Nilipigwa na kufukuzwa Msibani

Nilipigwa na kufukuzwa Msibani

Kumbe ndo ww yule jamaa tulokushushiaga kipigo

Yess bishoo hasWaaaa
 
Mwaka fulani kijiji kulitokea msiba wa mzee mmoja hivi mkubwa na aliyekuwa na mali nyingi hasa mifugo, nyumba na viwanja. Sasa vijana tukaitwa siku moja kabla ya msiba ili tujiandae na tuwe tayari kwa lolote, tukapewa majukumu ya kuhakikisha usafi umefanyika mazingira yote na maji yapo ya kutosha baada ya hapo tukarudi nyumbani kukaa na kusubiri yule mzee afe.

Majira ya saa 11 asubuhi akaja kiongozi wa vijana nyumbani akanigongea na kusema msiba tayari twendeni, basi tukaanza kukusanyika ile timu ya vijana na kweli tukakuta yule mzee kafariki tukaanza kazi zetu kila mmoja na majukumu yake.

Walichinja ng'ombe watatu siku hiyo na mziki uliletwa pale mambo yote yakawa yanaenda vizuri na watu wakaanza kula, sasa wakati wanagawa chakula akaja kijana mmoja na bakuli ambalo halikuwa na nyama za kutosha nikiwa naongea naye tukaanza kutoleana maneno makali ananitukana na kusema nimekuja kula au msibani, nikakasirika saa tulikuwa tunajibizana kwa sauti ya juu ila sababu sauti ya muziki ilikuwa juu watu walikuwa hawasikii.

Wakati naendelea kulumbana nae ghafla muziki ukazima na nikaongea kwa sauti 'hizo nyama mnazibania ili mmzike nazo marehemu au' umati wote ukageuka kunitazama, ghafla wazee wa mila wakasema huyo kijana akamatwe na apigwe. Nilipigwa nilipigwa jamani nilipigwa na nikaondolewa pale bila kula licha ya kufanya maandalizi ya msiba na usafi.

Niliumia bega la kushoto kuna mtu alinipiga na kitu chenye ncha kali ila nashukuru hali ilienda sawa na nikapona ila siwezi kusahau siku ile.

Sent using Jamii Forums mobile app

Walikupendelea sana, ilibidi wewe ubakwe tu ili ushike adabu.
 
kufa nawe na wenzako wakale nyama😳 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom