Habari ndugu zanguni.
Mwaka 2017 nilibahatika kupata milioni tatu katika harakati zangu. Kuna kaka yetu ambae baba alimzaa nje ya ndoa. Hakuwahi kuja kwetu mama yake hakupenda Kabisa tujuane.
Kaka huyo alikuwa hatuchangamkii Kabisa hata Kwa salamu. Niliumia sana kuona ndugu yangu hataki mahusiano na sisi Kabisa. Maisha yake yalikuwa duni Kabisa hata Nguo zake zilichanika. Nikamfuata siku Moja twende nyumbani akanifokea kabisa.
Kwa huruma zangu nikamtegeshea milioni Moja sehemu anazo pita akazíokota. Hivi sasa kapanua genge lake limekuwa kubwa Kabisa lakini bado hana haja na Mimi.
Nifanyaje na sipendi ajue ni mimi niliemtegeshea zile PESA.