Nilitaka kumuua mke na mtoto wa 'my best friend' kwa risasi!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Mimi ni muajiriwa wa JWTZ Kikosi cha 202 Faru Tabora. Nilipokutana na binti mrembo wa ki-singida nikampenda na kumueleza azima yangu kwamba namuitaji kifamilia na akanielewa. Na tukawa ktk mahusiano.

Lakini sababu alikua mwanachuo hatukuwa na haraka ya ndoa mpaka atakapo maliza chuo mwaka 1 baadae. Nilimuuliza kama ana boy friend maana nimekuta mlango umeshafunguliwa so niliitaji kujua hatima ya huyo aliyefungua mlango. Akasema sii mkweli na alishaachana nae kitambo. Nikasema ok, fine. Nilitaka kumjua mwenyeji wake Tabora na akaniambia amekuja likizo kwa sister wake pande za chemchem.

Nilimuomba anikaribishe kwao ili nipafahamu hakuwa na kikwazo juu ya hilo. Baada ya kufahamiana vizuri kiasi tuliendelea kula tunda, siku1 tukiwa chumbani kwangu huku tukiangalia albam alishangaa kuiona picha ya mtu fulani niliyepiga nae picha tukiwa depo...aliniuliza kuhusu huyo mtu na nikamwambia yes namfahamu vema ni my friend wa kitambo sana. Nilimuonyesha na picha nyingine za utotoni.

Cha ajabu majina na kazi yalikua tofauti na alilonitajia yeye alisema anayemjua anaitwa MASIGITI na ni TICHA WA SEC pale SINGIDA, na mimi ninayemjua ni John Manyama na ni askari wa JWTZ NGERENGERE MOROGORO. So tuliamua kupuuza na kuamini kwamba duniani ni 2x2...... binti alikua akienda chuo SINGIDA na alikua akija Tabora mara kwa mara.......siku 1 niliamua kumtafuta my friend Manyama ili nimpe taarifa hizi,lakini kwa bahati mbaya mawasiliano yalikua magumu sana.Zilipita siku,wiki,miezi mara binti akaniambia yu mjamzito.Nilifurahi sana na nikapanga safari ya kijijini kwetu ili kuwajulisha juu ya mimi kuoa mtoto wa kinyiramba.Kwa mila za kikwetu nilijua kabisa kwamba itakua ngumu wazazi kunikubalia.Lakini nikapiga moyo konde nikaelekea kwa wazazi wangu MUSOMA-MARA.

Wakuu ngojeni kidogo hapo hapo nakuja kuendelea na story hii yenye majonzi na huzuni mkubwa.....................

TUENDELEENI SASA:
Nilifika kijijini kwetu majira ya saa 4 usiku,wazazi wangu walifurahi sana kuniona na akachinjwa mbuzi usiku huo huo ili nitengenezewe ili kitu yetu inaitwa "KICHURI" baada ya kula nikenda chumbani kwangu kupumzika, asubuhi na mapema nilikata shauri kwenda nyumbani kwao my best wangu tuliyepoteza nae mawasiliano ili nijue ni vipi ntampata? Maana hatukua na mawasiliano tangu tulipopangiwa vituo vya kazi. Cha ajabu baada ya kufika kwao nikaambiwa kwamba walikuwa wanategemea labda mimi ntakua na taarifa nae maana inasemekana kwamba alitoroka jeshi na anatafutwa maana alitoroka na baadhi ya vifaa vya jeshi.

Taarifa hii ilinikumbusha tukio 1 pale kambini kwetu Tabora nilipoitwa kuhojiwa kuhusu inshu fulani fulani hivi ambayo huwa ni upelelezi wa kijeshi,lakini walibaini kwamba hata mimi sijui kitu.Walitegemea wangepata taarifa zake kupitia kwangu maana we was big friend kiukweli,nikawaambia sijui chochote kabisaaaa kuhusu John,i will be back again........

Niliporudi nyumbani niliwaeleza story nzima kuhusu safari yangu na wakanikubalia ombi langu maana tayari binti alikua tayari ni mjamzito.

Tulipanga baadhi ya mambo na nilipewa kazi ya kufatilia kujua wataitaji mahari(ng'ombe)kiasi gani.Becouse nilienda na picha basi ilifanyika tathimi kupitia picha kwamba tuandae ng'ombe 25-30.

Nilifurahi sana maana niliona ni jinsi gani wazazi wanavyonipenda.

Baada ya maongezi hayo walinigusia swala la my friend aliyetoroka jeshi. Waliniomba pia nisaidie kutoa taarifa au kumtafuta na nimuombe ili arudi jeshini maana ni aibu sana kutoroka jeshini na sasa wazazi wake wanasemwa vibaya kijijini hapa kwa kutomlea mtoto wao ktk ujasiri mpaka aona kazi ni ngumu jeshini mpaka katoroka....


NOTE:
WAKUU STORY HII INAENDELEA... Hapo chini https://www.jamiiforums.com/mahusia...wa-my-best-friend-kwa-risasi.html#post5363086
 
4. Ilipita siku,ikaja wiki,mara mwezi,kisha miezi huku tukiendelea na mausiano yetu,binti alikua akija Tabora na kisha kurudi SINGIDA,cha ajabu nilikua sipati ata hamu ya kwenda kwao ingawa alikua akiniambia twende.Nakumbuka ilitokea Operation ya kijeshi ktk nchi jirani ambayo na mimi niliunganishwa.Hii operation ilinifurahisha sana maana ilinikumbusha babangu mzazi aliwahi kuniambia kwamba sitakamilika kuitwa mwanajeshi mpaka pale ntakapoicha familia yangu na kwenda vitani.Niliwasiliana na babangu mzazi na kumpa taarifa hizo na wakaniahidi kwamba watafanya matambiko na ntarudi salama.

Pia niliwasiliana na my fiance juu ya taarifa hiyo na nikwamwambia kwamba kama atajifungua mtoto wa kiume basi ampe jina la john ili kumkumbuka my friend john....na akizaliwa demu atachagua mwenyewe jina la kumpa.

Nashukuru mungu nilienda na nikarudi salama baada ya miezi 7,na nilivyorudi niliandaa safari ya kwenda SINGIDA,nikaona nimtafute dadake ili anipe taarifa zaidi.......nilivyofika kwa shemeji yangu huyu nikaambia ameshahama na kaelekea MWANZA becouse alipata mume msukuma wa mwanza,

Niliishiwa nguvu maana niliona dalili za kumkosa mtoto na my wife to be na sijui kama alishajifungua au la ingawa muda wa kujifungua ulishapita kwa miezi5.

Lakini kwasababu alishanipa ramani ya kwao niliona sintapote,so kwa rikizo hii ya siku 30 niliyopewa inatosha kumtafuta na kukamilisha taratibu zote za ndoa.................

5.Niliandaa safari ya ukweni SINGIDA,nakumbua niliondoka na basi moja hivi nimelisahau jina lilikua nilaishia igunga,maana alivyoniambia ni Ilamba nikaangalia ramani na nikagundua kwamba nikipanda tren ntazunguka sana.Ikabidi nipitie njia ya igunga,tulifika igunga majira ya saa 12 jioni,nikaambiwa kwasababu ni msimu wa mvua mabasi ni mpaka kesho saa5-6 yale yanayotokea kanda ya ziwa,au niende sehemu moja inaitwa SHERUI pale ntapata usafiri wa malori alfajiri na ntafika ILAMBA kesho yake mapema kabla ya saa 2.Wazo hili nililiafiki na nikaanza safari ya miguu kutoka igunga mjini kwenda SHERUI kwa miguu maana hakukua na usafiri wa kutosha kipindi hicho na isitoshe hakukua na ata bodaboda.Mwanaume niliianza safari ya miguu kwenda SHERUI usiku kwa usiku,lengo ni kesho yake niwahi kumuona my love na my baby boy/girl,nilitembea kwa muda wa masaa 4 lakini ata dalili ya kufika SHERUI sikuiona,maana ilikua ni msitu mkubwa na giza na kwa mbali nilikua naona mioto ya wachoma mikaa pekee,ilivyofika mida ya saa 6 usiku nilikutana na jamaa fulani hivi 3 wamejifunika mashuka meusi tititi..........

6.Watu hawa ni jamii kama masai ila hawa niliambiwa wanaitwa "WATATURU"mbaya zaidi hatukuelewana lugha maana wao kiswahili kilikua hakipandi,haikunishughulisha sana mie akili yangu ilikua kwa mchuchuchu ukizingatia miezi9 ilishapita bila kumgegeda.......nilifika SHERUI mida ya saa 8.30 usiku na nikakuta kuna malori mengi sana yamepangana kwenye foleni kwa ajiri ya kupandisha mlima SEKENKE,fasta nilianza mchakato wa usafiri,kwa sababu nilikua nimevaa sale haikunipa shida kupata usafiri,tena bure kabisa.Saa10.30 alfajiri safari ilianza ya kupandisha SEKENKE,kwa kweli njia ilikua mbaya sana ingawa nasikia siku hizi kuna lami.Nilifika kijijini ukweni kwangu KINTINKO mida ya saa5 asubuhi hivi.Kwa sababu baba mkwe wangu alikua maarufu sana pale kijijini haikunipa taabu sana kumpata ingawa ilinichukua takribani dk40 hivi.

Tulifika nyumbani kwa mwenyeji wangu around saa6 mchana hivi.Nilikaribishwa vizuri sana pale nyumbani.
Wakati nikiwa nimekaa sebuleni nilikua nikipitisha macho huku na hiko mara macho yangu yakatua kwenye picha 1 nzuri sana ya dada akiwa amembeba mtoto mchanga,nilipoikodolea macho niligundua kwamba ni picha ya my love WITNESS akiwa amembeba mtoto mchanga................

6.Wakati wenyeji wangu wakiwa wanaangaika kuniandalia chochote na pengine wakiwa na furaha ya mkwe kuja nilitaka kuonana na my love maana sasa niloshajiridhisha vya kutosha kwamba pale ndio ukweni.Lakini sikua na papala sana maana sikujua mila zao zilivyo.......baada ya kuendelea kupepesa macho huku na huku niliiona picha nyingine ya kijana ambaye sura yake haikua ngeni sana kwangu maana anafanana sana my best nilie kua nae tangu utotoni pale mtaa ya BUHEMBA-MUSOMA,huyu jamaa alikua dhahili kabisa ni my best friend JOHN MANYAMA niliyekua nae tangu utotoni na nikaenda nae jeshini na mpaka sasa anatafutwa,tofauti ya huyu ni kwamba alikua kanenepa sana na alikua na nywele nyingi kiasi kwamba kwa mtu wa kawaida asingeweza kutambua.......

7.Yes ni kweli duniani wawili wawili,lakini kwa huyu hapana.......maana ata jina sasa ni geni kwamba eti anaitwa mr MASIGITI MAJINGE?ni katika maongezi na kijana mmoja hivi aliyeingia kunipa kampani ya kupata msosi na eti huyu jamaa ni mwalimu,nilikumbuka one day my WITNESSES aliwahi kumfananisha mtu huyo na wa kwenye picha na akaniambia kwamba yeye si askari na wote tukajiridhisha.Nikaona ngoja niendelee kudadisi juu ya huyu jamaa,akaniambia yeye ni shemeji yao kawaolea dadao na wamezaa nae mtoto mmoja wa kiume,

Baada ya kumaliza kula nilipasha shauku ya kumuona my wife na mambo sijui ni John au siye nikaamua kuyapotezea maana niliamini pia duniani ni 2x2........lakini baadae niligundua kwamba sasa ata wao walikua wanatamani kujua mimi ni nani na ninashida gani maana hawana ndg mwanajeshi na wala hawajawahi kufiria kama ipo siku watatembelewa na mwana jeshi.Hii kitu ilinishangaza sana maana nilijua fika kwamba kabla sijafika ukweni basi sura yangu ilishafika huko kitambo maana witness alishachukua picha zangu kitambo kuja kuwaonyesha,sasa why wanishangae?

Ilibidi nijitambulishe kwa jina langu maana niliona wananizingua wakati mimi nataka kuiona familia yangu.Baada ya kumwaga story nzima niliona wakibaki wakishangaana,lakini cha ajabu baada ya kuisoma picha ya sura ya mama mkwe niligundua kitu fulani hivi ingawa sikutaka kujionyesha kwanza ili nione mwisho wake...............

8.Mbona Witness kishaolewa?na aliolewa wakati ni mjamzito?na mumewe ni mwalimu anaitwa MASIGITI MAJINGE?
Ni kauli ya mama mkwe ambayo ilininyong'onyesha sana.

Nikasema ok jee naweza kuonana nae?wakasema hapana wao wanaishi singida mjini.Niliomba kujua shule anayofundisha ili kuweza kupata ukweli,cha ajabu walikataa kunitajia shule.

Nikaona hakuna shida nikaaga nikaondoka zangu nikiwaaga kwamba narudi Tabora ila wamtafute WIT wamwambie nampenda sana naomba anitafute ili tuoane na ata kama mtoto sii wangu ntamlea,mwanaume nikachapa mwendo,safari yangu haikua ya kurudi Tabora bali niliamua kwenda moja kwa moja SINGIDA mjini kumtafuta WITNESS.

Nilifika SINGIDA mjini mida ya saa5 usiku.Ki ukweli nilikua nimechoka sana lakini kwasababu ya muda ilibidi nibadili nioge kisha niingie mtaani kumsaka WITNESS.Nilikua kama chizi maana nilikua nazunguka bila mpangilio,baada ya akili kutulia niliona bora nikalale ili nifanye mchakato huo asbh.

Majira ya saa2 asbh nilikua mbele ya office za elimu ili kwanza nimpate huyo MASIGITI kisha yeye ndio atanipeleka kwa WITNESS ata kwa nguvu.......

Ktk kumbukumbu zao wakasema hana kumbukumbu na mtu huyo hapo officen kwao,niliona kazi ya kumpata mwanangu na WITNESS wangu sasa inakua ngumu,lakini namshukuru bwana mmoja jina limenitoka aliweza kunipa information ambazo kwa 100% niliweza kupata uthibitisho anapoishi WITNESS NA MUMEWE MASIGITI huku wakiwa na mtoto wa kiume anayeitwa JOHN.......

9.Saa 10.30 nilikua mlangoni kwa mr Masigiti nikiongea na dogo mmoja niliyemkuta hapo nyumbani.Aliniambia MASIGITI yuko likizo na amesafiri asbh hiyo kwenda ITIGI MANYONI kupanda tren kwa ajiri ya safari ya MWANZA maana kwao ni MWANZA,nikafatilia ratiba ya tren ili kujua inapita Tabora lini,nikapata jibu kwamba itafika tabora siku ya 3 alfajiri,nikapata matumaini na nikasema nikimpatia Tabora basi atakua amenirahisishia kazi.Mwanaume nikaanza safari ya Tabora,siku ya siku alfajiri nilikua stesheni pale mitaa ya ISEVYA Tabora nikiweka 'AMBUSH'mtego wa kumnasa Witness,saa11 alfajiri tren ikatia nanga Tabora mjini.Nakumbuka nilikua dada mmoja hivi pia alikua askari ambaye nilimuomba anisaidie kumsaka WIT wangu,tulianza kuingia behewa moja baada ya jingine,mungu si ATHUMANI punde........

10.Punde nilimuona mtu ninayemfahamu ambaye sasa niliona WITNESS nimeshampata,huyu alikua ni TT kwenye hiyo tren,nilimsogelea na kusalimiana nae na pia akanikumbuka pia kwamba tulikwaruzana miaka2 iliyopita pale maeneo ya TINDE shinyanga baada ya kutaka kunishusha kwenye tren eti kwasababu sina tiketi.Lakini baada ya kumfahamisha kuwa mm ni askari alinikubalia kisha nikampoza kwa buku.

Ni kweli kabisa nilikua sina tiketi becouse nilipofika MWANZA nikakuta tren imejaa mpaka wiki 2,kwasababu ilikua ni lazima niwahi kulipoti ilibidi nitumie nguvu kupanda.Tulipita kila behewa akinisaidia msako maana nilisha mpa intro.
Lakini sikumuona Witness wa MASIGITI,huyu bwana akaniambia nisubili tren itakayopita wiki ijayo maana ameacha abilia wengi Itigi pengine alikosa tiketi........

Nikakubaliana nae na nikaamua kurudi camp huku kichwa kikiuma juu ya huyu mtoto wa kinyiramba.Siku2 baadae nilipata barua ya WITNESS ambayo inaonyesha iliandikwa wiki 3 nyuma kwamba yeye alishajifungua mtoto wa kiume na alimpa jina la John,pia akanisisitiza kwamba nikirudi kutoka kwenye military operation nimjulishe ili aje amlete mwanangu nimuone na tufanye mipango ya ndoa.

Niliona kama naota maana kwao nimefika na nimeambiwa kishaolewa,sasa hizi habari za kwamba aniletee mtoto nimuone na tufunge ndoa vipi tena?

Nikaangalia address nikakuta ni ya SINGIDA mjini na kwamba yeye siku hizi anaishi SINGIDA mjini na kwamba alifukuzwa na wazazi wake baada ya kuwambia ni mwanajeshi wa Tabora na ni mkurya na wazazi wake wamechukizwa na kitendo cha kuzaa na mkurya tena mwanajeshi maana eti sisi watu wa MUSOMA ni katiri sana.......

11.Nilimjibu kwa barua kwamba nimesharudi na nna hamu sana ya kumuona,pia nilimpa namba ya simu ya jirani ili anitafute kwa simu as soon as possible.

Niliituma barua na nikatulia nijue kama ataijibu au la,pamoja na kwamba nilikua nimepata mawasiliano nae ya barua lakini bado niliendelea kuweka AMBUSH pale stesheni na ili ikitokea nikimuona nimdake palepale Tabora maana nilikua na uhakika kwamba alishaolewa.

Kwasababu nilishilikisha baadhi ya watu wangu nilikua na uhakika wa kumpata witness wangu na mwanangu.Nakumbuka siku moja hivi wiki 3 baadae nikiwa job alikuja jamaa mmoja hivi akajitambulisha kwamba yeye ni police na ana maongezi na mimi ya haraka sana,nilimkagua kwanza na kuthibitisha kwamba alikua mwema kwangu,kisha nikamsikiliza anachonitafutia,akaniambia yeye ni police pale stesheni ameniletea taarifa kwamba kuna mtu wangu niliyekua namtafuta yuko stesheni na anasafiri kuelekea SINGIDA usiku huo.Nilikua nimeshasaini na tayari ninasiraha mkononi kwa ajiri ya kuingia lindoni.......

Sikujari sana maana tayari mtu wangu yuko stesheni na anasafiri usiku huo na siko tayari kumuacha aondoke,nilipanga safari ya kwenda stesheni na ikapangika sawia.......

12.Wakati nikiwa najiandaa kutoka aliingia mkuu wangu na kuniletea taarifa za msiba wa babangu mzazi na kwamba nimepewa siku 3 tuu niwe job maana kuna coz nilitakiwa kwenda kuifanyia SONGEA wiki inayofuata,so natakiwa kuondoka usiku huo kuelekea airport maana kuna ndege ya jeshi inatoka DAR inaenda BUKOBA kupeleka vifaa na vya kijeshi kambini KABOYA na kwamba wangeshuka MWANZA........

Sasa wakuu ebu bashirini kabla sijaendelea jee nilienda airport kwa ajiri ya safari ya msibani kumzika my dad au nilienda stesheni kumtafuta witness wangu?

13.Damu nzito kuliko maji jamani lol,niliamua kuachana na habari za witness na badala yake nikawahi airport ili nipate rift ya dege la jeshi kwenda kijijini kwetu MUSOMA vijijini,tulishuka mwanza salama mida kama ya saa5 night hivi na moja kwa moja nikaenda mpaka stendi buzuruga kucheki usafiri wa fasta,nilipanda CHAI MAHARAGE wale wenyeji wa Kanda ya ziwa wanazikumbuka hizi gali maana zilikua zinapata sana ajari na kuuwa watu wengi,nilifika msibani nikazika na baada ya 3days nikawa nimerudi niko Tabora...nilivyofika Tabora nikajiandaa kwa safari ya songea,kabla ya kuondoka nilipeleka ujumbe kwa ndg na jirani yangu kwamba pengine witness anaweza piga simu,so kama atapiga amwambie mie nimeenda coz na ntarudi baada Ya miezi 3 na kama inawezekana amwachie mawasiliano(nur ya simu ili nikirudi kutoka coz nimtafute).......

14.Wakati nikiwa coz niliamua kupiga simu Tabora ili kujua kama Witness alishapiga simu au lah.Nikiambiwa hajapiga simu ila kuna barua yake imefika tangu wiki 3 zilizopita,nilimwambia ebu niambie anasemaje ndani ya barua?akanijibu hajaisoma,nikamwambia aifungue aisome.

Baada ya kuisoma akanipa mchapo ambao ulizidi kunipandisha hasira.

Eti kama kweli ninashida ya kumtafuta na kwamba kama bado nampenda na nnataka kumuona mwanangu basi nimtumie nauri aende kwa dadake Dar kisha akirudi ndio aje moja kwa moja Tabora,nikasema na sweti,maana alikua Ameweka no ya simu nikaamua kutwangia.Simu ilipokelewa na mwanadada fulani hivi mpaka moyo ukashituka,nikajitambulisha kisha nikaomba kuongea na mwl WITNESS.Akanijibu kwamba pale ni postal na simu na kwamba kwasababu anamjua anamfuata job kisha nipige baada ya 2hrs.......

15.Baada ya masaa2 nilikua naongea na mpenzi WIT huku tukicheka kwa furaha,lakini alinilaumu sana why nimemtelekeza na mtoto?cha ajabu eti nilisahau kila kitu na sikuweza ata kumwambia kama nilienda SINGIDA kumtafuta,nilimuomba msamaha kisha nikamuomba alieleze shida zake zooote.Alipita bajeti yake ya matumizi,safari ya dar then dar-Tabora.Kimahesabu ilibidi ni drow mshahara wa miezi mitatu ingawa bajeti nzima ilikua ni nusu ya amount ninayota ku draw.

Baada ya wiki2 nilikua stesheni nikimsubili my WITNESS aingie TABORA,punde tren iligota mara nikamuona dada mrembo sana akiwa na mtoto wa kiume akitabasamu.Alikua ni witness niliyemtafuta kwa miezi kibao baada ya kupoteana kwa miezi 11.Baada ya salamu tulichukua tax nakuanza safari ya nyumbani kwangu.Nilikua nimempaka mtoto na kwasababu alikua ni asubuhi na ni baridi nikaona sina aja ya kumuamsha mtoto aliyekuwa amelala kwa wakati huo.Tulipiga story mbili tatu lakini kichwani kwani nilikua nafikilia kitu 1 tuu,jee ni kipi hicho?I will be back........

16:Sasa niko ndani na my Witness,ni mida ya saa2 usiku baada ya kushinda siku nzima nikiwa job.Nilikua nikiwaza kitu kimoja tuu kana kwamba nimerogwa.Kwa jinsi mtoto alivyokua amenona niliona kama nachelewa kwenda kwenye ule mchezo wetu,maana hicho pekee ndio nilikua nikikiwaza maana nilikua na zaidi ya mwaka sijamgusa mwanamke maana mimi akiri yangu yote ilikua kwa Witness........

Kwanza aliandaa maji ya uvuguvugu kisha tukaenda zetu kupiga bafu,tukiwa bafuni mambo aliyonifanyia nusu nizimie.

Maana niliogeshwa kama mtoto.Mkuki ulikua wima tangu nakabidhi office kurudi nyumbani.Tulivyoingia bafuni nilipata wakati mgumu sana katika maisha yangu ya mahusiano,alinifanyia vitu ambavyo sijawahi ata kuvisikia aise lol.......

17:Baada ya kufika tuu ndani(kitandani)tayari nikaanza kuisachi channel"o"punde nikaipata na mara sebene likaanza.Nilishangaa dume zima nikitokwa na machozi bila kujitambua.Sijui huyu mtoto alikua kajifunzia wapi huu mchezo Lol.Maana akiri yote ilipotea,kwa jinsi nilivyokuwa nimempania niliapa kabisa kwamba lazima leo anikimbie,lakini badala yake mie ndie niliyeweka mpira kwapani.

Nilimuuliza vipi mbona leo uko fiti sana?
Akanijibu kwamba tangu nilivyompa nauri kwenda kwao wakati akiwa mjamzito alinitunzia mali zangu na kwamba hajawahi kuguswa na mwanaume yoyote so alikua na hamu na mimi.Nilifurahi sana na kuona kama nina bahati ya mtende kwa kupata mke mwaminifu.......

Baada ya story na sebene kuisha majira ya saa9 hivi tuliamua kupumzika maana niliona dhahili shairi anausingizi mwingi....

Tukiwa tumepumzika gafla iliniijia picha nzima ya ile safari yangu ya SINGIDA kwenda kumtafuta.Nilijaribu kuvuta hisia kama ni kweli nilisafiri au ilikua ndoto.

Baadae nikaamua kujiaminisha kwamba ilikua ndoto na maadamu tayari my love nimempata lets forget the past na tukaanza maisha na mipango ya kumpeleka kwa wazazi wangu.Na pia nilifurahi kwamba alimpa mwanangu jina nililomchagulia.......

18.Tukiwa nyumbani kwetu MUSOMA one morning my mother aliniita chemba na kuniambia story ambayo niliishngaa..kwamba hana uhakika kama yule mtoto ni wangu,akaniambia kama nataka anithibitishie basi atanithibitishia,nikamwambia no,he is my baby boy.Akaniambia nalea damu ya watu na ipo siku ntaamini mwenyewe.

Sikujari sana maana niliona labda kaanza kumchukia my wife au pengine anataka ku cancel ile ahadi ya marehemu father ya kunipa ng'ombe 25 niolee.

Nikamwambia mother ok fine kama shida ni ng'ombe basi ntatafuta mahari mwenyewe.

Cha ajabu huyu my wife wakati tukiwa home alikua hapendi kutoka,nikimuuliza anasema hawezi kuzunguka na mtoto mitaani,nikimwambia basi tumuachie bibi yake anasema hapana mwanae hawezi kumuacha na mtu mwingine,

Nilipanga tukae mwezi mzima lakini baada ya wiki moja visa vilianza,alikua usiku anapiga kelele kwamba kuna mtu anamkaba,hali hii ilinishitua sana na nikaamua kufuta likizo na kurudi Tabora ili kumuepusha my love na matatizo.

19:Tukiwa nyumbani Tabora niliendelea kumdadisi ili kujua nini hasa kilikua kinamtokea tulipokua MUSOMA?
Akasema kuna bibi mtu mzima kidogo alikua anakuja kumkaba na kweli shingoni alikua na alama za kucha.Nilimuomba msamaa wa yoye yaliyotokea tukiwa kwetu na kikamuahidi ntamfatilia huyo bibi ili nifundishe adabu.Alinikataza na akasema tumuachie mungu,nilifarijika maana niliona kabisa kwamba nina mke mwenye hekima sana,kumbe ilikua ni tofauti maana alikua ni chui aliyevaa ngozi ya kondoo.......

20:nilimuomba my wife kwamba hizo 2wks zilizobaki why tusiende SINGIDA?alinikubalia kwa sharti kwamba yeye atatangulia kwanza ili akaweke mazingira fresh kisha atanipigia simu ili niende,nikamkubalia wazo lake hilo na tukaanza mipango ya safari yake na kisha yangu.......

21:Siku moja kabla ya safari yake back to SINGIDA nilikua job akanifata kuniomba ruksa aende postal kupiga simu kwa dadake kwamba kesho anarudi nyumbani,nilimruhusu.

Lakini wakati akiondoka mie niliona ngoja pia nirudi nyumbani ili nikamwandalie baadhi ya vitu kwa ajiri ya safari.Nilifika nyumbani na baada ya kuingia ndani nilikuta card ya mtoto ya clinic,akili iliniijia niisome ili nijue mwanangu kazaliwa tar ngapi maana kwa jinsi nivyokua ----- eti sikuwahi kuuliza swali hili,nikiwa nasoma kadi hiyo nikakuta sehemu imeandikwa hivi:

Jina la mtoto John Masiti.
Jina la mama Witness.......
Jina la baba Masigiti Majinge.

Nilitokwa na jasho kana kwamba nilipewa adhabu ya kukimbia kwa miguu kutokea pale makongo jwtz mpaka bunju,asila zilinipanda mpaka nikawa na hamu ya kuua tuu,na nilipanga nimuue mama yake na mtoto kisha nijimalize mwenyewe,nilikumbuka kauli ya my mother kwa he is not my blood,sikuona faida ya maisha tena,sasa nikawa natamani ili arudi nimmalize pale pale........

Punde nikasikia hodi hodi nikasema yes sasa leo huyu malaya atajibu kesi yote.

Niliinuka kwenda kufungua mlango........

22:Nilivyofungua mlango nilikutana na sura ya huyu kimwana,nilimkamata kisawasawa na kumbamiza ukutani na kumwambia aniambie kila kitu bila kuficha maana tayari nilishabadilika.

Nilivyomuana anachelewa nilinyakua mtoto na kumlaza chini kisha nikachomoa kisu na kumtishia mamake kama asipo sema ukweli namchinja mtoto na ole wake apige kelele.Demu alimwagika A-Z,kisha nikamuuliza why umenipotezea muda?

Alikosa jibu la kunijibu nikamwambia sasa achague yeye,mwanae au mumewe mmoja wao nimuue ili kupunguza hasira zangu,alinijibu kwa upole kwamba nimsamehe yeye na mwanae na badala yake nimuue mumewe,nikamwambia afanye kila njia mumewe afike Tabora ndani ya masaa24,ilinijibu hajui cha kufanya nikamwambia ampigie simu amwambie yeye yuko Tabora amepata matatizo alipotoka dar alienda mwanza kwa dadake mwingine...mumewe yule hakua na ajizi alitafuta usafiri wa fasta
Akaja Tabora........

Kwa sababu alikuja kwa basi nilimuomba mtu aende na demu wake huyo akampokee lakini deme ajifiche akishampokea wachelewe kwa muda fulani hivi ili niweze kumuondoa demu wake ktk uso wangu maana nilikua nimemshikilia mtoto wake kama mateka.......

23:Kiukweli nilikua nimedhamilia kuua,lakini mlengwa wa kuuwawa alikua ni deme na wala sii jamaa wala mtoto.Nilimuita jamaa ili aje nimkabidhi mtoto wake na yeye aniachie demu nimmalize.

Nilipanga tuonane ndani ya uwanja wa mpira wa VITA pale jirani na shule ya secondary ya UYIA kama sikosei.

Ni kweli jamaa alifika kwa muda muafaka,wakati nikiwa nimemficha demu sehemu nyingine kwa kumtumia mateka mwanae jamaa aliingia kwenye anga zangu nje ya uwanja nilipokuwa nimesimama.

Sikuta kumwangalia usoni nilimkabidhi mtoto wake na kumwambia aondoke akamlee maana ni yatima wa mama kuanzia muda mfupi ujao.......

INAENDELEA... CHINI https://www.jamiiforums.com/mahusia...wa-my-best-friend-kwa-risasi.html#post5363231
 
NOTE: STORY HII NI YA KWELI KABISA.

Ntawathibitishia mwisho mwa story.

24:Jamaa hakuta kunielewa kirahisi namna hiyo,aliniulizo maswali mfululizo juu ya mkewe,wakati akiniuliza nilisitaajabu kusikia sauti inafana na ya my best friend John Manyama.Niligeuka kumwangalia mara 2x2. Nilijiridhisha kwamba haswa ndiye mr John Manyama mwenyewe,kwasababu yeye alikua hajanifahamu kutokana na jinsi nilivyokua nimeificha sura yangu niliamua kumwita kwa jina lake halisi la john Manyama,alishangaa maana ni miaka mingi sana hajaritumia jina hilo.Nilijitambulisha kwake kwamba mimi ni fulani,hakuamini mpaka nilipovua miwani iliyokua imeziba usoni wangu kwa sehemu kubwa.

Alitaka kujua nini kinaendelea nikamwambia usiwe na shaka na I'm very sorry for every things.

Ila naomba tumpitie shem nimemuhifadhi sehemu then twende home kwangu tukatete fresh.Tulimpitia shemeji na safari ya camp ikaanza.......

Wakuu naombeni kwa leo tuishie hapa then kesho mapema ntamalizia.

Na kwa yeyote aliyevutiwa na story na anadhani anaweza kuitengeneza kibiasha naomba tuwasiliane nae maana ni kosa kuicopy na kupast bila ruksa yangu.

Tayari mmoja wetu amekwisha tangulia mbele ya khaki,amefariki siku 3 kabla ya xmas na amefia Arusha Kijengee juu na tumezika tayari.

25: Tulifika nyumbani wote kwa pamoja huku mimi nikiwa na mawazo tele ni aina gana ya adhabu anastahili kupewa huyu malaya kwa kutuchanganya mimi na rafiki yangu,niliona hakuna adhabu itakayomfaa tofauti na kifo.

Ila kabla ya kutekeleza azimio langu nilitaka kujua kama my friend alikua na mpango wa kuendelea nae au la!

Baada ya mapumziko mafupi kwanza nilitaka Kujua kwanini aliamua kubadili jina?

Alinipa mchapo wote bila kubakiza ata kipande,kisha nikamuunga mkono kwa maamuzi yake.

Baada ya hapo alitaka kujua mkasa mzima wa mimi kuonana na WITNESS wakati alimuaga anakwenda Dar?

Nilimpa full story tangu tulipoonana na WITNESS mpaka nilivyoenda kwao kumtafuta na yeye na my baby. Pia nilimwa nilikua na rafiki yangu akiitwa John Manyama lakini amepotea ktk mazingira ya kutatanisha so nataka kumuenzi kwa kumpa mwanangu jina lake. Point hii ilimfurahisha sana na akauthamini urafiki wetu ambao ulikua zaidi ya urafiki.

Aliniambia kwamba kutokana na picha mbaya aliyotuchezea WIT nadhani hakuna aja ya kumuacha akiwa hai,mbaya zaidi aliniomba tummalize na mtoto ili tuweze kufuta kizazi chote cha huyu malaya.

Baada ya makubaliano tulipanga ni wapi tukatekelezee mauaji yetu,tulikubaliana kwamba twende msituni ambako baada ya mauaji tutawazika huko huko bila mtu kujua.

Alinipa kazi ya kutafuta pori zuri la kufanyia mauaji,nilimwambia kuna sehemu inaitwa USOKE njia ya Urambo,kule kuna msitu mnene ambao tutafanya kazi bila mtu kujua.

Tuligawana majukumu kwamba wakati mimi nafanya mauaji yeye atakua akichimba kaburi la kuwazika.

Baada ya maongezi tulikubaliana kwamba mimi niendelee kuwa na huyo mwanamke ndani ili kumwaminisha kwamba hakuna baya then yeye akalale chumba kingine.

Pamoja na kwamba nilikua ndani ya kambi na tulikua tunapanga mipango mizito namna hiyo bado sikutaka kumuamini sana my friend juu ya mpango wa kutekeleza mauaji.

Tukiwa tumelala nilimfaliji mrembo Wit kwa kumwambia kwamba yamekwisha na alichokifanya kimesaidia mm kukutana na rafiki yangu kipenzi,kwahiyo hakuna shida yoyote na sasa yeye achague angependa kuendelea na nani kati yetu?

Ingawa mm ndiye niliyekua nae kitandani kwa wakati huo huku nikimuanda kwa sebene alisema angependa kuendelea na MASIGITI maana tayari kwao wanamfahamu....hali ile ilinikera zaidi na kuona kanidhalau sana.
Lakini sikutaka kumuonyesha hasira zangu waziwazi.

Nilimwambia basi kutokana na hali hiyo naomba nipe penzi la mwisho ili nikiamka asubuhi kesho nianze kukuheshimu kama shemeji yangu na mumeo ntamwambia kwamba ulikataa kunipa mzigo maana unamuheshimu mumeo.

Demu alikubali na ndani ya dk kama 20 hivi kila mtu alikua kando ya kitanda akitweta kama mbwa wa afande kova aliyetoka kuzuia maandamano ya CHADEMA muda mfupi uliopita.

Asubuhi niliamka mapema kwa ajiri ya maandalizi.

Kwa kumtumia my friend tulimwambia ajiandae twende nje ya mji kwa ajiri ya mtoko wa wiki moja kupumzika kutokana na sekeseke lililotokea.

Nilifanya maandalizi yangu huku nikichukua tahadhari kubwa kwa my best friend maana nilikua simuamini hata kwa 40%.

Tukiwa ndani landrover kuelekea USOKE mwanaume nilikua niko full kwa lolote hata kama ni kuua watu wote tuliokua ndani ya gari.

Tulifika sehemu moja hivi inaitwa TUMBI,nikahisi kuna hatari mbele yangu,maana kuna sura 2 za watu nilihisi ni askari.

Nilijiweka tayari kwa ajiri ya kujilinda,niliishika siraha yangu kiunoni nikaona iko poa huku nikipiga hesabu nianze mimi mtifuano maana tayari nilishajiridhisha kwamba wale ni askari.

Tulifika sehemu moja inaitwa MABAMA nikaona kama nikiruhusu tuvuke eneo hilo basi kazi itakua ngumu sana kwangu.

Maana ndani ya gari kuna wanaume 3 ambao natakiwa kupambana nao,muongoni mwao mmoja ni my best na tayari alikua ni commando aliyeacha jeshi,hawa wengine nilikua siwajui kabisaa.

Nilimuamuru dereva asimamishe gari ili kama ni mtifuano uanzie hapo,ndani ya sekunde chache nilikua chini bila kujijua..................

26: Baada ya kufika chini sikuona dalili yoyote ya hatari,nilimuamuru my friend na Witness washuke maana tumeshafika.

Walikubaliana na mimi maana wao walikua wageni eneo hilo.

Ingawa tulishukia out of target nilirekebisha harakaharaka mambo ili waamini ndio eneo husika.

Tulianza kutembea kwa miguu kuelekea upande wa kusini,tulitembea kwa muda wa kama dk 50 hivi huku tukipita mashamba makubwa ya tumbaku.

Atimae tulifika sehemu iliyotulia huku kukiwa na miti mingi za zambarau zilizoiva sawia.

Niliwaomba kwa pamoja tupige camp ndogo tule matunda kisha tuendelee na safari yetu iliyokua imebakiza dk chache tuu.

Nilishajiridhisha kwamba pako salama kwa 85% na sasa ninaweza fanya lolote.

Baada ya dk chache nilimpa ishara my friend na akaenda kuandaa kaburi huku nami nikijiandaa kwa kufanya unyama,baada ya yeye kuondoka nilichomoa siraha yangu na kuiweka tayari kwa kazi..............

27:
Sasa wazo la kuwaua wote watatu liliniijia na Nilipanga kufanya mauaji yao kwa risasi na ni risasi mbili tu ndizo zilizokua ndani ya bastola.

Na ili kazi iwe rahisi inabidi nianze na my friend kipenzi,kisha Witness na yule mtoto nimwache pale pale fisi wamtafune.

Nilinyanyuka machine mkononi huku witness akinikodolea macho bila kujua kwamba ana dk zisizozidi 10 kuliona jua,nikamfuata JOHN(MASIGITI)aliyekua mbali wa mitatu kama 300 kutoka tulipokua,ili niwahi kumaliza mchezo hasira zangu zipoe,masikini nilimkuta JOHN(MASIGITI)akiwa amevua shati akitokwa na jasho jingi kwa kuchimba kaburi kwa kutumia mti aliokua ameuchonga vema kama mkuki.

Sikujari sana niliendelea kumsogelea huku yeye asijue kinachoendelea................... INAENDELEA
 
humo nilimo weka ka mkazo napatafsili hivi, binti mrembo kutoka singida usishangae hilo alilo lifanya ni kawaida yao, hata mimi lilinikutaga enzi zile, pili ukisikia demu katoke chemuchem ni hafai maana ni waswahi kupita maelezo na ni washilikina balaa yani tena kwa li mbwata ni hatari napajua ndio maana nasema hivyo maana chemuchem pamepakana na mwanza road chini kidogo shule ya Mirambo High School, yani wale watoto wa chemchem tulikua tukiwaambia tu, tunasoma mirambo wanatupa mzigo na haraka haraka wanaenda kututambulisha kwao, pale nahisi nitakua na mtoto nisie mfahamu, piliulikosea kula tuna huenda kakupa na ukimyaaa
Ni kweli kabisa mkuu maana nilikutana nae maeneo hayo hayo ya mwanza road..mkuu huyu mtoto alikua ni kifaa sana,kwanza white.
Any way ngoja niendelee na story kisha utaona tabu niliyoipata kwa kumpenda huyu mtoto.
 
chezea toto la singida mixer na unyamwezi wa sikonge? mi nilipata toto shombe shombe la kiarabu hatarrriiii mkuu huyo wako hamfikii wa kwangu, yeye alikua mixer mnyramba na mnyamwezi mwarabu tobaaaa kidogo niache shuleeee

Ni kweli kabisa mkuu maana nilikutana nae maeneo hayo hayo ya mwanza road..mkuu huyu mtoto alikua ni kifaa sana,kwanza white.
Any way ngoja niendelee na story kisha utaona tabu niliyoipata kwa kumpenda huyu mtoto.
 
chezea toto la singida mixer na unyamwezi wa sikonge? mi nilipata toto shombe shombe la kiarabu hatarrriiii mkuu huyo wako hamfikii wa kwangu, yeye alikua mixer mnyramba na mnyamwezi mwarabu tobaaaa kidogo niache shuleeee
Aha ha ha ha,mkuu mie ilibakia kidogo nikatae kwenda coz maana mtoto alikua ananiliza weweeeee!
 
Tehe!tehe!tehe!,hii story ni nzuri sana ila msimuliaji, anatumia technic za ngumi,anashtukiza ukizubaa unapewa,mara anapotea kama NINJA!chezea MJEDAA weye! Ukirudi na mimi narudi!!
 
Back
Top Bottom