Nilivyomtamani rafiki wa mpenzi wangu, na kuambulia 'block'

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,421
40,411
Siku moja, nimejichokea zangu mida ya saa nne usiku, nikaamua niende 'club' nikapate 'vibe' la kule ili niweze kuondoa 'stress' za maisha.

Muhudumu akaniletea bia zangu tano za kuanzia, nikazinyonya zote zikaisha; akaniongeza tena zingine. Baada ya kufika ya nane, akili ikahama, nikajiuliza kwa nini nakunywa pekee yangu; inabidi nitafute mrembo wa kunipa kampani.

Basi nikawa nainua macho huku na kule, angalau nione mrembo machchari atakayenivutia kimuonekano na unenguaji. kwa mbali nikamuona mlimbwende mmoja , ana mzigo wa kichokozi; kichwani amesuka rasta ndefu zinafika kiunoni.

Nikamsogelea huku nimeshika glass yangu, huku nikimtizama bila kumuambia chochote; nikamuuliza unakunywa kinywaji gani mrembo?, akanijibu savana.

Muhudumu aliyekuwa ananihudumia, akaja kumsikiliza, na akamletea nne. Huku tunakunywa huku tunachombezana hapa na pale; ili asinione lofa, nikamuagizia nyama choma kidogo.

Ghafla mrembo akaniuliza, baby si tutaondoka wote?, nikamwambia hakuna matata we kula maisha; maisha ni haya haya.

Baada ya usiku kuwa mnene sana, ikabidi tuondoke twende nyumba ya wageni ''lodge'', kufika kule, mhudumu akanipatia vitendea kazi ili niweze kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.

Kazi ilienda vizuri sana, kila mmoja alitaka aonekane anajua zaidi kuliko mwenzake.

Wakati wa mapumziko, huku akichezea 'radiator' kifua; akaanza kuniambia, unajua baby kwenye huu mkoa, watu wengi wanapenda starehe sana, unaonaje sasa ukanifungulia ka-grocery kadogo angalau na mimi niwe bize kusimamia? Kupiga mahesabu ya haraka haraka kichwani, mahesabu yakawa yanagoma.

Nikaamwambie nipe muda niweze kutafakari na kujipanga.

Kesho asubuhi tukaachana; baada ya siku tano kupita, nikaona niende tena kwenye kile kiwanja kuosha macho na kusikiliza mziki. Sijakaa sawa, meseji inaingia kwenye simu; ''baby njoo kwenye hii meza karibu na kaunta hapa, nimekuona''. Kutazama vizuri, ni yule mrembo yuko na wenzake watatu.

Nikamjibu, nitakuja baadaye; akanilazimisha angalau niwape salamu. Basi nikawasogelea pale nikawasalimu, akanitambulisha kwa wenzie; ghafla jicho langu likagongana na rafiki yake, amenoga ile mbaya, moyo ukaanza kwenda mbio; Nikaishia kumshika mkono tu.

Basi nikarudi kwenye meza yangu, kwa sababu nilijua nikikaa nao, ningekosa hata buku ya kuagizia maji.

Kwa sababu rafiki yake alikuwa ameniteka zaidi; nikamtumia meseji anipe namba za huyo rafiki yake, akaniuliza utamuweza? Nikamwambia, kwa nini nisimuweze?

Akanifokea, huna adabu wewe, unataka utembee na rafiki yangu, kwani kwangu umekosa nini; kuanzia leo tusitafutane.

Nikamwambia, lakini wewe si ndio umenikutanisha nao; baada ya hapo nikaambulia 'block' tu.

Ndio tukawa tumeachana hivyo
 
Usiku mmoja tu kukutana mshakua wapenzi dah
 
Alitaka akumiliki kiboya..
Wkt ni muuza nyaku tuu.
Wako sana madem wa hivyo!na hivyo umefanya hata mi huwa nafanya ili kukata mazoea
 
Kweli mkuu, mazoea yakizidi unaweza usipige hatua kimaendeleo
 
Baada ya usiku kuwa mnene sana, ikabidi tuondoke twende nyumba ya wageni ''lodge'', kufika kule, mhudumu akanipatia vitendea kazi ili niweze kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.
Screenshot_20230308-203702.jpg
 
Back
Top Bottom