Ananionesha mahaba mazito ila kila tukikutana amekuwa mtu wa vijisababu

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
433
695
Habari kwa wana Jf,

Kwa upekee sana ninawapa salamu wana MMU wote. Mimi ni mgeni wa jukwaa hili na ninawaomba mnipokee.

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Ipo hizi, nilikutana na huyu mwanamke kwenye sherehe baada ya kuoshiriki pale kwa kitambo nikaondoka. Baada ya siku moja kupita nilimuomba mmoja kati ya watu aliyekuwepo kwenye sherehe anitumie picha tulizopiga pamoja siku ya sherehe. Baada ya muda nikatumiwa picha whatsApp na namba ngeni, baada ya kujibu nikagundua alikuwa mwanamke mmoja ambaye alikuwepo kwenye sherehe.

Baada ya siku kama mbili tulikutana majira ya usiku, muda huu nilikuwa nikirudi kutoka kwenye shughuli zangu za uzalishaji mkate. Baada ya kukutana naye alitaka tuingie anakokaa (kapanga) nilimwambia nilikuwa na haraka na ningeondoka baada ya muda mchache. Sijui alikuwa na genye maana alinishika mguu kwa ghafla, baada ya kumuuliza kulikuwa na nini (niliuliza nikijua alichotaka ila nikaona bora kuuliza kwakuwa sikuwa na uhakika).

"Kuna mdudu amepita mguuni" ili ndilo jibu alilonipa, nikaona haikuwa na shida sana na nilitaka kuondoka.

Baada ya kama nusu saa akinisimulia vitu ambavyo havieleweki alinikumbatia ghafla na kuishia kusema "samahani" ,kwa siku hiyo nilikuwa hovyo hovyo na sikuwa na hamu na mwanamke kwakuwa nilivurugika toka mchana kwahiyo na mimi nikampa ushirikiano wa kumkumbatia na baada ya hapo nilimuona akisisimkwa na kunifata na kunipiga busu zito, na mimi nilimpa ushirikiano na nikaona kabisa ni genye zilizomsumbua. Sijui ilikuwaje na mimi nilipatwa na ashki ya tendo ila nafsi ilikuwa inasita sana nikamuaga na kuondoka.

Baada ga siku kama tatu akiwa ananichatisha sana nikamgusia kuhusu kukutana naye na yeye akasema anatamani tukatembee mahali na baada ya hapo tuagane nikakubali ila nilipomfuata akaanza kunipa sababu na akaishia kusema hatoweza kutoka na anajisikia vibaya, baada ya tomaso chache naona kabisa hana ushirikiano nikasepa.

Siku ya jana amenitumia (huyu mwanamke) kanitumia meseji ananiambia ana mtu wake na mambo mengine mengi nikamuuliza sasa alikuwa ananipa makisi yale ya nini ameishia kuumauma maneno na anadahi ananipenda kama kaka yake tu!

Shida hapo ni nini? Au mimi ndiye niliyepoteza?
 
Ulishajijibu mkuu....alikuwa na genye it's true, ila kampata mtu KAMUWEKA sawasawa, hivyo huna maana Tena kwake, temana nae TU kwa usalama wa nafsi yako, utakuja kunishukuru ohoooooo!!!
 
Siku aliyokuhitaji ambayo ulitambua kabisa nini kinamsumbua YOU FAILED HER. Kilichokuwa kinamsumbua kimeshawekwa sawa na aliyetambua na kuchukua hatua, UNAJIPELEKA PELEKA. Once a chance is gone call it a bygone bro😃😃
Angalia mambo yako mengine
 
Back
Top Bottom