Nilivyonusurika kifo Beit bridge

Nilivyonusurika kifo Beit bridge

Nimeona watu wakishare namna walivyopambana na baadhi ya matukio katika maisha Yao nami nimeona sio mbaya Leo nikaeleza namna nilivyonusurika kifo katika harakati za kutafuta maisha.

Mwaka 2007 nikiwa kijana mdogo 18yrs niliamua kwenda kutafuta maisha South Afrika nikitokea Dar na hii ni baada ya serikali kuwa imevunja maduka na vibanda pale kariakoo chini ya ndugu Kandoro akiwa mkuu wa mkoa wa Dar

Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya vijana nami nikiwa mmoja wao tuliona Giza mbele yetu binafsi nikaamua kuja kufungua duka Ukonga Mombasa ambapo baadae niliona kama halinipi maisha niliyokuwa nayataka(duka la Mangi)hivyo niliamua kumuita mama na kumkabidhi Ile biashara na kumuambia mi nataka kwenda SA kutafuta maisha.

Mama hakukubaliana na wazo langu Moja kwa Moja ila unajua sisi vijana wa kiume huwa tukiamua tena dam changa inakuwa sio rahisi kutuzuia basi hakuwa na namna aliruhusu nikafanya taratibu za pasipoti na viza (sikutaka kuzamia)nikapata na safari ya SA ikaanzia pale ubungo muelekeo ukiwa ni kupitia Zambia

Sasa mi nilikuwa naelekea Cape town maana huko ndio nilisikia maisha yapo na kusema kweli Kuna rafiki alikuwa kule (mrundi)alipita mitaa yangu nikamsaidia kwenda huko basi akawa anasema njoo.
Sasa kitu nilichemka ni hela maana kuhofia nisifilisi duka na kumuacha mama mnyonge ilibidi nijaze sana duka Kisha nichukue hela kidogo sana nadhani ilikuwa haizidi laki 3 ambayo niliichange kwenye dollar na Randi

Siku ikafika nikapanda basi hadi tunduma Mbeya kufika pale basi likadumu pale siku nzima ambapo Sasa tukajichuja na wanaoenda SA tukaonana rasmi na tukaanza kushare story za ndoto yetu hii kuu tulikuwa kama 6 mmoja mwenyeji si wengine wageni ila Hawa wengine 5 walikuwa wanajuana

Nikiwa tunduma pale ndio niligundua kuwa nimechukua hela kidogo kichwa kikawaka moto ila nikasema liwalo na liwe sirudi nyuma ,kufika jioni tukaenda kugonga pasipoti pale mpakani yule askari akaniuliza unaenda SA!?nikasema ndio akahoji mbona hujui kiingereza sikumjibu ukweli pale ndio nikajua umuhimu wa kingereza nje ya Tanzania
Safari yetu iliendelea hadi Lusaka ambapo tulifika asubuhi na kuunganisha gari kuelekea Zimbabwe

Tulifika Zimbabwe usiku kidogo pale Harare Kisha tukachukua hiace hadi mahali pengine ambapo ndio tulitakiwa kuchukua gari kwenda Beit Bridge hapa tulilipa nauli kubwa sana sijui kama niliibiwa au lah ila ndipo hela ilipoishia na nikabaki na Randi 120 pekee mfukoni hapa kumbuka kwa vile sikuwa na hela basi nililazimika kujizuia kutokula kwa hiyo nilikuwa na njaa sio poa

Tulifika Beit bridge asubuhi kama saa Moja hivi Sasa hapa ndio wale jamaa watano baada ya kuona kama vile story zetu haziendani wakaniambia hapa Sasa si tutaenda njia yetu na wewe inabidi uende njia Yako Mungu akipenda tukutane Joburg nikasema poa sikutaka kuonesha huruma
Nikatembea hatua kadhaa mbele yangu ikapaki hiace kubwa (dungu)na wakaniuliza "my friend Jo burg !?"nikasema Yes basi wakachukua ka begi kangu hadi ndani nami nikaingia nakutulia!!!!

Ndugu zangu hapa ndio muujiza ulipotokea na hadi Leo sijawahi kusahau
Ile hiace haikuvuka mpaka Bali ilirudi nyuma na kupaki kwenye kaeneo kama kaliko jitenga hivi Kisha jamaa aliyekuwa kama kiongozi wa Ile gari akaanza kunipa interview ya natoka wapi na naelekea wapi Kisha akaniambia kuwa Kuna abiria wanawangoja Kisha tutaondoka lakini mi nikiangalia gari naona imejaa ila ni vijana na mabinti ambao wote wanaonekana kujuana

Majira ya mchana hivi jamaa walichukua pasipoti yangu na Randi 100 Ile Randi 20 nilikuwa nimeificha sehem nyingine hapo Sasa nikajua kuwa siko mahali salama ila nikatulia sana pasi na kuonesha hofu yoyote
Jamaa kwanza wakaenda kuninunulia chakula supermarket ila nilikataa kula nikawaambia nimefunga na kuweka nadhiri kwa Mungu nitakula nitakapokanyaga SA (hii ni kweli) basi hawakunilazimisha

Siku ikaendelea nikawa nimetoa biblia na kuendelea kusoma jambo lingine ambalo hawakulielewa wale jamaa ni kuwa lugha Yao ya kizulu ni kibantu hivyo nilikuwa naelewa Kila wanachoongea angalau kwa uchache
Majira ya saa Moja jioni ikaja gari Moja nyeusi inayoweza kubeba watu watano basi jamaa wakaniambia my friend ingia ndani ya hiyo gari itakupeleka Joburg nikasema poa hakuna shida sikuhoji hata kidogo

Ndani ya Ile gari nilikaa kati ya jamaa wakubwa hatari dereva na jamaa mmoja walikaa mbele tukaenda kuvuka mpaka wa Zimbabwe pale nikaona Kuna signal baina ya mtu wa uhamiaji Zimbabwe na jamaa mmoja wao nikapotezea ila nikaweka moyoni
Tukaenda kabla hujafika boda ya SA ya kukagua viza huwa Kuna ka boda kadogo pale kati ambapo mnavuka kwa miguu Ile sehemu nilikaguliwa hadi nikasema hapa Sasa mnirudishe TU tz basi tukaendlea hapa wale jamaa hawakukaguliwa ila jamaa walikuwa Kila hatua wameniweka kati wawili mbele watatu nyuma

Tulipofika Sasa kukagua viza pale boda ya SA watu ni wengi sana kwa hiyo mnapanga mstari na ule mstari ni mrefu sana na umejaa nidham ya hali ya juu hakuna kuvunja line basi tukaingia kwenye mstari kama kawaida mi Niko kati Sasa pale pembeni nikaona Bomba la maji nikasema hapa patam
Hapo walikuwa wamenirudishia pasipoti yangu ninayo mkononi nikaacha ule mstari ukaenda hadi kuingia ndani nikasema nasikia kiu ngoja nikanywe maji pale jamaa kama wakastuka ila wakapiga kimya

Nikatoka nikaenda pale bombani nikanywa maji kiuongo Kisha nikaenda ilipopaki gari kioo kilikuwa na nafasi nikakidandia nikatoa kibegi changu njia hadi polisi nikafika nikatulia pale polisi nikakuta Kuna polisi mmoja mbavu kinyama nikamwambia mkasa mzima jamaa akanielewa sijakaa dk hata moja jamaa wakaja kunitafuta pale polisi nikawaambia my friend siwaamini na naomba nisiongozane na nyie basi nikawa nimeponea namna hiyo

Yule polisi alinisaidia kuwasiliana na jamaa yangu Cape town ambae alikata tiketi ya treni kutoka Mesina hadi cape town asubuhi jamaa alinichukua na gari ya askari hadi Mesina akanipa maelekezo yote nilitumia Ile Randi 20 kupata chai asubuhi ndani ya SA jioni treni ikaja nikaanza safari yangu kuelekea Cape town
NB:huwa sio msimuliaji mzuri ila nimeona niweke hiki Kisa hapa ili siku Moja Nije kusoma na kukumbuka namna Mungu alivyonilinda ndani ya Ile nchi
Kama hujawahi kuishi SA basi hujui maana ya kuishi mahali penye hatari duniani Yale unayoona kwenye movie zao ni 4%ya uhalisia wa mitaa Yao
Niliishi Cape town kwa mwaka mmoja Joburg na Pretoria kidogo Kisha nikarejea kwenye nchi ya Samia
Mkuu nimeishi Retreat Capetown kwa miaka mitano tena ktk hizo flat.Upo sahihi kabisa.

Je umewezaje kutulia na kukomaa na life la Bongo?Nina miezi sita toka nirejee lakini bado Sijasoma ramani licha ya kwamba nina kimtaji changu ila naona kila nikiangalia fursa naona giza.
 
Mkuu nimeishi Retreat Capetown kwa miaka mitano tena ktk hizo flat.Upo sahihi kabisa.

Je umewezaje kutulia na kukomaa na life la Bongo?Nina miezi sita toka nirejee lakini bado Sijasoma ramani licha ya kwamba nina kimtaji changu ila naona kila nikiangalia fursa naona giza.
Rudi zako SA. Hapa hapaelewek hata Dola (USD) kupata ni kwa dili. Ukijichanganya biashara utawajua TRA vizuri. Kiufupi hapa umeyatimba.
NB: Wauza sembe ndio wanatamba
 
Hahaha South hawana hurumaaa mkuu nilikuwa joberg birtchwod hotel kama mwezi na jamaa wakazin

Tukajichangajya club caption park wacha kabisa kaja mdada anaongea kiswahili..tukajua mwenzetu wacha tumzooee ..tukamkaribisha hotel ni...

tukakagonga wee weekend sasa tumerudi pale pale club kama jamaa mwingine anajuana na kadada mbongo tukamfurahia..mmoja wetu akaonyesha ana hela aka za kuwazungushia pombe wewee..yaan kutoka kuitafuta tax tuliakia makofi puffffy wote sek wachatusachi kila kityu mmoja akasema mmekuja na hela njooni tena kiswahili..
..nkajua kale kadada kametuchoma yaani mwaka wa tatyu nikikumbuka nasikia sikioo linauma yaaani kofi utahisi nyundoo...

Wabongo wanamalizana sana
Hahaaaa ,wakaona mbugila hizi zimetoka Bongo kuja kuturingishia pesa ,mamaee makofi na kuporwa juu
 
Mkuu Zimbabwe miaka ya 2000 kushuka chini, ilikuwa na uchumi mkubwa zaidi ya Kaburu.

Alichoharibu Mugabe ni ile sera yake ya kuwapora mashamba wazungu wazawa na kujimilikisha yeye na genge lake.

Baada ya hapo uchumi wa Zimbabwe ukaporomoka mara 10 zaidi ya uchumi wa Burundi na Congo. Sasa katika hali kama hiyo unafikiri nani atapakimbilia hata kama mji wao msafi lkn watu hawaendi sehem kwa ajili ya usafi wa mji. Bali wanakwenda kwa ajili ya kutafuta ahueni ya maisha.

Mkuu mbona wazalendo walimsifu sana Mugabe kwa kitendo chake cha kuwafukuza wazungu mabwanyenye?!
 
Asante ila mi ni Mungu aliingilia kati nje ya hapo nilikuwa sitoboi panahitaji utulivu mkubwa sana na ukiwa na kiongozi Inasaidia ila ukiwa solo tena mara ya kwanza kupotea ni kugusa
Kumbuka uliondoka ukiwa umemuacha your mama anajua uko safarini, so ulikuwa moyoni mwake hata wkt unawasiliana na mwenyezi Mungu hadi kusoma maneno yake, naye hakuona nia hovu kwako akakupa kampani ndiyo maana ukatoboa.

Vijana wengi hujitutumua sana wakitegemea uwezo wao na maguvu ya mwili na kumsahau Mola na ndiyo maana sometimes kuna kufail sana.
 
Hivyo ni vingi mno mkuu na mi sio msimuliaji mzuri ila tangu naingia Musina hadi nafika Cape ni miujiza TU
Kwanza pale Musina nilienda kunywa chai na slace ya mkate mama muuza akaniuliza unatoka nchi gani nikamwambia "Tanzania"akainuka kwa tahadhari kubwa na kuondoka pale ndio nikajua tz ni red flag kwa SA baada ya hapo kwa utulivu TU Nika switch ukiniuliza natoka wapi nasema Burundi basi
Sikutaka kutengwa
.
 
Ni nchi hatari sana saa 12 wote MKo ndani Wala sio amri ya serikali ni amri ya magenge ya uhalifu
Hii ni kwa wale wanaokaa township, hususa ni huko Mandalay Gugulethu, Philipi, Delft, Danoon, Langa, Nyanga na maeneo mengine yanayofanana na hayo, kwa miaka miwili niliyoishi capetown (blouberg) hakukuwa na matatizo haya kabisa.
 
Back
Top Bottom