Nilitakiwa kulipa tsh 20,000/= badala yake nikalipa tsh 200,000/= . Je kuna uwezekano wa kurudishia kiasi kilichozidi?

macjay

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
371
408
Nimefanya malipo ya bili baada ya kutumia huduma katika idara moja ya serikali kwa kutumia control number kwa njia ya simu.
Nilitakiwa kulipa tsh 20,000/= badala yake nikalipa tsh 200,000/= .
Je kuna uwezekano wa kurudishia kiasi kilichozidi kwani katika meseji ya risiti wameandika ilo zidio.
Utaratibu?
 
Control nyingi za serikali ukilipa kiwango tofauti na bili kinakataa; acha kutulaghai
 
Cikupenda kuweka wazi idara ...jaribu mamlaka za maji uone kama itakaa
Nimetumia neno "nyingi" na sikutumia "zote".

Fanya process ya kurudisha pesa kama inawezekana kwa kuomba maelekezo toka "provider" wako
 
Control nyingi za serikali ukilipa kiwango tofauti na bili kinakataa; acha kutulaghai
Sio zote zinakataa,zingine ukilipa pungufu ndio zinakataa ukizidisha inakubal,nadil na mfumo kwenye wizara yangu naelewa,lakufanya aende ofisi husika wayaingize malipo ya ziada then kila mwezi itakuwa inajideduct taratibu,kurudisha fedha hakupo
 
Ni ngumu sana sana sana .... hasa kwa malipo ya serikali tena ukitumia control number.

Why?

- Kwa sababu TRA tayari wanakuwa wameshakata VAT ambayo huwa hairudi
 
Utaratibu ni kuwa unatakiwa kuandika barua kwenda idara ya hiyo taasisi. Mara nyingi utaielekeza barua yako kwa mhasibu.
Utarudishiwa kiasi kilichozidi baada ya wiki kadhaa au mwezi, pia unaweza usirudishiwe badala yake utakuwa umejijengea uaminifu kwa kulipia bill zijazo.
 
Nimefanya malipo ya bili baada ya kutumia huduma katika idara moja ya serikali kwa kutumia control number kwa njia ya simu.
Nilitakiwa kulipa tsh 20,000/= badala yake nikalipa tsh 200,000/= .
Je kuna uwezekano wa kurudishia kiasi kilichozidi kwani katika meseji ya risiti wameandika ilo zidio.
Utaratibu?
asante sana mkuu kwa kuunga mkono Juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kuichangia 180,000/=. Mchango wako utatumika vizuri katika shughuli za maendeleo
 
Nimetumia neno "nyingi" na sikutumia "zote".

Fanya process ya kurudisha pesa kama inawezekana kwa kuomba maelekezo toka "provider" wako
Sasa kumbe unajua ni nyingi na sio zote kwa nini unasema anakulaghai?
 
Hapo sahau kurudishiwa hio hela....we fahamu tu kwamba umelipa advance ya miezi 9 mingine(kama bili zako ni 20k kwa mwez).Tegemea kuanza kudaiwa April 2020,haya sasa tafuta hela ya kula mwezi huu
 
Back
Top Bottom