Njemba Soro.
JF-Expert Member
- Oct 5, 2013
- 4,281
- 7,476
Habari....
Ilikuwa mwaka fulani msimu wa kilimo mvua ikaacha kunyesha. Sasa plan B ili mazao yasikauke ni kutumia mifereji inayotoa maji mtoni. Mwenyekiti wa kijiji akaleta utaratibu wa kihuni na kupendelea zamu za kumwagilia. USIKU NIKAWA NAENDA KUJIFUNGULIA MAJI BILA RUHUSA.
Aisee siku moja jamaa wakaniwinda wakanikamata, na walijua ni mimi maana shambani kwetu kulikuwa na maji bila zamu kufika na mahindi yamesitawi tofauti na majirani. Nilipigwa rungu la kichwa ghafla nikajua hapa nikishindana hawa jamaa wapo wengi wananiua.
NIKAJIFANYA NIMEKUFA, NIKAPIGAPIGA MIGUU NIKAJINYOOSHA KAMA NIMEKUFA. Jamaa walikimbia mbio za ajabu nikaamka nikafungulia maji kuelakea kwetu nikamwagilia hadi asubuhi, nilibakiza sehemu ndogo sana ya shamba letu ndipo wakaja kucheki wakakuta sijafa na nimekaribia kumaliza shamba. Wakalalamika sana kwa baba yangu lakini mimi nikasema nilikuta maji shambani nikaanza kumwagilia mahindi....
WALE WAZEE WANNE WAMESHAKUFA NA WENGINE NI WAZEE SANA KWA SASA ILA NI WASHKAJI ZANGU SANA.