ngorongoro Mkoani Arusha, mahala nilipo ajiriwa ni karibu sana na Kenya almost kilomita 20 kuingia nchi Jirani. Huku kabila kubwa ni Wamasai.

Mwaka jana mwezi wa 8 Nilipata wazo la kuanzisha biashara hii hasa kutokana na wilaya hii kujaliwa kuwa na mifugo wengi pamoja na eneo kubwa la malisho kwa Ng'ombe pamoja na Kondoo.

Nikatafuta mchungi mmoja ambaye alikuwa rafiki yangu kwa muda mrefu ambaye alinielekeza namna biashara inavyoenda pamoja na soko lake lilivyo katika miezi huska. Alinishauri mengi pamoja na kuniambia gharama za uchungi pamoja na dawa za kunenepesha. Alinifahamisha nikiwa tayari atachunga pamoja na Kondoo na Ng'ombe wake kwa Pamoja.

Nilipata ushauri mwingi lakini kwa kuwa nilikuwa na mtaji kidogo alinishauri nifuge Kondoo badala ya kununua ndama.

Tulienda mnadani Wote pamoja na mchungi kutokana na kufahamika maeneo yale pamoja na lugha ya eneo huska ambapo tulinunua Kondoo 23. Ilikuwa ni mwisho wa mwezi wa 8, 2021 na Kupanga kuja kuwauza Mwezi wa 4, 2022.

GHARAMA ZA UNUNUZI WA KONDOO PAMOJA NA MENGINEYO

Nilinunua Kondoo 20 kwa gharama ya 70,000/= kila mmoja.

23 x 70,000/= Jumla 1,610,000/=

Gharama za usafirishaji wa Kondoo kipindi cha ununuzi, Kondoo mmoja 2,000/=

23 x 2,000/= Jumla 46,000/=

Gharama za Uchungi kwa mwezi ni 20,000/= ambapo Jumla ni miezi 9

9 x 20,000/= Jumla 180,000/=

Gharama za dawa ya kunenepesha Kondoo kwa miezi 8 kila mwezi nilitumia 25,000/=

8 x 25,000/= Jumla 200,000/=

Gharama za kusafirisha kwenda kuuza, Kila Kondoo 3,000/= ambapo tuliwauza nje ya nchi jirani Kenya.

23 x 3,000/= Jumla 69,000/=

FEDHA niliyopata baada ya Kuuza Kondoo, Jumla kuu ni 2,905,000/=

FAIDA NILIYOPATA BAADA YA GHARAMA ZILIZOKUWEPO

(Faida 2,905,000/=) - (Gharama 1,610,000/= + 46,000/= + 69,000/= + 200,000/= + 180,000/=)

(Faida 2,905,000/=) - (Gharama 2,105,000/=)

FAIDA KUU = 800,000/=

CHANGAMOTO

1. Soko la bei ya kondoo kushuka ndani ya muda na kusababisha Faida ndogo sana.

2. Kuwepo na changamoto ya wanyama wakali kama Fisi na Chui ambao husababisha kufa kwa mifugo.

3. Mifugo/Kondoo kuugua hasa kipindi cha mvua na kusababisha hasara.

4. Mifugo/Kondoo kukosa malisho stahiki hasa kipindi cha ukame kuanzia mwez wa 8 hadi wa 11 na kupelekea kufa. Hasa Ng'ombe ndo hufa kipindi hiki kwa kukosa Majani.

5. Kubadilishiwa mifugo na mchungi hasa usipokuwa makini kwa kuto kuwatembelea mara kwa mara.

6. Malisho kutokana na kukosekana kwa maeneo ya kulishia kwa sasa hasa baada ya maeneo mengi kuchukuliwa na Serikali na kuwa PORI TENGEFU.

7. Kondoo wanahitaji matunzo mengi (gharama) sana tofauti na Mbuzi pamoja na Ng'ombe.

USHAURI

1. Biashara ya kunenepesha ina Faida kubwa sana hasa ukiwa mkazi wa eneo lenye malisho ya kutosha na ukiwa unawapatia dawa. Kondoo wengi zaidi ndo Faida kubwa zaidi.

2. Ufugaji ni kama kuwekeza benki maana ukipata shida tu unaweza kuuza Kondoo/mifugo baadhi na kutatua tatizo huska.

3. Kupitia ufugaji unaweza kupata maziwa, nyama, ngozi pamoja na mengineyo mengi.

Asanteni. Wekeza!
 
Vipi kama ukiamua kununua na kwenda kuuza? Yaani tofauti na kusubiri miezi yote hiyo ndio uuze, namanisha nanunua leo kisha nafanya harakati za kwenda kuuza ndani ya siku mbili.
 
Vp kama ukiamua kununua na kwenda kuuza? Yaani tofauti na kusubiri miezi yote hiyo ndio uuze, namanisha nanunua leo kisha nafanya harakati za kwenda kuuza ndani ya siku mbili.
Hiyo inawezekana kabisa mkuu, kutoka soko moja kwenda jingine. Watu wenye mtaji mkubwa ndo huwa wanafanya biashara hii ya kununua Tanzania na kwenda kuuza masoko ya Jirani nchini Kenya ambapo Kuna uhitaji mkubwa zaidi.
 
Hongera mkuu…

Mchanganuo wako unapaswa kuwa hv:-
Sales (mauzo ya Komodo)
  • purchases (ununuzi wa Komodo)
  • Closing (Kama kuna kondoo hukumuuza)

= Utapata: Gross profit (Faida ghafi)

Afu:- utatolea hzo gharama zengne za kuendeshea hyo biashara (Operating cost)

=baada ya apo utakachopata ni faida kamili (net profit)
 
Hakuna biashara hapo,faida wastani laki moja kwa mwezi na biashara imejaa risk na changamoto lukuki
Faida ipo: 100,000 kwake ni kubwa ukizingatia ana kazi nyingine inayomuingizia kipato.Pili kajifunza jinsi ya kufanya biashara, kwahiyo hapo ana uzoefu mdogo wakati mwingine ataanza na mtaji mkubwa na kupata faida kubwa.
Tatu katoa elimu kuhusu ufugaji wa kondoo, mfano mimi sikuwa ninafahamu mbuzi ni rahisi kufuga kuliko kondoo.
Nne katoa hamasa kwa vijana wafuge au wafanye biashara ya kondoo.Hizo zote ni faida tusiangalie tu fedha zinazoingia.
 
Kwenye biashara kikubwa tunachoangalia ni faida vs risk.
Kama risk ni nyingi na faida ni kidogo ni rais sana kufirisika.kondoo na bata ni mifugo yenye risk sana ndio maana sio wengi
 
Mi nakusifu kwa kuwa pamoja na hiyo faida uliyoipata,

Umechangia pia kupata fedha za kigeni maana ni exporter wewe, hata kama labda ni 0. xx ni pato la taifa hilo ✌🤭
 
Salamu Wakuu wa Jukwaa.

Mimi ni moja ya wafanyakazi katika Taasisi wilaya Ya Ngorongoro Mkoani Arusha, mahala nilipo ajiriwa ni karibu sana na Kenya almost kilomita 20 kuingia nchi Jirani. Huku kabila kubwa ni Wamasai.

Mwaka jana mwezi wa 8 Nilipata wazo la kuanzisha biashara hii hasa kutokana na wilaya hii kujaliwa kuwa na mifugo wengi pamoja na eneo kubwa la malisho kwa Ng'ombe pamoja na Kondoo.

Nikatafuta mchungi mmoja ambaye alikuwa rafiki yangu kwa muda mrefu ambaye alinielekeza namna biashara inavyoenda pamoja na soko lake lilivyo katika miezi huska. Alinishauri mengi pamoja na kuniambia gharama za uchungi pamoja na dawa za kunenepesha. Alinifahamisha nikiwa tayari atachunga pamoja na Kondoo na Ng'ombe wake kwa Pamoja.

Nilipata ushauri mwingi lakini kwa kuwa nilikuwa na mtaji kidogo alinishauri nifuge Kondoo badala ya kununua ndama.

Tulienda mnadani Wote pamoja na mchungi kutokana na kufahamika maeneo yale pamoja na lugha ya eneo huska ambapo tulinunua Kondoo 23. Ilikuwa ni mwisho wa mwezi wa 8, 2021 na Kupanga kuja kuwauza Mwezi wa 4, 2022.

GHARAMA ZA UNUNUZI WA KONDOO PAMOJA NA MENGINEYO

Nilinunua Kondoo 20 kwa gharama ya 70,000/= kila mmoja.

23 x 70,000/= Jumla 1,610,000/=

Gharama za usafirishaji wa Kondoo kipindi cha ununuzi, Kondoo mmoja 2,000/=

23 x 2,000/= Jumla 46,000/=

Gharama za Uchungi kwa mwezi ni 20,000/= ambapo Jumla ni miezi 9

9 x 20,000/= Jumla 180,000/=

Gharama za dawa ya kunenepesha Kondoo kwa miezi 8 kila mwezi nilitumia 25,000/=

8 x 25,000/= Jumla 200,000/=

Gharama za kusafirisha kwenda kuuza, Kila Kondoo 3,000/= ambapo tuliwauza nje ya nchi jirani Kenya.

23 x 3,000/= Jumla 69,000/=

FEDHA niliyopata baada ya Kuuza Kondoo, Jumla kuu ni 2,905,000/=

FAIDA NILIYOPATA BAADA YA GHARAMA ZILIZOKUWEPO

(Faida 2,905,000/=) - (Gharama 1,610,000/= + 46,000/= + 69,000/= + 200,000/= + 180,000/=)

(Faida 2,905,000/=) - (Gharama 2,105,000/=)

FAIDA KUU = 800,000/=

CHANGAMOTO

1. Soko la bei ya kondoo kushuka ndani ya muda na kusababisha Faida ndogo sana.

2. Kuwepo na changamoto ya wanyama wakali kama Fisi na Chui ambao husababisha kufa kwa mifugo.

3. Mifugo/Kondoo kuugua hasa kipindi cha mvua na kusababisha hasara.

4. Mifugo/Kondoo kukosa malisho stahiki hasa kipindi cha ukame kuanzia mwez wa 8 hadi wa 11 na kupelekea kufa. Hasa Ng'ombe ndo hufa kipindi hiki kwa kukosa Majani.

5. Kubadilishiwa mifugo na mchungi hasa usipokuwa makini kwa kuto kuwatembelea mara kwa mara.

6. Malisho kutokana na kukosekana kwa maeneo ya kulishia kwa sasa hasa baada ya maeneo mengi kuchukuliwa na Serikali na kuwa PORI TENGEFU.

7. Kondoo wanahitaji matunzo mengi (gharama) sana tofauti na Mbuzi pamoja na Ng'ombe.

USHAURI

1. Biashara ya kunenepesha ina Faida kubwa sana hasa ukiwa mkazi wa eneo lenye malisho ya kutosha na ukiwa unawapatia dawa. Kondoo wengi zaidi ndo Faida kubwa zaidi.

2. Ufugaji ni kama kuwekeza benki maana ukipata shida tu unaweza kuuza Kondoo/mifugo baadhi na kutatua tatizo huska.

3. Kupitia ufugaji unaweza kupata maziwa, nyama, ngozi pamoja na mengineyo mengi.

Asanteni. Wekeza!
Dawa ya kunenepesha inaitwaje ..je inafaa kwa mbuzi na ng'ombe?
 
Hongera mkuu…

Mchanganuo wako unapaswa kuwa hv:-
Sales (mauzo ya Komodo)
  • purchases (ununuzi wa Komodo)
  • Closing (Kama kuna kondoo hukumuuza)

= Utapata: Gross profit (Faida ghafi)

Afu:- utatolea hzo gharama zengne za kuendeshea hyo biashara (Operating cost)

=baada ya apo utakachopata ni faida kamili (net profit)
Wasomi uchwara mmeanza tena mambo Yenu.
 
Back
Top Bottom