Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,013
- 1,635
Kwanza nikiri kwamba Mungu Yuko pamoja na Mimi kwa kuniuepusha na majanga haya Kwa mara ya pili kwa mwaka huu
Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo matapeli wa mitandaoni wanakuja kwa kasi kwani jeshi la polisi mkoa wa Tanga lilikamata vijana zaidi ya sita wanaishi kwenye nyumba na kodi wanalipa Tsh 800000 kwa mwezi kazi yao kubwa ni utapeli wa mitandaoni
Stori inaanza kama ifuatavyo
Ofisini huwa anakaa wife kutokana na Ratiba zangu za kilimo kuwa ngumu
Sasa siku moja alikuja mteja wa kiume na kujitambulisha kwa majina na kusema wao wamehamia mkoa wa Tanga kikazi.
Alitoa hela kama kawaida na kumuachia wife hela ya soda TSH 10000 na kuondoka.
Siku nyingine akaja na mtoto akatoa hela tena na kama kawaida akamuachia wife hela ya soda na kumtambulisha kwamba yule ni mtoto wake siku akiwa mbali atamtumia pesa na kumtuma huyo mtoto aje achukue na kweli alifanya hivyo kama mara mbili na kama kawaida alikua anamuagizia huyo mtoto aache hela ya soda.
Siku nyingine akaja na mwanamke na kujitambulisha ni mke wake alitoa hela kama kawaida akamuachia wife hela ya soda na akaacha maagizo kwamba siku akiwa mbali atatuma hela na atakuja kuchukua huyo mwanamke na kweli alifanya hivyo mara mbili na alikua anamuagizia huyo mwanamke amuachie wife hela ya soda hapo uaminifu kwa wife ukazidi maana alijua kwamba kumbe mpaka mke wake anaridhia kutoa hela ya soda basi hakuna tatizo usalama upo
SIKU YA TUKIO
Nikiri kwamba huwa nampa wife kila mbinu ya utapeli ninayoijua lakini hii nilikua siijui na sija muelekeza
Siku moja alikuja yule mteja na ki begi chenye fedha na kumwambia wife kwamba amuhifadhie Kuna sehemu anaenda ila hakuamini sana hivyo jioni atakuja kuzichukua zile pesa kwa uzoefu wa wife alisema ukiziangalia Kwa haraka haraka ni kama million tano, wife akazichukua zile pesa na kuzihifadhi pembeni.
Baada ya muda yule jamaa alipiga simu kwa wife na kumwambia huko aliko amepata changamoto amtumie million Tatu pesa si anazo akirudi atakata hela yake na kumkabidhi iliyobaki kweli wife alikua ana upungufu wa flot akaomba kwa wakala mwenzake na kupewa ila kabla hajatuma machale yakamcheza akakumbuka kwamba wakala unatakiwa kuhakiki pesa kabla ya kutuma.
Aisee wale wate ni mafundi chief Godlove anasingiziwa yaani vipande vya boksi vimepangwa kwa ustadi mkubwa na kuwekewa kiasi cha pesa kidogo juu ambazo baada ya kuzihesabu ni kama laki tatu.
Aisee Mawakala usije ukamuamini mtu yoyote kila mteja muone kama tapeli