Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Chapati 2

Senior Member
Joined
Dec 11, 2020
Posts
137
Reaction score
295
Habarini,

Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.

Mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.

Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.

Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.

Siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.

Sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango.

Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.

Baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.

Baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu...

Baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.

Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

Ewe maisha, nilikukosea nini?
 
Pole broo .....lakini mbona kila siku tunawaambia humu kuwa mwanaume ishi maisha yako kwanza mbona hamuelewi.....? Tatizo ni ubishi na kujiona nyie ndio romantiki sana kushinda babu zenu na baba zenu....! Inauma sana ila ndio ishakuwa tutafanyaje sasa ...
 
Umeongea kwa hisia sana mkuuu.. Maisha ndivyo yalivyooo mi naomba unisaidie kufikiria haya
1: mpka unaajiriw na kumfumania huyo mwanamke. Nini kilkushawishi kuw singo!!? Na sasa unaishi vipi hapo ulipo?
2 : huu ukarib kati yake na salim uliUpandikiza vipi katk mazingira gani?
3 : maisha inabid yaendleee huo ulemavu umepunguza nin katika taaluma yako uliyoisomea nje ya kutembea!!? Unasahau!!?
4 : huyo aliyetaka kuolew ni nani!!? Au stor imeanz mbele kurud nyuma?
 
😢😢😢😢

Kama ni kweli!huyo dada atakuja kupata tukio hevi sanaaaa labda afanye toba na kukuomba msamaha.

Ninachoamini hakuna mtu anaeweza kumlipa binadamu mwenzie mateso baada ya wema aliotendewa aka endelea kubaki salama..hakuna.

Nimejikuta napata uchungu sana.

Namshukuru Mungu kwa hivi nilivyo mpka sasa.

Pole ndugu yangu.tiba kubwa unayotakiwa kuifanya ni kumsamehe..najua kiubinadamu ni kazi sana kumsamehe mtu aliyeujeruhi moyo wako.lakini hakuna namna samehe tu maana ndipo iliponjia ya uponyaji.

😥😥😥😥😥
 
Pole mkuu kwa yote naamini MWENYEZI MUNGU mwingi wa rehema atakupigania ana kusudi na we we ndio maana upo hata Leo hii usikate tamaa yalishapita hayo huwezi kubadilisha chochote ukiendelea kuyaweka akilini ni kujitafitia tatizo zaidi,jiamini weka mipango mipya utavuka inshalah
 
Pole broo .....lakini mbona kila siku tunawaambia humu kuwa mwanaume ishi maisha yako kwanza mbona hamuelewi.....? Tatizo ni ubishi na kujiona nyie ndio romantiki sana kushinda babu zenu na baba zenu....! Inauma sana ila ndio ishakuwa tutafanyaje sasa ...
mkuu laiti ningejua kesho yangu nisingeomba kukutana nae ila ni Mungu ndio anaeijua kesho yetu.
 
mkuu salim alikuwa rafiki wa ukubwani tu na tulitokea kuzoeana kutokana na kukaa karibu, urafiki ulitokea baada ya yeye kuona nipo karibu na salim hivyo wakazoeana kama mashemeji ili ikitokea sipatikani basi salim anaulizwa nipo wapi.sio ulemavu wa mguu tu mkuu naulemavu wa masikio pia
Umeongea kwa hisia sana mkuuu.. Maisha ndivyo yalivyooo mi naomba unisaidie kufikiria haya
1: mpka unaajiriw na kumfumania huyo mwanamke. Nini kilkushawishi kuw singo!!? Na sasa unaishi vipi hapo ulipo?
2 : huu ukarib kati yake na salim uliUpandikiza vipi katk mazingira gani?
3 : maisha inabid yaendleee huo ulemavu umepunguza nin katika taaluma yako uliyoisomea nje ya kutembea!!? Unasahau!!?
4 : huyo aliyetaka kuolew ni nani!!? Au stor imeanz mbele kurud nyuma?
 
dada yangu najitahidi kuwa na moyo wa kusamehe ila hali yangu ya ulemavu na majuto yananiumiza na kunitesa mimi siwezi sahau na kusamehe nimejitahidi nimeshindwa

Back
Top Bottom