Niliposema kabla ya Kombe la Dunia kuanza kuwa sishabikii timu yoyote ile ya Afrika nilikuwa namaanisha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,910
109,663
Kama akili tu za kuliendeleza kimaendeleo bara letu la Afrika kwa utajiri wa rasilimali tulizopewa na Mwenyezi Mungu tumeshindwa je, huku katika soka (mpira wa miguu) na hasa katika michuano ya Kombe la Dunia ndiyo tuweze kutoboa/kufanikiwa?

Tayari Tunisia, Ghana na muda mfupi Cameroon wameshayaaga mashindano na hata hawa wawili waliobahatisha kupenya katika last 16 Morocco na Senegal mwisho wao ni mechi zao zijazo nao watatolewa na kurejea zao bara jeusi kuendelea na maisha mengine na tuliyoyazoea.

Kama kawaida yangu GENTAMYCINE huwa sipendi vibovu vibovu na timu zangu nilizozichagua tokea awali, japo kimiujiza moja wapo imenishangaza ni Argentina, Germany, France, Spain na Portugal.

Siipendi na kamwe sitokuja kuishangilia Brazil kwakuwa wanavaa jezi zenye rangi mbaya na nisiyoipenda hata nikiwa hapa Tanzania mitaa ya Twiga na Jangwani.
 
Sasa mambo yako ya Simba na Yanga unayapeleka mpaka WC, Brazil wanavaa rangi za bendera ya nchi yao acha sasa kula ndizi kisa ni ya njano.
 
Umezingua hapo mwisho tu..,
 
Lazima tuende na takwimu. Timu 5 kutoka Africa zimeingia timu mbili. Je huko Asia, Europe, American waliingiza timu ngapi na kwenye 16 Bora wameingiza timu ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…