Nilivyonusurika kutapeliwa Mawakala kuweni makini

Nilivyonusurika kutapeliwa Mawakala kuweni makini

Mdigo gani hustuki ?
Kila siku wife aachiwa elfu kumi ya soda, huyo jamaa kawaona nyie maskini au kawazidi umri Sana? Iweje mkeo apokee hela ya soda toka kwa mtoto mdogo au mwanamke mwenzie.
Kikwete alisemaje kuhusu kula vya watu?
 
ila pia mzuie mkeo asipende kupokea za soda, mazoea ya namna hiyo hayafai hasa kwa mke wa mtu.
 
Kwahiyo mkeo akawa anachekelea tu ya soda,na wewe ukaambiwa bado ukakenua meno?
 
Kwanza nikiri kwamba Mungu Yuko pamoja na Mimi kwa kuniuepusha na majanga haya Kwa mara ya pili kwa mwaka huu

Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo matapeli wa mitandaoni wanakuja kwa kasi kwani jeshi la polisi mkoa wa Tanga lilikamata vijana zaidi ya sita wanaishi kwenye nyumba na kodi wanalipa Tsh 800000 kwa mwezi kazi yao kubwa ni utapeli wa mitandaoni

Stori inaanza kama ifuatavyo

Ofisini huwa anakaa wife kutokana na Ratiba zangu za kilimo kuwa ngumu

Sasa siku moja alikuja mteja wa kiume na kujitambulisha kwa majina na kusema wao wamehamia mkoa wa Tanga kikazi.

Alitoa hela kama kawaida na kumuachia wife hela ya soda TSH 10000 na kuondoka.

Siku nyingine akaja na mtoto akatoa hela tena na kama kawaida akamuachia wife hela ya soda na kumtambulisha kwamba yule ni mtoto wake siku akiwa mbali atamtumia pesa na kumtuma huyo mtoto aje achukue na kweli alifanya hivyo kama mara mbili na kama kawaida alikua anamuagizia huyo mtoto aache hela ya soda.

Siku nyingine akaja na mwanamke na kujitambulisha ni mke wake alitoa hela kama kawaida akamuachia wife hela ya soda na akaacha maagizo kwamba siku akiwa mbali atatuma hela na atakuja kuchukua huyo mwanamke na kweli alifanya hivyo mara mbili na alikua anamuagizia huyo mwanamke amuachie wife hela ya soda hapo uaminifu kwa wife ukazidi maana alijua kwamba kumbe mpaka mke wake anaridhia kutoa hela ya soda basi hakuna tatizo usalama upo

SIKU YA TUKIO

Nikiri kwamba huwa nampa wife kila mbinu ya utapeli ninayoijua lakini hii nilikua siijui na sija muelekeza

Siku moja alikuja yule mteja na ki begi chenye fedha na kumwambia wife kwamba amuhifadhie Kuna sehemu anaenda ila hakuamini sana hivyo jioni atakuja kuzichukua zile pesa kwa uzoefu wa wife alisema ukiziangalia Kwa haraka haraka ni kama million tano, wife akazichukua zile pesa na kuzihifadhi pembeni.

Baada ya muda yule jamaa alipiga simu kwa wife na kumwambia huko aliko amepata changamoto amtumie million Tatu pesa si anazo akirudi atakata hela yake na kumkabidhi iliyobaki kweli wife alikua ana upungufu wa flot akaomba kwa wakala mwenzake na kupewa ila kabla hajatuma machale yakamcheza akakumbuka kwamba wakala unatakiwa kuhakiki pesa kabla ya kutuma.

Aisee wale wate ni mafundi chief Godlove anasingiziwa yaani vipande vya boksi vimepangwa kwa ustadi mkubwa na kuwekewa kiasi cha pesa kidogo juu ambazo baada ya kuzihesabu ni kama laki tatu.

Aisee Mawakala usije ukamuamini mtu yoyote kila mteja muone kama tapeli
laki 3 ulimrudishia tapeli?
 
Nasubiri umalizie alipoona hela ni za chief godlove alifanyaje, alimwambia jamaa na jamaa ali react vipi.
 
Pamoja na kutapeliwa vilevile huna Mke,una chagudoa a.k.a malaya.
Mwanamke anaye accept offer tena zaidi ya mara moja kutoka kwa Mwanaume mwingine unasemaje ni Mke kama sio changudua.

Jamaa angekuwa ndio mteja halisi angeendelea kumpa hela mpaka kuna siku angemla kiulaini.
kweli
 
hadithi za kufikirika
1.Hakuna tapeli mjinga wa kutoa elfu kumi ya soda kila anapokuja kufanya muamala.
2.Hulka ya binadamu lazima ustuke,faida ya muamala mmoja tu haifiki hata 5000.
mathalani mtu akitoa 3,000,000 Faida/Mrejaa/Commission ya wakala ni SH 2500 tu.
mtu akiweka 1,000,000 faida ni sh 1800 tu.Ndo aje akuachie 10000 ya bure bure hujashtuka tu.?
3.Yaani aache 10,000 kwa wakala kila anapokuja kufanya muamala ni kitu kisichowezekana kwa mpokeaji na mtoaji coz either mtoaji atamtia mashaka mpokeaji,ama mtoaji hajui hesabu za makato mpaka amuongezee wakala 10000 kila afanyapo muamala.
4.Na makabdhiano ya pesa ndefu kama hiyo ni lazima uifungue unapokabidhiwa kuhakikisha kama kweli ni mabunda ya M5.
By the way Umejitahidi kutunga na kuelimisha mawakala wazembe.Good job!
 
𝐞𝐭𝐢 𝐦𝐭𝐮 𝐚𝐧𝐚𝐤𝐮𝐩𝐢𝐠𝐢𝐚 𝐚𝐧𝐚𝐤𝐮𝐮𝐥𝐢𝐳𝐚 𝐮𝐧𝐚 𝐬𝐡 𝐧𝐠𝐚𝐩𝐢
 
Nasemaje biashara za miamala usimuweke mwanamke ata siku moja matapeli wanapenda Sana wanawake
 
hadithi za kufikirika
1.Hakuna tapeli mjinga wa kutoa elfu kumi ya soda kila anapokuja kufanya muamala.
2.Hulka ya binadamu lazima ustuke,faida ya muamala mmoja tu haifiki hata 5000.
mathalani mtu akitoa 3,000,000 Faida/Mrejaa/Commission ya wakala ni SH 2500 tu.
mtu akiweka 1,000,000 faida ni sh 1800 tu.Ndo aje akuachie 10000 ya bure bure hujashtuka tu.?
3.Yaani aache 10,000 kwa wakala kila anapokuja kufanya muamala ni kitu kisichowezekana kwa mpokeaji na mtoaji coz either mtoaji atamtia mashaka mpokeaji,ama mtoaji hajui hesabu za makato mpaka amuongezee wakala 10000 kila afanyapo muamala.
4.Na makabdhiano ya pesa ndefu kama hiyo ni lazima uifungue unapokabidhiwa kuhakikisha kama kweli ni mabunda ya M5.
By the way Umejitahidi kutunga na kuelimisha mawakala wazembe.Good job!
Sio ya kutunga sababu story kama yake nishakutana nayo sana kwa wakala haswa wa kike hizo pesa za soda kama chambo kuleta mazoea anaziwekeza anajenga mazoea undugu angefanikiwa kutapeli pesa yake ingejilipa.
 
Back
Top Bottom