Nilimpa milioni moja lakini ananichukia

Nilimpa milioni moja lakini ananichukia

Nguva Jike

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
1,292
Reaction score
1,867
Habari ndugu zanguni.

Mwaka 2017 nilibahatika kupata milioni tatu katika harakati zangu. Kuna kaka yetu ambae baba alimzaa nje ya ndoa. Hakuwahi kuja kwetu mama yake hakupenda Kabisa tujuane.

Kaka huyo alikuwa hatuchangamkii Kabisa hata Kwa salamu. Niliumia sana kuona ndugu yangu hataki mahusiano na sisi Kabisa. Maisha yake yalikuwa duni Kabisa hata Nguo zake zilichanika. Nikamfuata siku Moja twende nyumbani akanifokea kabisa.

Kwa huruma zangu nikamtegeshea milioni Moja sehemu anazo pita akazíokota. Hivi sasa kapanua genge lake limekuwa kubwa Kabisa lakini bado hana haja na Mimi.

Nifanyaje na sipendi ajue ni mimi niliemtegeshea zile PESA.
 
Ulikosea kumtegeshea, ungempa ajue ili akuheshimu pengine angekuwa anakuthamini, maake maisha ya Sasa bila pesa huthaminiwi.
Nimejitahisi kumvuta tukutane amekuwa akinikwepa hataki kuwa karibu halafu anafanana sana na baba kuliko hata sisi
 
Muulize tu vpi biashara inaendeleaje?,ile milioni imemsadia kupiga hatua?,akiuliza milioni gani?,mpe ukweli..
 
Hii sasa ndio mitego ya kutegesheana, Mkuu nikupe namba unitege.
Huu ni mtindo Wangu huwa nacheka kimoyomoyo na kufurahi Sana PESA au kitu MTU ninae mlenga.[emoji1]
 
Ulimtegeshea ndio.
Unataka afanyeje akulambe miguu?

Utalipwa na Mungu
 
Back
Top Bottom