Nilipigwa na kufukuzwa Msibani

Nilipigwa na kufukuzwa Msibani

Mwaka fulani kijiji kulitokea msiba wa mzee mmoja hivi mkubwa na aliyekuwa na mali nyingi hasa mifugo, nyumba na viwanja. Sasa vijana tukaitwa siku moja kabla ya msiba ili tujiandae na tuwe tayari kwa lolote, tukapewa majukumu ya kuhakikisha usafi umefanyika mazingira yote na maji yapo ya kutosha baada ya hapo tukarudi nyumbani kukaa na kusubiri yule mzee afe.

Majira ya saa 11 asubuhi akaja kiongozi wa vijana nyumbani akanigongea na kusema msiba tayari twendeni, basi tukaanza kukusanyika ile timu ya vijana na kweli tukakuta yule mzee kafariki tukaanza kazi zetu kila mmoja na majukumu yake.

Walichinja ng'ombe watatu siku hiyo na mziki uliletwa pale mambo yote yakawa yanaenda vizuri na watu wakaanza kula, sasa wakati wanagawa chakula akaja kijana mmoja na bakuli ambalo halikuwa na nyama za kutosha nikiwa naongea naye tukaanza kutoleana maneno makali ananitukana na kusema nimekuja kula au msibani, nikakasirika saa tulikuwa tunajibizana kwa sauti ya juu ila sababu sauti ya muziki ilikuwa juu watu walikuwa hawasikii.

Wakati naendelea kulumbana nae ghafla muziki ukazima na nikaongea kwa sauti 'hizo nyama mnazibania ili mmzike nazo marehemu au' umati wote ukageuka kunitazama, ghafla wazee wa mila wakasema huyo kijana akamatwe na apigwe. Nilipigwa nilipigwa jamani nilipigwa na nikaondolewa pale bila kula licha ya kufanya maandalizi ya msiba na usafi.

Niliumia bega la kushoto kuna mtu alinipiga na kitu chenye ncha kali ila nashukuru hali ilienda sawa na nikapona ila siwezi kusahau siku ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuuuh pole sana bro
 
Ndo uache sasa uroho wako wa nyama kaka
 
Daah! mnasubiri mtu afe, mnamkatia tamaa kabisa, kwakweli kuna watu wakatili sana, mbaya zaidi mkachinja ng'ombe watatu, hivi si bora mngempeleka akafie hata hospitali kwa kuuza hizo ng'ombe, tena yawezekana asingekufa.
Siyo poa kwakweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu una sura ya kisukuma kama ndiyo wewe kwenye avatar.
 
Hahaaa ,ww jamaa story zako ,kwahiyo mliandaa msiba kabla jamaa hajafariki

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu misiba mingi ya wajanja hufanyiwa maandalizi.

Mtu kama amefikia ukomo wa maisha waufuzaji lazima wajue, hasa vifo vya watu wazima.

Hata hayati Mwalimu Nyerere maandalizi ya mazishi yake tulianza kuyaandaa kabla hajafariki mwezi mzima nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii KORONA itatuletea mengi: KORONA ondoka watoto warudi shule😁
 
Niligundua ni kua uyu Mtanesco mgombea wa Ukuu wa wilaya ni jamaa flani ivii smart tu kichwani na anajielewa vizuri kabisa, ila kwa makusudi kabisa kaamua kujichetua katika Mada/thread zake ili apate Attention au watu waweze kumjadili kwa namna yoyote ile. Kiufupi kaamua kuusaka Umaarufu umu JF kwa staili yake hii.
Angalieni Uandishi wake utaona kuna flow na uandishi mzuri tu ila stori anayosimulia ndo anazingua.
Kwahiyo uyu jamaa ebu tumpuuze tu ni Attention seeker
 
Back
Top Bottom