Niliposema kwa shida na raha ,Nilimaanisha.

Niliposema kwa shida na raha ,Nilimaanisha.

Suprise

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2012
Posts
2,696
Reaction score
1,063
Habari wana MMU,
Nimesikia na kushuhudia mengi na kupokea ushauri juu ya kuyumba kwa ndoa yangu lakini napenda kukiri kua wengi wamekua wakinikatisha tama na kunitaka nijiengue .hivyo naombeni msaada wa mawazo utakaonifanya niirudishe ndoa yangu na si kuivunja,
Nna miaka tisa na mume wangu kipenzi, tumebahatika kupata watoto 2, miaka 6 ilikua ya amani na pendo ndani ya nyumba, mume wangu alinionyesha upendo wote niliokua nautaraji toka kwake.
Hali ilikua mbaya mwanzoni mwa mwaka 2011, ambapo mume wangu alianza kunionyesha vitendo vya tofauti , hakua msikivu tena, anachelewa kurudi home , baada ya muda nilicikia na kuthibitisha haya;
1. Ni kweli kua ana nyumba ndogo kimara
2. Ni kweli kua ana uhusiano usio rasmi na mfanyakazi mwenzie
3. Ni kweli kua safari za kikazi zimeongezeka maradufu
4. Ni kweli kua hana mda na familia yake,
5. Ni kweli kua hata haki ya ndoa inasuasua na mpaka nilazimishe.

Vikao vya familia na wasimamizi wa ndoa vimefanyika viwili akakiri na kusema atavunja mahusiano ya nje , na hii ilionyesha mafanikio kidogo kwa mwaka jana alijirudi na inasemekana ameachana na nyumba ndogo hiyo ya kimara,

Kilichonisukuma kuandika ni kua amebadilika tena na nahisi ameanzisha makoloni mapya ingawa haya cjayahakikisha,amekua ni mtu mkorofi halali ndani, akirudi mda anaotaka,

Kuhusu matumizi ya nyumbani na mengineyo hana matatizo anaprovide inavyotakikana,

Naumia , natamani miaka 6 ya mwanzoni ya upendo irudi tena, hana sababu aliyowahi kuitoa zaidi ya kupitiwa na shetani,

Wengi wamenishauri kuivunja ndoa lakini moyo wangu bado upo kwake na nahitaji kiapo changu kwake kiwe cha milele, Hivyo naombeni ushauri wa kuirudisha ndoa yangu na c kuivunja.
 
^^
Tuliza akili ukumbuke, je kabla ya ndoa alikuwa ni mtu wa aina gani? Je ulimkubali ukitegemea kumbadili tabia yake? Kama alikuwa si mhuni je wewe uliteleza wapi kiasi cha yeye kuwa alivyo sasa! Unaweza kuiapia nafsi yako mwenyewe kuwa hukuwahi kumsaliti pia? Ukipata majibu utapata njia ya kurudisha ndoa na unyumba uliopotea.
Epuka kujipa majibu mazuri yanayokufurahisha nafsi yako.
^^
 
Pole sana dada yangu,.

Bila shaka MUNGU pekee ndiye aliyekupa ujasiri wa kuyavumilia hayo yote ya mumeo,.

Endelea kumtegemea MUNGU daima!!
 
Ni wachache wenye moyo wa uvumilivu kwa hayo unyopitia.. pole sana.....ngoja waje, watakuambia zadi
 
Basi kama kiapo ni cha muhimu kiasi hicho, kumbatia kiapo chako achana na amaumivu ya moyo.

Kumbuka 'asiyefunzwa na mamaye, atafunzwa na babaye'. Naona wewe unataka kuwa ndio mama na baba wa mmeo.
 
hapa nikitoa ushauri wa kujenga nitakuwa nakudanganya............

ila wewe endelea tu kuvumilia huku ukiomba mungu , ni upepo tu utapita...........

mnaweza kwenda vacation mwisho wa mwaka kama uwezo unaruhusu.........
 
Kuna wakati wanawake muache kujifanya victims na kulalamika kusiko kwisha, fanya maamuzi magumu once and for all.

Kama mmeo na kiapo ni cha muhimu hivyo, na tabia zake ziko wazi hadharani keshajipambanua yeye na nyumba ndogo ni kama mgonjwa na uji, hadi leo unalalama nini?

Kwa miaka 3 mizima umeshindwa kufanya maamuzi, sie ndani ya hiki kisredi tutakufanya kweli njano uione nyekundu?

Mie naona unatuchosha tu. Kama vipi vunja ndoa kama huwezi tulia na mmeo. Unaweza opt kujilipa kimya kimya ama kuokoka and blame all to the devil.

Once a cheater . . .
 
Upepo wa miaka mi3 ni upi huo? Hata mansoon wind zilidumu kwa miezi tu

hapa nikitoa ushauri wa kujenga nitakuwa nakudanganya............

ila wewe endelea tu kuvumilia huku ukiomba mungu , ni upepo tu utapita...........

mnaweza kwenda vacation mwisho wa mwaka kama uwezo unaruhusu.........
 
Pole sana na hongera kwa ujasiri wa kutambua nafasi ya mwenzi wako. Naomba sana ujaribu kuweka ukarib zaidi kwa mmeo na muda mwingi jaribu kuwa nae hasa baada ya kazi kwa kuanza kumtoa out au kuwa nae bar za karibu na nyumban. Waweza kaa nae kwa muda ukamwacha ukarud home na siku zingine kaa nae hadi mrudi wote. Na usionyeshe kukerwa kwa jambo lolote utakaloliona mkiwa nae. Siku za weekend jaribu kumshawishi make wote au mshinde pamoja ukibeba majukumu ya nyumban. Usimzuie kutoka japo mshawishi mle nae chakula na siku zingine unamuomba kumtoa baada ya chakula. Usichoke kuomba tendo hata kama itaonyesha usumbufu kwae wewe usiikereke
 
jamani Kongosho, tatizo moyo, nampenda , nipo tayari kuendelea kusubiri hiyo monsun upepo
 
Najitahidi ndugu na ctachoka, thanx, nachompendea ni kua anajua anachokifanya sometime ukikaa nae anaongea kama mtu
 
dada pole sana! mimi kinachonipa wasiwasi hapa ni suala Zima la MARADHI. maana kama mumeo hajatulia ni malaya, mi nafikiri tumia pia na akili zako kujua uko salama kiasi gani kwa mumeo huyo, na hatma ya watoto wenu.
 
Je, tangu ugundue kuwa mwenzi wako ana kimada unatumia kinga mnapofanya tendo la ndoa? Yote tisa, afya yako na wanao ndio kitu nambari one. Kapime na ukikuta uko salama,usikubali akurubuni ukashiriki tendo la kujamihiana pasipo kondomuuuuu.
 
Pole shosti lakini jee kuna jambo lolote ulimkwaza? au hiyo nyumba ndogo ulikanae chini kumuliza sababu kwanini akafanya hayo au amebadilika tuu bila sababu? wewe ni binadamu inawezakua unamapungufu yako zidi kumstahmilia na jaribu kuongea nae kwenye wakatu muafaka,zidi kumuomba mungu akupunguzie mitihani kama hiyo kwani mume anauma hasa
anapokujibu maneno mabaya na ukahakikisha kua yuko mwenzio,mungu akuzidishie moyo huo waustahmilivu mie siwezi
mwenzangu yangenishinda zamani sana.. inshallah mungu atampa moyo wa imani arudi na mfurahie ndoa yenu kuliko mwanzo...
 
tafuta kidumu na wewe uone utakavyoishi kwa amani usije ukajifia kwa presha na kuacha watoto na ndugu wanaokutegemea
 
tafuta kidumu na wewe uone utakavyoishi kwa amani usije ukajifia kwa presha na kuacha watoto na ndugu wanaokutegemea

asante kwa ushauri dada yangu ila ntatafuta upendo ukiisha yakibaki mazoea
 
hapa nikitoa ushauri wa kujenga nitakuwa nakudanganya............

ila wewe endelea tu kuvumilia huku ukiomba mungu , ni upepo tu utapita...........

mnaweza kwenda vacation mwisho wa mwaka kama uwezo unaruhusu.........

thanx ndugu for positivity
 
Huyo baada ya kuonja nje kagundua hauna utamu kunako bedi!
...
Kwa ushauri if ameanza kukucompete na hao wa nje, itabidi ujikaze na kuhakikisha ukimpa mchezo unampa kiukweli ie kwa ujuzi! Zungusha buno! Jaribu kua mbunifu!
For sure ke wengi mnakua na mautundu mwanzoni tu, soon after 2 yrs ktk ndoa, mnakua MAGOGOOOO!
Mme akijaribu nje siku 1 tu ndio anatekwa mzima mzima!
Na uhakika ukizidisha mautundu hata akitoka na kukuta wewe ni hodari zaidi ya hao, atatulia tu! Nani anatafuta maradhi ya bure wakati anaridhishwa?
...
Nadhani nimesoumeka hapa!
 
pole sana dada muombe Mungu aliyewaunganisha atawapa amani kama mwanzoni..ndoa lazima iwe na changamoto
 
Basi usilalame na kuona unaonewa, subiri ukiwa na furaha maana ni maamuzi yako mumsubiri.

jamani Kongosho, tatizo moyo, nampenda , nipo tayari kuendelea kusubiri hiyo monsun upepo
 
Back
Top Bottom