Nilivyohangaika kumfukuzia Hagai Ngoma mtoto wa TPC, Moshi

Opuk Jater

Senior Member
Dec 25, 2018
145
130
Habari wanandugu,

Ilikuwa mwezi wa 4 mwaka 2007 nikiwa zangu hospitali ya KCMC Moshi huko nimeenda kufanya field. Siku moja tukiwa tunakaribia kumaliza shifti akatokea mama mmoja na mwanawe wa kike akihitaji kupimwa.. Aisee mtoto Hagai alikuwa chuma si kitoto..

Nikampima huku nikitamani niachiwe hata dakika niombe contacts, ikashindikana na kuambulia tu jina Hagai lililoandikwa kwenye fomu ya vipimo.. Ijumaa iliyofutia ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu nikiwa nazunguka kwenye korido mara nikamwona tena Hagai akiwa na mama yake wakiwa wanatoka nje ya geti kuu la Hospitali.

Ikanibidi nivue koti na nigeuze nianze kuwafuatilia nikijipa imani kuwa leo lazima nijue anakaa wapi, yaani hata kwenye daladala nitakwenda nao... Muda wote huo Hagai alishaniona akawa anageuka na kuniangalia na kutabasamu...

Sasa baada ya hatua chache nikaishiwa nguvu maana nikaona wanakata kulia kuelekea yalipoegeshwa magari binafsi wakati mi nilishajitayarisha na daladala...

Ikabidi nitumbue tu macho na kuambulia kuijua tu gari ilikuwa ni pickup rangi ya *****. Nikarudi zangu ndani, lakini nikajipa moyo kuwa nikienda TPC ziwezi kukosa kupajua kwao...

Sasa Jumatatu ambayo ilikuwa ni Pasaka nikazama zangu Pasua stendi nikachukua ki-hiace cha kwenda TPC, enzi hizo barabara ni vumbi la kufa mtu...

Baada ya mwendo tukatokea kama ka-centre fulani hivi nikaona abiria karibia wote wanashuka nikajua hapa ndo patakuwa centre yao na siwezi kukosa Mtu wa kunielekeza...

Nikashuka nikavuka barabara nikakaa chini ya limti likubwa nikisoma ramani... Ng'ambo nikaona saluni ya kiume na mshikaji flani white kakaa nje kwenye benchi nikaona niende kumuulizia.. nikavuka tena barabara nkaenda kwa mshikaji pale nikamsalimia na kumuuliza kama anamjua mzee ******* mwenye pickup yenye rangi ******.

Yaani ile namaliza kumuuliza tu jamaa wala hakunijibu yeye akaita jina la kike na mtu akaitika kwenye fremu iliyofuatia.. Yule mdada alipofika jamaa akamwambia tu "MGENI HUYU HAPA ANAMHITAJI MZEE ******

Du! nikashangaa ila nikasema ngoja nione itakuaje... Tukaingia na yule dada pale kwenye duka ambalo lilikuwa la nguo na vinywaji... Nikakaribishwa kwenye kiti ila mwenyewe nikanunua soda.

Tukiwa hatujaanza maongezi yoyote mara simu yake inaita akapokea katika maongezi yake nikagundua kuwa Hagai ni mtoto wa kaka yake, na familia yote iko nyumbani maana ilikuwa sikukuu... Vilevile akawaeleza kuwa mmoja aje anichukue anipeleke nyumbani maana nina shida na mzee...

Hapo nilihisi 'nya inagonga kufuli na kurudi maana kama familia yote ipo nyumbani it means mama yake yupo na atakuwa ananikumbuka kuwa tumekutana KCMC hospitali na iweje tena niwe mgeni wa mzee?

Baada ya kama dakika 10 nikaona mdada mwingine anaingia na anaulizia mgeni.. Nikaitika.. Kwa haraka nikapata njia ya kuchoropoka, nikawauliza kuwa kwani huyu mzee anaitwa E******" bin N****"", wakaniambia hapana..

Sasa cha ajabu kumbe jina lake ni tofauti ila naye linaanza na E kama nililotaja Mimi... Nikawauliza kwani huyu ni mstaafu, wakaniambia hapana, kumbe huyu mzee ana cheo kikubwa pale kiwandani....

Nikasema "DU! ITAKUWA SIYO YEYE KABISA MAANA NILIYEMFUATA NI MSTAAFU AMBAYE ANAFANYA BIASHARA NA MZEE WANGU"...

Nao wakakubali nikatoka nje nikitamani nipotee lile eneo maana niliwaza kuwa kama yule mshikaji wa mwanzo wakiongea naye anaweza kuwaambia mbona nilitaja aina na hata rangi ya gari...

Nilipovuka tu na daladala ikaja nikapanda zangu na kuondoka na sikuwahi kurudi tena TPC na hata sijui HAGAI MTOTO WA TPC yu wapi......

Hope hii stori IPO siku ataiona 😎
 
Duuuh fiksi ya kiwango

Hope hii stori IPO siku ataiona
 
Da umenifurahisha sana baharia
 
Back
Top Bottom