Nilipompelekea IGP Mangu majina ya wauzaji wa madawa ya kulevya mezani kwake

shukran A.Ngonyani IGP anayo majina mengine amepelekewa na mojawapo ni jina lako. inaelekea wewe na mbia wako mmedhulumiana sasa umeamua kumchoma. umeitwa polisi ili ukatoe ushirikiano unakwepa
Mwezi Novemba mwaka 2013 hadi February 2014, nilikuwa jijini Dar Es Salaam ktk mihangaiko yangu ya maisha.

Lakini nikaona si vyema nikae bure, wakati ule suala la watanzania wenzetu kukamatwa ktk viwanja mbalimbali vya ndege duniani wakiwa wanavusha madawa ya kulevya likiwa "hot". Nikaamua kulifuatilia.

Nilifanya uchunguzi binafsi jijini Dar Es Salaam na kujiridhisha kuwa wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya walikuwa wanajulikana bayana mitaani, nikajiuliza; je ni kweli jeshi la polisi halioni watu hawa? Kama vigogo wanaohusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya hawapatikani kwa nini isideal na hawa retailer wanaouza madawa ya kulevya mitaani huku wakijulikana?

Nikachunguza na kupita kufanyia utafiti maeneo kadhaa jijini Dar ambako wanauza madawa ya kulevya tena ilipobidi hadi kukutana na wauzaji ili tu kujiridhisha. Kisha nikafanya maamuzi mazito.

Wakati nimesharudi niko Tanga nikamwandikia barua pepe IGP nikimpatia majina na maeneo ya kijiografia hadi nyumba ambazo madawa ya kulevya yanauzwa. Nikaona ni busara pia nika CC; barua ile kwa maRPC wote mikoa yote, na maofisa wote wa jeshi la polisi makao makuu. Baada ya mwezi kupita bila majibu ya mrejesho nikatuma barua kwa njia ya posta(hard copy) kwenda kwa IGP nikimweleza kwa urefu maeneo na majina ya wauzaji wa madawa ya kulevya ktk maeneo kadhaa jijini Dar Es Salaam. Pia nikampigia simu kwenye namba yake 0754 785 557(IGP Mangu) nikimweleza nimemtumia barua pepe na barua ya nakala ngumu kuja mezani kwake.

Bahati mbaya naamini taarifa ile haikufanyiwa kazi, kwani kulikuwa maeneo ambayo nilitakiwa nitoe ushirikiano na nilikuwa tayari kufanya hivyo muda wowote ikibidi hata kwa gharama zangu, nilimweleza hivyo.

Najua ni hatari kwangu ktk suala hili lakini nilikuwa tayari kufa kwa ajili ya taifa langu, kumwaga damu kwa ajili ya kuleta ustawi wa vijana wenzangu wanaoharibika kwa madawa ya kulevya. Nilidhamiria kumwaga damu yangu ili iwe wino wa kielelezo cha upigaji vita wa madawa ya kulevya.

Kitendo kile cha jeshi la polisi kupuuza taarifa nyeti kama hizi ziliniacha mdomo wazi hadi leo na sijajua nini kusudi lake.
Je linawaogopa drug dealers? Lina maslahi binafsi(personal interest)? Jeshi lote hawakuziona barua zangu zaidi ya 48?

Bado natafakari!!

Shukrani A. Ngonyani,

February 10, 2015

Tanga,

ngonyani@naij.com/Sirngonyani@gmail.com

+255784 37 97 99.


UPDATES.......
Kuna wachangiaji wamedai niweke ushahidi wa vielelezo/barua nilizotuma ili waweze amini.

Nadhani na nafikiri tena upya kuweka hapa. Huenda huu ukawa mtego tu wa wahusika wajue kama majina yao yamo kwenye orodha au la.

Pia ifahamike kuwa mimi ni verified member hapa, natumia jina langu halisi sio kama wao na fake ID zao, pia nimeweka physical adress yangu na mawasiliano yangu hata namba ya simu, nimeweka original passport size yangu kama avatar, mwenye mashaka nami mimi nitamwekea mara tatu kwake.
 
Pole sana Ndugu yangu. Wakati mwingine jitahidi sana ku-read between the lines!!! Lukuvi alisema kuwa Bunge likiwataja wauza Unga hakuna mbunge atakaebakia madarakani!!! Pinda aliwahi kunukuliwa kwa kusema kuwa Wauza Unga wananguvu sana na wako juu ya Sheria!!! JK aliwahi kusema List ya Wauza Unga anayo... Hivi Unafahamu kuwa Fedha za kugharamia matumizi ya CCM inatokana na Biashara ya Sembe?.... Unafahamu kuwa Tanzania inatumiwa na mataifa ya magharibi kama eneo la kupitishia mzigo kwenda CHINA? Unafahamu kuwa Target ni Vijana wa China? ... Western wanambinu nyingi ya kuharibu mataifa threatens kwao... Sirahisi sana vita hivi Mkuu ..

kuna kitu nimekipata kutoka hapa
 
.. RockSpider vita havina mwisho hivi,CIA wenyewe walikuwa kwenye payroll za ma cartels wa Mexico na colombia
 
Last edited by a moderator:
...ingekuwa chadema apo sawa tungechukua hatua, sasa unareta habari za dawa za kurevya ? kwani zinaathari gani kwenye wagombea Wa richama retu tawara ? yaache yawe marevi yasipigie kura chadema. turiyanyima elimu ili tuyatawale yakajifanya utandawazi umewasaidia kufungua akili sasa tunayapa unga iri yarewerewe tu yasipige kura....
 
Mbona kesha sema amejiandaa kufa ili damu yake iwe wino...
Muwe mnasoma mada na kuielewa kabla ya kujadili...

Tafakari...

Nimesoma na nimeelewa in full. Maana yangu halisi ameshindwa nini kuanika humu ndani jamvini baada ya kuona huko wamemkaukia? Kama amejiandaa atuwekee nakala ya hiyo barua humu na akanunue jeneza lake mwenyewe.
 
Mkuu hapa ni kuitoa CCM madarakani ikiwezekana! Hawa ndio wafadhili wakuu wa sembe na dona, halafu issue ikibumbuluka wadau wa sembe na dona eti wanajipeleka wenyewe Polisi wachunguzwe!?!? We uliona wapi jambazi muuaji anajipeleka mwenyewe kwenye vyombo vya dola ili achunguzwe!? Hii ni sawa na kujichunguza halafu utegemee matokeo tofauti!
kuna mmoja yule alikamatwa magomen sijui anaitwa chonji, ajabu alikuwa hana hata pingu na alikuwa anachekelea kwenye defenda ya polisi!
 
Fuatilia kwa umakini mkubwa, drug lords wa mexico walikuwa kwenye payroll ya CIA ... CIA ndo wenye kumiliki plantations za kule Colombia, Pakistan na Afghanistan ..

.. RockSpider vita havina mwisho hivi,CIA wenyewe walikuwa kwenye payroll za ma cartels wa Mexico na colombia
 
Ndugu yangu Nakembetwa Ulichokisema ni sahihi kabisa. Tarehe 04/02/2014, Ilikamatwa Meli ikiwa na shehena nzito ya madawa ya kulevya. Meli hiyo ilikuwa ikiongozwa na Captain MPakstan, Na crew wenginge kutoka Ira. Chakushangaza, baadhi ya viroba vilikuwa vimeandikwa Kabisa coffee for the President of Tanzania. Pamoja na kwamba kukamatwa kwa meli hiyo kulihusisha vyombo vyote vya Usalama vya njini, pamoja na Interpol, na baadhi ya majasusi kutoka ubalozi wa Marekani. Lakini hakuna cha Case. Baadhi ya viroba vilipelekwa kwa mkemia mkuu ili kuthibitisha lakini taarifa zilizopatikana ni kwamba imeonekana hayakuwa madawa ya kulevya. Kwa kifupi ni kwamba huyo Dr. wenu ndiye huko kwenye mtandao wa wauzaji wakuu wa madawa ya kulevya. Kwa hiyo jamani acheni kuangaika. Huo mtandao ni mkubwa na hautuikisiki, Unaweza kupoteza maisha bure. Namshauri ndugu yangu Ngonyani. Dunia ya leo uzalendo haupo kabisa achana kujiingiza kwenye hatari ya kupoteza maisha, utaacha familia yako inaangaika bure. Angalia hii link ndo utajua kuwa mtandao wa walanguzi wa madawa ya kulevya.

https://www.youtube.com/watch?v=e7-lnu_PEJQ

daah hii nchi kifupi hatuna rais zaidi ya mpiga dili tu pale magogoni!
 
Ndugu yangu Nakembetwa Ulichokisema ni sahihi kabisa. Tarehe 04/02/2014, Ilikamatwa Meli ikiwa na shehena nzito ya madawa ya kulevya. Meli hiyo ilikuwa ikiongozwa na Captain MPakstan, Na crew wenginge kutoka Ira. Chakushangaza, baadhi ya viroba vilikuwa vimeandikwa Kabisa coffee for the President of Tanzania. Pamoja na kwamba kukamatwa kwa meli hiyo kulihusisha vyombo vyote vya Usalama vya njini, pamoja na Interpol, na baadhi ya majasusi kutoka ubalozi wa Marekani. Lakini hakuna cha Case. Baadhi ya viroba vilipelekwa kwa mkemia mkuu ili kuthibitisha lakini taarifa zilizopatikana ni kwamba imeonekana hayakuwa madawa ya kulevya. Kwa kifupi ni kwamba huyo Dr. wenu ndiye huko kwenye mtandao wa wauzaji wakuu wa madawa ya kulevya. Kwa hiyo jamani acheni kuangaika. Huo mtandao ni mkubwa na hautuikisiki, Unaweza kupoteza maisha bure. Namshauri ndugu yangu Ngonyani. Dunia ya leo uzalendo haupo kabisa achana kujiingiza kwenye hatari ya kupoteza maisha, utaacha familia yako inaangaika bure. Angalia hii link ndo utajua kuwa mtandao wa walanguzi wa madawa ya kulevya.

https://www.youtube.com/watch?v=e7-lnu_PEJQ

Taarifa kuwa Dr anafanya biashara ya sembe mm nilikuwa nazo kabla hata hajaingia madarakani.

Kwa sasa naona amemuachia kijana wake aendeleze.s
 
Mtumie Majina hayo Obama Yupo Marekani hapa Bongo umeula wa Chuya...!
 
Hakika ni tendo lakijasiri. Sina zaid yakukupa pongezi na Mungu akutangulie hakika.

People humu zinabeza na kuzodoa ujinga tu. Hili suala ni vyema uwage unaliona kwa walioathilika tu.

Inasikitisha mno ndugu zanguni.
 
Mkuu nakupa pongezi kwa moyo wa ujasiri,mtaa ninaokaa kuna mama anafahamika kwa kuuza huo munaoita sembe,huku maeneo ya ukonga......watuamiaji wa hiyo bidhaa wanapita nje ya Nyumba yangu Ili kufika huko mashine wanaposaga huo Unga,siku moja nikamuambia Jamaa yangu ni askari ffu kuwa Mkuu vp jirani pale kuna biashara haramu inaendelea vp mbona sioni mukifanya lolote......Jamaa akanijibu yule mama Kila wiki kuna fungu anampelekea mkubwa,nilipojaribu kuhoji mkubwa gani Jamaa akanijibu kijana Achana na hayo mambo ww kaa na familia yako mfanye yenu hii Nchi inawenyewe...... Nikachoka.

Duuu!! Jamani,jamani,jamani nchi yangu Tanzania..
 
Sidhani kama usalama wa taifa wanashughulika na habari za unga labda useme yule bwana wanamuita Nzowa nadhani na kikosi chake.

Nini maana ya usalama wa taifa? unga siyo usalama wa taifa? usalama wa taifa wanashughurukia mambo yote yanayoweza kusababisha usalama wa taifa uwe hatarini? kwa kifupi usalama wa taifa wapo kila sehemu? husiadia taaisisi nyingine kufanya kazi, wanaweza wasijihusishe na kukamata lkn wanatoa taarifa muhimu ikulu.

OK tuache usalama wa taifa tuna taasisi mbili moja inasimamiwa na huyo Nzowa na nyingine inasimamiwa na kamishina shekiondo. zote mbili zimeshindwa?
 
Mkuu achana na watoto hawa,ukiweka data hapa wakajijua watakuua,chifupa yuko wap?mtaandao wa wauzaj wa madawa ni mkubwa sana,karbu kila idara ya serikal inahusika kwa kuptia rushwa ,kuna watu wamepata vyeo nyeti il kuwatetea wasambazaji,pgana vitana kimya kimya mkuu
 
Back
Top Bottom