floow
JF-Expert Member
- Mar 20, 2017
- 411
- 858
Mwaka jana ilikua majira ya asubuhi, nilienda hospital baada ya kujiskia siko sawa kiafya, sikua mgonjwa sana ila niliamua niende nipime afya yangu..
Nilifika hospitali na moja kwa moja nikaonana na dokta, akanichukua kipimo cha malaria pamoja na tayfod..
Baada ya kunichukua vipimo hivyo akaniambia nimsubiri nje nisubiri majibu itachukua dk 30 kusubir majibu.
Ilinibidi nikakae nje ili kusubiri majibu ya daktari, nikiwa nje nasubiri majibu huku nikiperuzi na smartphone yangu ghafla ikaja gari na kupaki karibu na Mimi.
Walitoka vijana wawil mwanamke na mwanaume (rika yangu) kisha wakamtoa mama yao aliyekua akitetemeka mwili mzima huku akilia kwa maumivu makali anayoyapata
Walimkalisha karibu na Mimi, yule mama aliendelea kulia huku akitetemeka mwili mzima ,nilimwonea huruma sana.
Haikupita dk 1 akanigeukia na kunitazama kisha akaniambia "Kijana naomba uniombee kwa dini yoyote ile" naumia sana kijana naomba uniombee, aliongea huku akitokwa na machozi..
Ulikua ni mtihani mkubwa kwangu coz nilikua nina miaka 7 sijakanyaga kanisani. Pia toka nizaliwe sikuwah kufanya maombi sehemu yenye watu wengi zaidi ya kufanyia maombi nikiwa chumbani peke yangu.
Alirudia tena kwa Mara ya 3 "kijana naomba uniombee, nitakufa" niliwaangalia watoto wake walikua ni wenye kunitazama huku wakibubujikwa na machozi..
Sikujua nilitoa wapi ujasiri ila nikajikuta nimesimama na kumshika kichwani yule mama kisha nikaanza kufanya maombi. Nilijikuta natumia sauti kubwa kufanya maombi jambo ambalo toka nizaliwe sikuwahi kufanikiwa kulifanya.
Nilipomaliza kumuombea yule mama watoto wake walinishukuru pia mama Mgonjwa alinishukuru, na wakaingia ndani kuonana na daktari. ..
Uamuzi niliochukua nikaamua niondoke bila hata ya kusubiri majibu ya daktari. Nilijifikiria sana kwanini yule Mgonjwa alinipoint mimi moja kwa moja lakini sikupata jibu.
Hili tukio limebaki kama kumbukumbu kwenye maisha yangu.