Nilivyoingiza 17.6M ndani ya mwaka mmoja na nusu, kwa biashara ya Mgahawa kwa mtaji wa kawaida kabisa

Na kwenyewe kule mkuu ungeenda ungetengeneza fedha nimetokako karibuni watu wenye migahawa ikifika saa 3 usiku huwezi kupata chakula na Ni mgodi mkubwa Sana !! Watu Ni nyomi utasema lowasaa kaitisha mkutano wa kuomba kura
Iko mkoa gani na wilaya gani hkk NYAMISHEGA
 
Hilo la kupotea kwa cash nimelisikia kwa wafanyabiashara wengine pia baada ya kuuliza, pengine wapo humu pia labda.

Ni sawa mkuu, mimi nimejaribu kuelezea uzoefu wangu juu ya huo mradi bila kuficha kitu na hakuna sehemu ambayo nimejaribu kushawishi watu kupita njia zangu. Hata mimi sikuwahi kufikiria katika biashara nyingine zote nilizowahi kufanya, pengine labda mazingira ya unapofanya nayo yana athari zake. Huenda Bariadi ikawa ni tofauti na huko uliko.

Mwisho wa siku tunaangalia namna ya kufika point fulani, njia zinaweza kutofautiana.
Kwa mtu ambae halijawahi kumkuta atabisha sana swala la kupotea kwa hela. Mimi pia nilikuwa na biashara ya chakula nilikuwa nauza sana na chakula kinaisha ila ikifika muda wa kufumga hesabu huna unachobaki nacho.

Kuna mtu aliniambia nitakuwa nasahau nikinunua vitu, basi nikamkabidhi kitengo cha chips na nyama choma. Siku ya pili kauza hajanunua chochote na asubuhi alikuwa na chenji za mauzo ya jana yake kama 50000 hivi zote zilipotea.

Location ya ile biashara ni nzuri sana ila shida ni kupotea kwa pesa. Kama hajakukuta utabisha mpaka kesho ilifika kipindi nikawa narekodi kwenye daftari kila sahani inayouzwa nione nakosea wapi.
 
Wewe sasa ndo umeelewa nilimaanisha nini.

Biashara haiwezi kwenda kichwakichwa au kwa kutegemea unayoyajua tu, huku mitaani kuna mabingwa wa kuharibu jitihada za watu kwahiyo bila kuwadhibiti hakuna hatuna unaweza kuivuka.

Hili huwezi kulielewa mpaka uingie ulingoni.
 
Biashara haiwezi kwenda kichwakichwa au kwa kutegemea unayoyajua tu, huku mitaani kuna mabingwa wa kuharibu jitihada za watu kwahiyo bila kuwadhibiti hakuna hatuna unaweza kuivuka.
Mimi nilikata tamaa nina miezi kadhaa nimeifunga biashara, maana mwisho wa siku unalipa hadi pango kwa kutoa hela nje na biashara, ila Mungu akijalia nitarudi tena maana ni biashara ninayoipenda.
 
Moja kati ya biashara nzuri ni hoyo maana haina trend wala misimu, ukipata muda rudi uifanye katika namna nzuri zaidi, naamini kuna vitu tayari umejifunza na hautavirudia tena.

Usirudi kabla haujaimaliza shida iliyokufanya ushindwe mara ya kwanza.
 
Naomba nikutafute kama ulivyosema ( kama ilikuwa serious) mkuu nakupataje??
 
Mkuu igombe vipi ulifanikiwa kufungua?
 
Naomba nikutafute kama ulivyosema ( kama ilikuwa serious) mkuu nakupataje??

Mawasiliano yanaweza kufanyikia hapa (kama haujali privacy) au PM (kama unajali privacy).

Namba za simu pekee ndio kitu ambacho huwa siwezi kutoa.

KARIBU.
 
Pm yako haiwezi kuanza kupokea meseji, naomba nitumie kwanza if its okay
 
Baada ya hesabu na kuwalipa wafanyakazi kukunja 60k-70k kama faida ilikuwa ni swala la kawaida kabisa. Nikikaa pale kama cashier kwa wiki tatu kisha baada nikaleta ndugu asimamie ili nirudi mwanza kuendelea na issue nyiingine ila akaanza kuniletea habari za faida 20K wakati mimi nishapiga hesabu za mbali kabisa, nilimtoa nirudi mwenyewe mzigoni
Dah, hapa ulicheza vyema kabisa yani kidogo ukabidhi nyani shamba la mahindi. Biashara ni mtu mwenyewe, yani ukiweka ndugu, halafu ukawa kazi yako ni kupiga simu tu kama telephone operator lazima ulie.
 
Back
Top Bottom