Nilivyoanza safari ya kuwa Youtuber πŸ˜€

refan

Member
Joined
Feb 14, 2025
Posts
11
Reaction score
17
Wakuu salama? Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mimi nilitaka sana kua youtuber, hivyo nikasema lazima nijaribu nikifeli ni sawa.

Basi nikafungua gmail hatimae channel, safari ya gaming content ikaanza Octoba 2022, Sina ujuzi wowote, muda kidogo nikapigwa strike kadhaa, Nikajifunza, nikaendelea hadi March 2024 nikaingia monetization, safari ikaendelea hadi 2024 sikufanikiwa ku pokea pesa sababu sikufikisha kigezo cha 100$, Hivyo ilivofika April 2024 nikafungua channel nyingine kwasababu channel ya mwanzo ilikua taratibu sana.

Baada ya miezi mitatu (July) nikakubaliwa monetization ilivyofika September nikapokea paychek ya kwanza 109$, vivyo hivyo miezi iliyofuata: Hivyo Nimejifunza kila kitu kinawezekana ukitia bidii na bado napambana nikuze channel yangu zaidi :Usikate tamaa
 
weka chanel yako hapa tu subscribe
 
Kama una account ya gmail basi ingia kwenye app ya youtube. Kwenye account settings kuna sehem ya kufungua channel. Kila la heri
Asante
Kwa hiyo nitaweka account ya bank ili pesa ziingie huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…