Nilimpa mtaji mzazi mwenzangu ili asinisumbie kulea mtoto ila sasa kaanza kuomba hela ya matumizi tena

Habari za mchana WanaJF,

Nilikuwa naomba ushauri nini sahihi cha kufanya maana miezi kama mitatu imepita mzazi mwenzangu alikuwa anaomba pesa ya matumizi ya mtoto mfululizo mara mtoto anaumwa kwa wiki mara 3.

Kwanza kabla ya hapo mtoto alikuwa anaumwa mara kwa mara nikahisi ananipiga pesa tu nikaacha kutuma pesa kuna doctor mmoja ni rafiki wa baba yangu so nikaongea na doctor.

Halafu nikamwambia mzazi mwenzangu mtoto akiumwa asinipigie simu ampeleke tu moja kwa moja hospital na achukue dawa hapo hapo lakini kuanzia hapo mtoto akapona hakuwa anaumwa tena.

Sasa leo kama miezi mitatu imepita baada ya kukubaliana nimpe mtaji ili asinisumbie kulea mtoto ila sasa naona kaanza kuomba hela kwa kasi ya ajabu.

Leo asubuhi kanitumia sms asubuh anataka hela ukwel nilipanic nikamporomoshea matusi makali lakini nimekaa sijui nifanye nini.

USHAURI WENU NINI NIFANYE KUFUTA TATIZO HILI.

ASANTE
Kisheria unatakiwa uwekwe hata ndani, maana mnazalisha kizazi mnachoshindwa kukihudumia mnaleta majambazi, maana yake usipo mpa mtoto mahitaji anakua teja na omba omba in the end anakua jamabazi, muwe mnawajibika kutunza watoto wenu kama mnavyowajibika kukata viuno kwenye kumtafuta
 
Kasema tayari ana familia inamana huyo n mchepuko wake....
Kwani mchepuko si kamzalia mtoto mzee, mnazalisha watoto wa watu mnasema michepuko, mchepuko awe burudani ya muda huo tu lakini sio mnawazalisha na kuanza kuwakimbia, hivi damu yako (mtoto wako) utaiita ni ni damu ya mchepuko, hichi kizazi kina laana eti
 
Hiyo ni consequence ya zinaa,haikwepeki, itakusakama mpk unaingia kaburini,salama yako muombe huyo mwanamke mrudiane,then muombe toba kwa uzinzi wenu,muoane then muanze kuishi maisha ya kumtukuza Mungu kwa kudhamiria...
Kuna mda mnataka kuifanya jf iwe kama fb
 
Nikukumbushe pia hyo biashara isingeweza kusimama wakati anategemea hyohyo maana faida badala ya kupanuka faida yote anaitumia, sa we ulitegemea hyo biashara ikueje,naona n makosa yako siku nyingine ukimpa mtaji msimamie wakati huo unaendelea kutuma matumizi ikishakuwa kiasi cha kutegemea hela ya hko ndo uje useme nilimpa mtaji akaula,nadhani kwa wafanya biashara mnanielewa yaani kwa navojua mtoto anamatumizi makubwa hata kama haumwi na unajua biashara ipanuke inachukua mda mpaka mwaka(wateja wakuzoee lakini faida inayopatikana unaongeza mzigo)sasa wewe unakula faida unategemea biashara ikue kweli?na nna uhakika mpaka amekuja tena ujue amezidiwa na inawezekana mama mtoto wako anakula mlo mmoja ila we hujui,do something pls
 
Itabidi nimpeleke kwa Bibi ake akapambane nae tu aisee najilaumu nataman nikikate hichi kidudu
Wakati mnatongozana na kutiana mimba bibi mlimshirikisha na akakubaliana nanyi? Acheni kuwatwisha mizigo wazazi wenu bila sababu za msingi, unless you are both dead.
Usiweke mbegu zako mahali ambapo hupahitaji, ni lini mtaamka na kutumia akili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi ya wanaume wengi wanadhani kupokonya watoto ni suluhisho

Kumbe wanazidi kumuumiza mtoto kihisia

Mtoto anatakiwa apate malezi ya baba na Mama

Imeshindikana Basi apate malezi ya mzazi mmoja (hasa mama Kama mtoto bado mdogo, labda tu Mama awe hajielewi)

Washirikiane kulea, mmoja alee mmoja ahakikishe mtoto anapata mahitaji

Sijui tunakwama wapi
Hongera sana kwa kuelewa hilo, mtoto huwa anapata tabu sana kuwa mbali na wazazi wake, pia ni bora mtoto akabaki na mama basi kama baba hawezi kuwa nae karibu au kukwepa majukumu na kuwapa huduma, akienda ustawi wa jamii ataulizwa mshahara wake wataugawa kiasi kiwe kinaenda kwa mtoto kila mwezi ambapo hiyo itakua ni lazima na sio ombi, lakini huyu ndugu anavyoongea ni kama hata mtoto atakua anamchukia,
 
Labda alifungua biashara akiamini itampa kipato lakin biashara imekwama... Yanatokea. ....
 
Back
Top Bottom