Nilivyoparamia mtumbwi wa vibwengo!

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,223
56,876
Si mmekuwa mkisikia kuhusu mtumbwi wa vibwengo? Tupo tuliouparamia na ukatushinda almanusra nafsi, roho, uhai ututoke!

Ilikuwa ni pisi fulani hivi tamtam ambayo nilidumu nayo kwenye dimwi la mapenzi kwa takribani miezi 6 hivi, mtoto alikuwa ni zile pisi za kwenda, pisi ambayo utaombea mkopo utaondolewa na riba na ukichelewa kulipa basi unasamehewa.

Have you ever believe in karma? On my side yes I was but not now!

Matatizo yalipoanzia
Siku isiyokuwa na jina mtoto akaamua kuniacha! Bora angeniacha kwa kuniambia ni ile niliachwa bila taarifa! usiombe kuachwa namna hii ni kama umebanwa pumzi na unata kupumua au kupiga mwayo.

Kunionyesha kuwa yeye ni mshenzi wa tabia aliamua tu kukaa kimya, halafu upande wangu ndio nilikuwa nimefika ile stage ya kupenda kufa ama nilietopea kwenye dimbwi la mahaba nakujaza vibaba. Nilikuwa ni yule kiberenge ambae siambiliki sishikiki, penzi mshindo!

Ukipiga hapokei, sms hajibu, mtaani huoni mtu! Baada ya wiki sio tu simu kuita ni kwamba haiiti kabisa, sms hazifiki, nikawa mnyonge ambae ukiniangalia tu ungejua mimi ndo yule mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Sura ikanishuka ikawa mpaka najionea aibu kujitazama kwenye kioo.

wiki ya pili hii hapa nikaona haitoshi tafuta mtu katika njia zi kihayawani haonekani,ana kwa ana napo haonekani. Ule wembamba unene niliokuwanao ukaanza kukonda, hata kujipa moyo kukaniisha.

Wiki ya tatu from no where wale waliosema milima haikutani lakini binadamu hukutana hawakukosea. Nikamuona mahali kakaa mnyamwezi kwa pupa za mahaba yakuteswa nikamkaribia hakuna cha salamu nikaanza kubwatuka "wewe ndio wakunifanyia mimi hivi?"

Nilibwatuka wee baada mtoto akaamua apigilie msumari kwa kusema hanitaki, kwamba mimi nayeye tufanye yameisha. Hiyo sentensi kwangu ilikuwa kama pigo la Ak 47 ambayo ilinipeperusha kama samaki alietolewa kwenye maji nakutupwa jangwani. Niliganda nikimtizama akiondoka kama kuku aliefauru kumtoroka mchinjaji.

Masikusiku yakapita nikajizoeza nakusema yatapita, lakini huku ndani moyo hautulii, wafurukuta kama pishi la makande. Ukilala hivi hapalaliki, ukila hapaliki unaona ugali kama unakucheka halafu huohuo ugali unagonga mkono na mboga kukucheka zaidi ya kwamba "Umeyakanyaga!"

Huu ndio ule muda ambao nilikuwa nikiamini kuhusu "karma" Kwamba kwa hichi alichonitendea lipo jambo litamkuta! Nae kitamfika na kitaumana kama mimi! Mwezi ukakata na mwezi mwengine ukakata.

Kwake ushindi huku kwangu moyo uliokuwa wa binadamu umebadirika umekuwa wa peremende.
Ile niliyokuwa naisubiria ya kuiita karma nikaona inachelewa. Ndipo Sasa nikaamu Mimi niwe karma yake nisimcheleweshee.

Ilikuwa ni siku ambayo siikumbuki jina, siku ambayo yule mwenye moyo wa peremende na mwenye anguko la mahaba akaamua akaanzie bar kabla ya kwenda kuitekeleza karma yake. Kilichokuwa mbele yangu ilimradi kilisoma kina alcohol basi nilikimiminisha kwenye koo langu, ilifika hatua mpaka wahudumu walianza kunitaza kwa jicho la "Bwana tuepushe na kikombe hichi!"

Nilipoona tosha yangu nikaona Sasa ndio ule muda wa fimbo kwenda kuua nyoka, ama kwenda kudhihirisha ule usemi wa "Usiempenda kaja". Kijua fulani hivi cha saa saba kikinikung'uta huku njia yote yangu nikiimba ule wimbo juma nature inaniuma sana.

Wakati huo najua yule jeraha wangu wa moyo alikuwa katika moja ya saluni yakike akijipendezesha nami nikaona huo ndio ulikuwa uwanja wangu pekee wa Mimi kwenda kuonyesha manjanjali yangu.

Dakika kumi si nyingi nikafika huku nayumbayumba hapo nautizama ule mlango wa saluni aliyopo nikaanza kuita jina lake kwanguvu. Nikaita kama mara tatu wakakaa kimya wadada wote waliokuwemo humo hata waliokuwa pembezoni nao wakakaa kimya kama vile wakisuburi mtumbuizaji nianzie kutumbuiza.

Bila haina na hisana nikaanza kuporomosha matusi mazito huku nikitaja jina lake!,watu wakaanza kuvutiwa na tamasha langu. Wakaanza kuzunguka Lile eneo nilipoona kumbe wamependa nikavua na shati hapo nikabaki ni pensi huku kijasho fulani cha ulevi kikinitoka.

Miporomoko yamatusi haikukatika mdomoni mwangu kiasi kwamba yule mdada akashindwa kuhimili akaanza kulia mule saluni wenzake wakaanza kumpoza. Wasamalia wema wakaanza kunionya lakini mtukanaji mimi niliechafukwa Kila alienionya nae sikumkalie pembeni, nilimvagaa kwa matusi mpaka walikiona kidaka tonge changu kilivyokuwa kimehamaki.

Lahaula kumbe kuna kitu nilikuwa sikijui na waswahili walisema jambo usilolijua ni sawa na usiku wa Giza nami giza lilikuwa limenitanda Sasa likatanduka. Nilichokuwa sikijui ni kuwa mrembo huyo nimtukanae alikuwa ameshaingia kwenye mahusiano mapya. Hilo la kwanza ambalo lilikuwa sio tishio kwa muda huo.

La pili ambalo ndio lilikuwa tishio la maisha yangu nikuwa huyo mpenzi wake alikuwa njiani kuja kwenye hii saluni aliyokuwepo ambayo mlevi mimi nilimtangulia. From no where ghafla msanii Mimi nilipata msanii mwengine jukwaani ambae alikuja kwa style ya aina yake.

Teke moja la kiuno lilitosha niyasahau matusi yote niliyokuwa nikiyatukana nakufanya niyakumbuke majina ya mama yangu ambayo niliyataja pasipokutaraji. Nikiwa kifua wazi nililamba vumbi nakuwa kama kituko mbele za watu.

Attention ya watu iliongezeka, wenye kucheka wakacheka na wenye kuona huruma wakaona. Nikiwa chini nikaona mtesi wangu akinijia mkukumkuku, nilipotaka kunyanyuka pakashindikana mara huyu hapa nikala pigo la pili banzi zito lamgongo ambalo lilitoka kwasauti kali, nikajihisi sasa nimekuwa Ile ngoma ya sindimba.

Haya ikanishika, mishipa ya damu ikanisimama kabla sikapumua uzuri, likashuka banzi jengine zurizuri ambalo lilitosha kuniambia "Amka ujitetee utakufa kiboya".

Kwa ujasiri wa pombe nikaamka kama mzimu hata waliokuwa wanataka kuamulia wakaona ngoja kwanza tuone, lakini ni heri wangekuja tu kuamulia maana sekunde hiyohiyo niliyosimama ndio sekunde hiyohiyo niliyorudishwa chini kwa mtama wa matamanio yakutaka kutoa uhai wangu.

Huo ndio wakati ambapo zile hesabu na mojamoja zikageuka mbilimbili na ndio wakati huohuo nikaanza kuona nyotanyota. Nilitamani kuangua kilio lakini hakikutoka. Nikabebwa mzegamzega nikarambwa kichwa cha pua! Nikatoa ukelele ambao ulionyesha kidaka tonge changu kile ambacho kilikuwa kikitoa matusi sasa kiliomba Msaada!

Upuuzi wa watizamaji hawa badala wasaidie wenyewe ndo wanasema "Waache wafundishane adabu" jambo ambalo niliona ni uongo maana Mimi pekee ndio niliyokuwa nikifundishwa adabu.

Jamaa likaja tena huku limefura nikaona hapa nitaacho roho yangu bure! Kabla hajanifikia nikajikwatua kwanguvu asalaleeeee, njemba ikanikwepa, alivyonikwepa nikataka kama kusimama ili nimgeuki ndio hapohapo akili ikaniambia acha upimbi hii spidi uliyoianzisha ndio itakayokuokoa!

Nikaona sasa huu ndio ule muda wakuyaokoa maisha yangu, sikusimama kwa tafsiri nyengine gari haikuzima nilijitungua mbio na ileile spidi niliyokuwanayo ili tu nitoke mikononi kwa huyu nunda! Huku nyuma niliacha kituko cha haja!

Damu puani,v umbi usoni na mwili mzima ndivyo nilivyoambulia! Ile karma niliyoipeleka ndio ikawa imenigeukia na mtumbwi niliodandia niliamua nijitose kabla vibwengo hawakuamua yakwao.😅
 
Damu puani,v umbi usoni na mwili mzima ndivyo nilivyoambulia! Ile karma niliyoipeleka ndio ikawa imenigeukia na mtumbwi niliodandia niliamua nijitose kabla vibwengo hawakuamua yakwao.
Haya maelezo yote umeyatoa kichwani...?
 
Back
Top Bottom