Nilivyonusurika kifo Beit bridge

Sababu hasa za vurugu zilisukumwa na nini kama unakumbuka?....ni raia wa kundi lipi walilengwa zaidi ?

na response ya serikali ya huko ilikuaje ?

Bado hizo chuki dhidi ya wageni zipo mpaka sasa ?
 
Seen.
 
Tusitishane basi mkuu!

Unataka kuniambia Warundi wanakubalika SA kuzidi Watanzania?

Hawamjui Nyerere?
Sio kwamba Nyerere hawamjui au Tanzania hawaijui au hawaipendi.

Watanzania ndio raia ambao washafanya matukio mabaya na yenye kutisha katika nchi nyingi za kusini mwa Afrika.

Mfano ukienda Maputo katika wageni labda watano au kumi wanaokamatwa wakiuza madawa ya kulevya, bangi au uhalifu wowote, basi hapo utakuta watanzania ni wawili au watatu kati ya watano waliokamatwa.

Hivyo hivyo kwa Sauzi au nchi zingine za bondeni. Ni kama vile unavyoona wanigeria kwa uhalifu. So wananchi wengi wanatuogopa kutokana na vitendo hivyo.
 
Hata kwa abiria aliyepanda basi la moja kwa moja kutokea Dar kwenda SA kupitia Zimbabwe anaweza kukutana na hiyo changamoto ya kiusalama?
Hata ukipanda la kuunga unga au moja kwa moja. Kama una document nzuri, na pia una maelekezo mazuri au una mwenyej wa kukuongoza basi hauwezi kukumbana na matatizo yoyote mpakani.

Wanaokumbana na matatizo ni wale wanaokuja bila vibali vya kueleweka, alaf wakifika hapo beit bridge wanatafuta watu wa kuwapitisha njia za panya ili waingie kinyume na sheria, matokeo yake hao wanaojifanya kuwapitisha njia za panya huwaibia, vijana hujeruhiwa, wanawake hubakwa na wengine kuuwawa kabisa.
 
Za Wazungu ni Kingereza na Kikaburu?
Ndio mkuu.

Sauzi ni nchi iliyotawaliwa na mataifa mawili ambayo ni UK (waingereza) na Netherlands (waholanzi)

Hawa wazungu waliotokea UK wao wanaongea kingereza na hawakuwa makatili sana, ndiomaana weusi wa hapa walijifunza lugha yao na ndio lugha ya taifa kwa sasa (namaanisha lugha ya kwanza ya mawasiliano kwa watu wa rangi zote)

Hawa wazungu waliotokea Uholanzi ndio hao wanaoitwa makaburu neno hili linamaanisha "wakulima". Hawa kihistoria walikuwa makatili sana na ndio waliotesa weusi zaidi. Hawa lugha yao waliibadilisha kutoka kiholanzi na kuiita Afrikans ila wakiongea mtu wa uholanzi anaelewa vizuri ni kama English na UK na ile ya Canada, Australia au USA.

Pia kuna lugha 7 za wazawa weusi ukihitaj nitakwambia.
 
Mbona hakuna watu wanaopakimbilia huko kama nchi zingine?
Mkuu Zimbabwe miaka ya 2000 kushuka chini, ilikuwa na uchumi mkubwa zaidi ya Kaburu.

Alichoharibu Mugabe ni ile sera yake ya kuwapora mashamba wazungu wazawa na kujimilikisha yeye na genge lake.

Baada ya hapo uchumi wa Zimbabwe ukaporomoka mara 10 zaidi ya uchumi wa Burundi na Congo. Sasa katika hali kama hiyo unafikiri nani atapakimbilia hata kama mji wao msafi lkn watu hawaendi sehem kwa ajili ya usafi wa mji. Bali wanakwenda kwa ajili ya kutafuta ahueni ya maisha.
 
Nilipata kidogo nikaja kukichanganya na makaratasi nikapata cheti kimoja(degree)basi Niko kwenye serikali nalalamikia daraja na seminar
 
Wamalawi nao siku hizi ni washenzi. Toka wajifananishe na wabongo na wenyewe wamekuwa wasela Mavi.

Wanakaba, wanapiga michomoko ya usiku, wanavaa kata K, na kupiga watu vitasa kama kawa.
Basi hapo wamepoteza point ila way back wao walikuwa na unafuu kidogo
Ila wa tz ni namba ingine SA hata binafsi nilikuwa nawadanganya na wanakubali kuwa mi sio mtz wao walikuwa wanajua mi mkongomani ilinisumbua sana Pretoria kupata msaada ubalozini
 
Habari imefika,dogo wangu alilambwa visu mara 4.
Nilimpeleka mwenyewe akatafute maisha nikamrudisha mwenyewe.
Mi mara ya kwanza nilipambana imagine naokoa baiskel mara ya pili nilikutana na colored Wana panga za maana nikawauliza Nini wao Rand mbona niliwapa kiroho safi wakaondoka bila kunigusa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…