Nilishindwa kulala usiku baada ya kusoma 'Sheria mpya ya Usalama wa Taifa'. Nimeumia sana kama mwananchi wa kawaida

Sheria hii inakuja nyakati ambazo kuna malalamiko kuwa usalama wa Taifa hawapo competent kwa maslahi mapana ya Taifa wana bias zaidi kulinda chama tawala.

Wengine husema ni Usalama wa CCM sio usalama wa Taifa kama watu wasemavyo ni Polisi CCM na sio Polisi Tanzania
 
Nimeona kama wasiojulikana wamewekwa rasmi kwenye mfumo wa kiutawala.

Kwanini?

Kwa sababu hakuna anayewafahamu maafisa usalama wa Taifa kwa uwazi. Wapo kwa kificho zaidi kama wasiojulikana. Hakuna anayefahamu mipaka ya maafisa wa usalama wa Taifa. Haijulikani wanaanzia wapi na kuishia wapi mipaka yao kimajukumu.

Mwekezaji mzawa ama wa kudumu anawezaje kuwekeza kwenye Nchi ambayo kuna mamlaka makubwa yasiyojulikana juu ya hatma yake kibiashara ama kimaisha ama uhai wake? Ni ngumu sana.

Wakuu, nimeogopa hili Taifa kuliko kawaida. Ni Taifa langu la kuzaliwa. Lakini siwezi tena kujivunia. Naogopa. Nadhani, busara ni kufanya utaratibu wa kuhamia Burundi, kule huenda kuna unafuu zaidi kuliko Tanzania.

Hawa huwezi kukabiliana nao kwa lolote lile. Utahatarisha maisha yako bila sababu. Wana mamlaka makubwa kuzidi hata ya Rais mwenyewe. Watakufanya lolote lile watakalo na huna la kuwafanya. Yaani, kitakachokuokoa ukijichanganya ni Mwenyenzi Mungu pekee ama huruma za tu za kibinadamu na si vinginevyo.

Unaweza tena kugombania nao demu? Thubutu.

Unaweza tena kujimbwafai ukiwa bar ukisema hii ni nchi yetu wote, usinitishe? Thubutu.

Unaweza tena kubishana Yanga na Simba kijiweni? Thubutu.

Unaweza tena kubishana ishu za Chadema na CCM kijiweni? Thubutu.

Nikiwa kama kiongozi wa Umma, kwa mfano: Kwa nini nisihakikishe mwanangu anaingia usalama wa Taifa ili apate kinga ya kudumu?

Hata hivyo, inasemekana mtaani waliojaa usalama wa Taifa ni watoto wa wakubwa. Inasemekana.

Je, huenda wakubwa na familia zao wameamua kujiwekea kinga za kudumu kwenye Taifa hili? Mungu anayajua. Itakubidi, uishi kwa kujikunyata maana hujui nani ni nani na anatekeleza majukumu yapi ya usalama wa Taifa.

Pamoja na hayo, kama Baraza la Mawaziri wameona sheria hiyo ipo kamili basi tena na iwe kama watakavyo. Kila mwananchi aangalie namna ya kujihami.

Huenda ni hofu yangu kwa kuwa sijaelewa vizuri sheria yenyewe. Kama hivyo, basi na uzi huu uondolewe isilete taharuki kwa wengine wasioelewa kama mimi.

"Unapowekewa kinga ya kutoshitakiwa ni kama vile umeambiwa fanya makosa kwa kadri uwezavyo ili mradi unafanya kwenye line ya majukumu yako kikazi. Ni kama vile umeondolewa umakini wako kazini........yaani ni sawa na kama umeambiwa huna sababu ya kuwa makini kazini kwako kwa sababu hata ukikosea hakuna kitu utafanywa maana ni makosa kazini".

Eeehhh Mungu Baba ingilia kati Taifa hili.

Naomba kuwasilisha!

Pia soma: Muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaoifanya iwe chini ya usimamizi wa Rais watua Bungeni
Sheria mpya ya Usalama wa Taifa', Kwanini Wabunge wapishe kama haifai?
Waikatae tu
 
Na hiyo ndiyo democrasia yetu 😅😅😅
 
Mada zingine bora nikae kimya tu kuliko nijifanye mjuaji kumbe sijui sheria wala lolote juu ya usalama wa taifa hili.
Wajuzi/wajuvi tuleteeni ufafanuzi tujifunze.
 
Kwa hiyo nisifanye mambo yangu ya msingi kisa nawaogopa wasioogopeka
Ntakutanana nao wapi kwanza

Halafu kama wameajiri watoto wa vigogo au wakubwa unafikiri watakuja kukaa kwenye local bar kusikiliza mlevi anashangilia badala awe kwenye kumbi zenye hadhi huku akijirusha au hata hapa karibu Paris tu

Hakuna taharuki itakayotupata ila ni mauza uza yako tu Mkuu
Ishi maisha ya furaha bila kufuatilia ya watu
 
Mbona nakumbuka huwa inasemwa kuwa “ hakuna mtu aliye juu ya sheria” ?

Au maana yake ni nini?
 
Kuna mamlaka ya kidunia ila Mamla ya Mbinguni ni kubwa sana ,ukilijua hili , huwezi test mitambo ,

Shida ni pale wale katika mamlaka ya kidunia hushindwa elewa siri hii wakiamini katika watumishi wa kidunia wa dini mbalimbali kwamba ndo uwakilishi halisi wa mamlaka ya mbigu,

Amini na wambieni, wakapitishe tu ipo siku watajua hawajui, washindwe leta pia katiba mpya watajua hawajui,na imekua
Wengi wanajidanganya kwamba kwenye Siasa hakuna masuala ya Mungu ! Yaani hapo Mungu hagusi !
 
Back
Top Bottom