kiss ov love
JF-Expert Member
- Jan 21, 2025
- 9,388
- 16,188
Asante sana nashukuru Mungu hakutumia mabavu tulikuwa tunabishana sana na mimi nilikuwa mkali pia naona ilisaidiaPolee sana Mkuu, kikubwa hukufanyiwa ukatili huo
Yaani hilo siwezi kurudia kabisaKama haumpendi mtu usiende geto kwake. Hakuna urafiki wa watu walio balehe na mavuzeeeerrrr kibao
kwamba unaenda kwenye chumba cha mwanaume na hujui anachohitaji? hukwendea hili? tangu lini mwanaume akawa rafiki wa mwanamke? never. pia, hivi unafikiri unaongea na watoto? kwamba tuamini ulitoka bure na akakupeleka kwa gari yake hadi kwenu. acha uzinzi, ni dhambi, itakugarimu, mpokee Yesu na uache dhambi au la ujinga wako hauna mwisho mwema.Kuna kijana alikuja kupata huduma ofisini kwetu akawa amechukua namba yangu yeye ana ofisi yake huko town anauza viatu vya kike.
Mwanzoni alikuwa mpole tukawa tunawasiliana vizuri tu, kwa vile ana ofisi yake nikajua atanipa ushauri mzuri wa biashara na kujiajiri hivyo nikawa nimemuamini, na kumchukulia kama kaka au rafiki wa kiume.
Ikatokea siku akanialika kwake nikitoka kazini, kwakuwa siyo mbali na ofisini kwetu nilivyotoka nikaenda, tukakaa tukapiga story tukala chakula, baada ya hapo nashangaa mtu mara anisogelee atake kunishika, akaninyanyua kanipeleka chumbani weee hapa nilibadilika nikawa mbogo, maana mimi sikujia hayo mambo iweje atake kunibaka bila ridhaa yangu kisa nimekuja kwake ndiyo aone kuwa nimekubali kila kitu.
Tulivutana sana hiyo siku nakumbuka, mimi hadi nimefura kwa hasira ndiyo kumlazimisha akanipeleka home maana ana usafiri wake, tangu hiyo siku nimetoka sijapokea simu yake wala kujibu meseji zake, nimemuona ni mwanaume wa hovyo sana tangu lini mapenzi yakalazimishwa? Mwache mwanamke akupe kwa kuridhia mwenyewe.
Mimi nimeshangaa sana huyu kijana kwanza anaonekana ana mademu kibao nikajua mimi atanichukulia kama mdogo wake tu loh! Kumbe alikuwa ananipigia mahesabu nikimaliza kula kitimoto anile na mimiPole sana, mtu asiye Kaka yako wa damu kwenda nyumbani kwake mmm hata siwezi kabisa, wanaume wakati mwingine akili huwa inahama kama kabisa, sasa wewe na mkia wako mkae wawili dhubutu yake!
Mshenzi sana huyu kijana kwanini hakuomba tangu sijafika si wenzie ndiyo huwa wanafanyaga hivyoYeye Alijua mbuzi kafia kwa muuza thupu
Mimi sijapoteza kitu maana sijawahi kuwa na hisia naye kabisaLakini na nyie mnazingua! Eti nilimuona kama kaka yangu au rafiki wa kiume ... nilienda anipe ushauri wa jinsi ya kujiajiri.... Mweeeh! Hakuna kitu kama hicho. Nyote mlizingua! Na yeye angekuandaa na kuchukulia fursa kutega nyavu akunase kimasihara! Ona sasa, kamwaga mboga, wewe ugali! Mmekosa nyote!😝