Nilime nini kati ya nanasi, machungwa, maembe na mapapai?

Wana jf wengi wanalima kwenye keyboards na kwenye smartphone. Kwa bei ilivyosokoni Leo wananunua kwa bei ya jumla 1000 liwe kubwa liwe dogo .
Huwezi kujua faida na hasara za kilimo kama hulimi ,kama hutembelei wakulima wenzako.

Katika tafiti zangu Papai ni rahisi kulima kilimo mazao mengine na huwezi kutosholeza soko LA Papai maana kuna kiwanda bagamoyo wananunua kwa Tani
 
Wow! Hii ni habari njema kwa wakulima wa papai. Vipi bei yake hapo kiwandani ikoje, ndio hiyohiyo 1000 au pungufu?
 
Mapapai hapana mpendwa wangu. Labda kama wewe ni risk taker.
Yanaweza kukupa pressure. Hasa ikitokea bahati mbaya inyeshe mvua ya mawe, uwiiiii.
Halafu pia yana ugonjwa fulani yanadonolewa yakishazaa.
Mengine unaweza kulima, kwanza yanasoko (Azam ni mnunuzi mzuri kama una mzigo mkubwa)
Comments zingine ni hatari mbona Mimi nalima Papai mwaka wa tatu sijakutana na changamoto unazoandika hapa? Au hujawahi kulima umesimuliwa?
 
Kabla hujafanya lolote ,tambua wazo lako ,jua changamoto za kila zao,fanya kautafiti,ka kina wewe mwenyewe ,pima udongo wa shamba lako anza kazi
 
Mapapai hapana mpendwa wangu. Labda kama wewe ni risk taker.
Yanaweza kukupa pressure. Hasa ikitokea bahati mbaya inyeshe mvua ya mawe, uwiiiii.
Halafu pia yana ugonjwa fulani yanadonolewa yakishazaa.
Mengine unaweza kulima, kwanza yanasoko (Azam ni mnunuzi mzuri kama una mzigo mkubwa)
Mbona mnatunchanganya! sI Mnasemaga Juice za SSB ni feki na kwamba sio matunda halisi?
 
Kabla hujafanya lolote ,tambua wazo lako ,jua changamoto za kila zao,fanya kautafiti,ka kina wewe mwenyewe ,pima udongo wa shamba lako anza kazi
Shukrani kwa ushauri wako
 
Asante kwa ushauri wako! Kama hutajali waweza share na mimi kuhusu kilimo cha mbogamboga?
Kilimo cha mbogamboga ni moja kati ya kilimo rahisi kulima lakini kigumu kwa maana yakikifanya biashara

Moja kilimo cha mbogamboga kwa maana yakukifanya kuwa biashara yako kinakuitaji mda mwingi kuwepo bustani ivyo iliuweze kulima mboga mboga kibishara uwe na mda wakutosha kuzihudumia

Pili uwe na maji ya uhakika kwani kinategemea sana maji kwa mfano mchicha ni moja ya mboga zinazoitaji maji mengi

Tatu uwe na mbolea ya samadi pia mbolea ya viwandani kama kani ni nzuri sana kwa kupandia kwani inafanya mboga kuwa na afya nzuri, pia uwe na eneo zuri lisilo nakivuli na lenye rutba nzuri yakustawisha,

Nne, SOKO hapa niongee kwa experience yangu kwani ni kitu ambacho nimewai kukifanya kwanza kabisa mbogamboga zinamsimu wake kwa mfano kipindi cha kwanzia mwezi wa saba hadi tisa kwendea kumi mbogamboga ni nyingi sana watu wengi wanalima mboga ivyo kupelekea bei kuwa ovyo sana sokoni hii kwa wewe mlaji utoona hapa tunaumia tu niwakulima kwani hata mboga ziwenyingi vipi wauzaji kwenye vibanda wataendelea kuuza bei ile ile fungu kwa mia tano,

Shida inakuja kwetu sisi wakulima mboga sinakuwa nyingi mashambani tunalazimika kuuza kwa bei ya chini sana tena kwa kuombea maana kila mtu anakuwa amelima, hiki kipindi wanalima watu wengi kwa sababu ya maji yanakwepo mengi ya mvua yaliotwama kwenye mabwawa,
Hivyo basi kwa ushauri wangu ukitaka kilimo cha Mboga Mboga kiwe na tija kwako nibora kabisa ukawa na soko la uhakika lakuuzia ndio uanze kulima kwa mfano unaweza ukaenda labda kwenye mashule wanayokula mboga, mahotelini, na hata kwenye masoko ukafanya tafiti na kupata mtu ambaye atakuakikishia kununua mboga zako ndio uanze kilimo serious kwa ajili ya Biashara,

Nimalizie kwa kusema kilimo cha mbogamboga ni kizuri kwani hata kikikupa hasara sio kubwa Sana kulinganisha na mazao mengi labda mda wako utakaokuwa umepoteza pia nikizuri ukikosa wateja unakula unajenga afya yako, japo unakuwa ujafikia lengo lako pia mtaji wake ni mdogo

Zingatio: uchambuzi huu ama uzoefu wangu nimeutolea kwa jiji la dar,
 
Nakushauri lima Papai hasa hybrid
1.miezi 8 unaanza kuvuna mfululizo hadi miaka 3
2.haishambuliwi na wadudu hasa Miche niliyonayo
3.haina gharama za matunzo zaidi ya maji palizi na Mbolea
4.utawahi kurudisha gharama tofauti na mazao mengine.

5.mipapai mmoja matunda hadi 120
Heka moja mipapai 1200

Piga hesabu za roughly kila mwezi uvune matunda 700x500 =350,000 kwa mwaka ?
Uje nikuuzie Miche
Pia pita masokoni uulize Papai wananunua bei gani
0755404226 dsm kiluvya
Mkuu naomba kujua bei ya mche kwa iyo mbegu ya hybrid
 
Wasalaam!
Waungwana naombeni ushauri wa zao linalostawi zaidi kwa mikoa ya Pwani/ Tanga na lenye faida kwa mkulima. Zao lipi linafaa zaidi kati ya nanasi/ machungwa/ maembe mapapai?
Natanguliza shukrani

Lima machungwa mkuu,ukishapanda baada ya miaka minne unaanza kuvuna adi unakufa (kwa mwaka unavuna mara mbili). Gharama ni kutunza michungwa,kupalilia,dawa incase wadudu watavamia. Ni hayo tu.
 
Lima machungwa mkuu,ukishapanda baada ya miaka minne unaanza kuvuna adi unakufa (kwa mwaka unavuna mara mbili). Gharama ni kutunza michungwa,kupalilia,dawa incase wadudu watavamia. Ni hayo tu.
Asante kwa ushauri murua. Hiyo ni michungwa ya asili au hata ya kisasa itakuwa jumla?
 
Back
Top Bottom