"Nilirudisha Bastola mara baada ya kushindwa masharti ya Umiliki wake"...Tunda man


Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,097
Likes
389
Points
180
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,097 389 180


Msanii wa kundi la Tip Top Connection Khalid Ramadhan aka Tunda Man, alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanamiliki silaha za moto (bastola), kitu kilichofahamika na kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari mapema mwaka huu.
Tunda amesema kwa sasa hamiliki tena bastola, sababu aliamua kuisalimisha silaha hiyo aliyokuwa anamiliki kutokana na masharti mengi ya kuimiliki.


“Mimi imenishinda mpaka nimerudisha, Kwasababu watu wengi walikuwa wanajua mimi nilikua na bunduki halafu maneno yakawa mengi”. Alisema Tunda leo katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Tunda amesema kati ya masharti yaliyomshinda ni pamoja na aina ya mavazi anayotakiwa kuyavaa mtu anayeimiliki .


“Kuna mavazi unatakiwa uvae kidogo, mavazi ya kipapaa yale, sometimes unatakiwa uwe nayo muda wote, kuna vitu vingi…watu wasijue kwahiyo watu washajua watu kibao kuwa mimi nina ile, afu kuna watu wanazitafuta zile ili wafanyie mambo yao”. Alimaliza.


Mwezi wa pili mwaka huu gazeti la Ijumaa liliandika habari isemayo ‘SOO LA BASTOLA, TUNDA MAN AKIONA CHA MOTO’.


Hiki ndicho kilichoandikwa katika gazeti hilo:


‘TABIA ya baadhi ya mastaa kuonyeshaonyesha bastola hadharani kimemtokea puani ‘memba’ wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’ baada ya hivi karibuni kuitwa na jeshi la polisi na kuhenyeshwa.


Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Tunda Man alisema makala iliyotoka kwenye gazeti ndugu na hili la Ijumaa Wikienda ikieleza jinsi baadhi ya wasanii wanavyozianika silaha kiholela imemfanya akione cha moto kwani wakati akizungumza na mwandishi wetu alikuwa Kituo cha Polisi cha Kati (Central) akihojiwa.


“Kwanza naomba nikwambie kuwa hakuna kitu ambacho kimenikosesha amani leo (Jumatatu) kama hii habari yako uliyoandika kwenye gazeti, hivi ninavyoongea na wewe niko ‘sentro’ nikihojiwa, kiukweli sina amani,” alisema Tunda Man.


Hivi karibuni msanii wa muziki, Aboubakar Chende ‘Dogo Janja’ alinaswa akiwa na bastola na alipoulizwa ni ya nani alidai ni ya Tunda Man hivyo kumpa msala mwenzake’.
 
FYATU

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Messages
5,268
Likes
3,455
Points
280
FYATU

FYATU

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2011
5,268 3,455 280

Wawajibishwe wale wote waliohusika kufanikisha kwa huyu bwana kuipata hiyo bastola na sio ujinga wa kusubiri matukio ndio ionekana makosa yalifanyika......tunahitaji wasimamizi makini WATAKAOZUIA na SIO KUSUBIRI KUPONYA.

Kesho mtampa bastola dudubaya alafu mtasubiri airudishe.......

......SHAME ON YOU..........

 
white girl

white girl

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2013
Messages
1,374
Likes
17
Points
0
Age
25
white girl

white girl

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2013
1,374 17 0
Atafute pesa ndio habari ya mjin sio kututanganzia bastola,maneno tumechoka
 

Forum statistics

Threads 1,252,211
Members 482,048
Posts 29,800,630