Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Asante dada yangu niombee niweze kuzuia hii chuki na majuto.
 
Asante dada naomba neno lako likawe baraka kwangu
 
Amen nitaufanyia kazi ushauri wako ndugu
 
Bonge la point
 
Kitu nilichojifunza in life, kila binadamu anabadilika na haijalishi utawapa nini ambacho unadhani kitawafunga in life lakini wakikutana na watu au mazingira mengine watabadilika tu.. so, usijilaumu kwa kuwa mwema au kuyalaani maisha yako maana ndio uhalisia wa dunia ilivyo

Pia Pole sana maana naelewa unachokipitia lakini usijilaumu kwa yaliyotokea au kwa ulivyopoteza maana mara nyingine maisha hutufundisha masomo tunayoyahitaji kwa njia ngumu sana kama yako. hivyo Jifunze kwa ulipokosea na uanze kuhesabu kila baraka iliyobakia katika maisha yako na utajifunza kuyapenda tena kama yalivyo.

Naamini utakaa poa brother
 
Asante mkuu natamani ningejua ya kesho nikakwepa kuonana nae ila haisaidii mwenzangu leo anafuraha mimi ninamajuto
Hakuna ajuae kesho yake na kupotea njia ndio kujua njia. Na wengi wetu huwa tunaamini yaliyotokea ni mipango ya Mungu, hivyo ni sehemu ya mitihani ya dunia. Msamehe kwa yaliyotokea, huwezi kujua pia Mungu amekupangia nini kurudisha furaha yako.
Mshukuru Mungu kwa kila jambo.
 
Asante ni kweli naumia sana ndugu yangu, na najutia sana kukutana nae namasikitiko mengi ila haisaidii kitu
Mkuu yameshatokea huwezi rudisha wakati nyuma.msahau,samehe move on na maisha yako
Jiweke karibu na Mungu atakulinda,atakubariki,atakuinua kwa viwango vingine.una ulemavu wa sikio na mguu sio wa akili.bado una uwezo wa kufanya mambo makubwa
Utafanikiwa,utapata mke mwema,utapata familia bora..yote yanawezekana ukiamini na kumtanguliza Mungu.
Samehe jifanye mjinga ili uruhusu baraka zitue katika maisha yako.
 
Mkuu napenda kusamehe ila hali yangu kila nikijiona naona nakuwa na moyo mzito kusamehe na kusahau

Kusahau haiwezekani ila kuweka kinyongo na chuki kwa mtu asiyejali maumivu yako ni sawa na kujiumiza mwenyewe kama unavyofanya sasa.
Yeye kashaendelea na maisha yake na wewe inakupasa kufanya hivyo pia yaani hakuna njia nyingine

naelewa Kitu kibaya kuhusu watu wema kama wewe ni kudhani kila binadamu ana utu na wema kiasi cha kutokuweza kuendelea na maisha yake akimuumiza mtu.. Si kweli kabsaa maana kuna watu hawajali maumivu ya watu wengine, Cha msingi usijiumize walq kujidhuru kwa ubaya wa mtu mwingine. Jitahidi uendelee na maisha yako na yeye atanyooshwa na maisha yake mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…